CCM vs Dkt. Bashiru: Nini kinaendelea?

CCM vs Dkt. Bashiru: Nini kinaendelea?

Mimi nilimchukia sana Bashiru enzi za mwendazake zake kwa ushenzi waliofanya,lakini nimemkubali sana juzi kwa jinsi alivyowajambisha maccm.
 
UKIONA VYAELEA, UJUE VIMEUNDWA walisema wahenga wa zamani. Tumeshuhudia press ya Dk Bashiru na baadaye viongozi mbalimbali wakipinga vikali msimamo wa aliyekuwa katibu mkuu wa CCM. Tukio hili linafanana kwa ukaribu na tukio la kujiuzulu kwa aliyekuwa Spika baada ya shinikizo Kali kutoka kwa wanachama.

Hivi majuzi tulishuhudia aliyekuwa Spika wa bunge akijiuzulu kufuatia "kumkosoa hadharani "Mwenyekiti wa Chama hicho. Hatukuona hoja za kufafanua au kumjibu badala yake tuliona akishambuliwa na kila kiongozi wa chama.

Je, tutegemee kuyaona ya Spika mstaafu? Au Ndugu Bashiru ataweza kutikisa kiberiti? Je ni kosa la jinai kuhoji utendaji kazi wa Serikali? Au ni hangover za kukosa madaraka? Au ni mkakati wa kutusahaulisha yanayoendelea (umeme na maji)?

ALL in ALL, strategist wa CCM anastahili pongezi kukaa madarakani 61yrs sio utani.
Katibu wa ccm kusema ya moyoni alikuwa ndg Kolimba (RIP) aliposema Chama kimepoteza dira.Wote tunakumbuka yaliyomsibu mara tu baada ya kuhojiwa na chama chake.Lakini nawe Bashi ungelisema nadhani viongozi tumekosa kutowashukuru wakulima na wafanyakazi kutuwezesha kutekeleza majukumu yetu.Maana nawe ulikuwa huko
.
 
Bashiru ni mlafi wa madaraka, chama kinamtwanga vilivyo
SSH amefanya sana uungwana angeweza kummwaga mazima baada ya kutangaza baraza la mawaziri.

SG walijificha mwanzoni lakini wameamua kujiweka wazi kabisa kwamba wanapambana na SSH. Walimtumia Mpina bungeni kama askari wa siri lakini sasa wameinua kabisa silaha tayari kwa mapambano.
 
Bashiru alisema nini . Mimi niliona kama vile amesema Serikali ikifanya wema hakuna sababu ya kusema asante kwa vile ule ni wajibu wa Serikali.
 
Bashiru alisema nini . Mimi niliona kama vile amesema Serikali ikifanya wema hakuna sababu ya kusema asante kwa vile ule ni wajibu wa Serikali.
Ndiyo, kauli hiyo iliwakera vijana wa UVCCM
 
ccm ni ukoo wa mafisi... waliwanyonyoa makatibu wao wakuu (Makamba na Kinana) kwa nyati fulani... Wakawanyamazisha wenyeviti wao (Mwinyi, Kikwete na Mkapa)... Wakanyonyoa spika wao... Na sasa wanashughulika na Bashiru wa ccm.
 
Bushiru anajenga utamaduni wa uwajibikaji ambao hauna cha kurudisha ASANTE. Hivi nikienda ofisi ya mtendaji akanihudumia vizuri na nisimsifu kuwa wewe ni mtendaji mzuri atachukia kwa vile sikumpa sifa hiyo,sidhani huo utakuwa ni wajibu wake ametekeleza?
 
Back
Top Bottom