CCM vs Dkt. Bashiru: Nini kinaendelea?

CCM vs Dkt. Bashiru: Nini kinaendelea?

Girland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2016
Posts
2,489
Reaction score
4,253
UKIONA VYAELEA, UJUE VIMEUNDWA walisema wahenga wa zamani. Tumeshuhudia press ya Dk Bashiru na baadaye viongozi mbalimbali wakipinga vikali msimamo wa aliyekuwa katibu mkuu wa CCM. Tukio hili linafanana kwa ukaribu na tukio la kujiuzulu kwa aliyekuwa Spika baada ya shinikizo Kali kutoka kwa wanachama.

Hivi majuzi tulishuhudia aliyekuwa Spika wa bunge akijiuzulu kufuatia "kumkosoa hadharani "Mwenyekiti wa Chama hicho. Hatukuona hoja za kufafanua au kumjibu badala yake tuliona akishambuliwa na kila kiongozi wa chama.

Je, tutegemee kuyaona ya Spika mstaafu? Au Ndugu Bashiru ataweza kutikisa kiberiti? Je ni kosa la jinai kuhoji utendaji kazi wa Serikali? Au ni hangover za kukosa madaraka? Au ni mkakati wa kutusahaulisha yanayoendelea (umeme na maji)?

ALL in ALL, strategist wa CCM anastahili pongezi kukaa madarakani 61yrs sio utani.
 
Mkuu, wamemfunga kamba na kumwacha azurure, kwa nukuu ya KM Taifa.
😃😃😃Hiyo clip ni ya muda kidogo, ilikuwa 2021 Kama sikosei unless walimtarget kitambo.
 
Bashiru akirudi CUF anaweza kuwa candidate mzuri sana kama prof Lipumba hatakuwepo ndani yake. Anaweza kusumbua mno, wasije kumruhusu icho kitu, ama la, wakumbushie ile issue za kigogo kwamba walikwapua mipesa kipindi jiwe amekufa ili wamburuze nalo kwa uhujumu uchumi. awe makini.
 
Bashiru ni mlafi wa madaraja, chama kinamtwanga vilivyo
Wakiwa nje ya mfumo akili zinawarudi, Uliona kipindi ndugu yetu wa mtama alivyokuwa back bencher? Alikuwa mnyenyekevu mno!

Polepole na Bashiru baada ya kukosa ulaji wanapayuka 😁😁
 
bashiru akirudi CUF anaweza kuwa candidate mzuri sana kama prof Lipumba hatakuwepo ndani yake. anaweza kusumbua mno, wasije kumruhusu icho kitu, ama la, wakumbushie ile issue za kigogo kwamba walikwapua mipesa kipindi jiwe amekufa ili wamburuze nalo kwa uhujumu uchumi. awe makini,
Nachojiuliza hii sio movie? Maana CCM washatujulia watanzania!
 
Nachojiuliza hii sio movie? Maana CCM washatujulia watanzania!
inaweza kuwa movie, na inaweza kuwa sio movie. ila kuwa movie ni possible zaidi kwasababu sidhani kama bashiru hana madudu anayoogopa watafukua makaburi akileta kiburi, lazima atakuwa na kitu cha kumfyatisha mkia, ukiona ana ujasiri ivyo, yote yanawezekana.
 
Hawa watu wanalindana Sana, Ndiyo maana nimeanza kwa kusema ukiona vyaelea ujue vimeundwa
 
Makinikia hawana chao, je 2025 watakuwa wapi? Watarudi upinzani au wataanzisha chama kipya?
Msajili wa vyama Yuko bize sana, hatasajilo chama mpaka mchakato wa katiba ukamilike
 
Makinikia hawana chao, je 2025 watakuwa wapi? Watarudi upinzani au wataanzisha chama kipya?
Mtihani mzito sana hui kwao. Maana huko upinzani kwenyewe, walinyea kambi.

Binafsi nawashauri waanzishe tu chama chao, ili waweze kupata wanachama kwa urahisi kutoka pande zote mbili! (upinzani + ccm)
 
Mtihani mzito sana hui kwao. Maana huko upinzani kwenyewe, walinyea kambi.

Binafsi nawashauri waanzishe tu chama chao, ili waweze kupata wanachama kwa urahisi kutoka pande zote mbili! (upinzani + ccm)
Waanzishe chama afu nani akisajili? ingekuwa hiyo ni rahisi mbona tungekuwa na vyama buku leo hii.
 
Wala hakuna vita. Ni CCM mpya iliyojengwa katika kusifu na kuabudu maarufu “chawa” vijana wanawaza kusifia kupata teuzi na kuheshimisha matumbo yao.
 
Nachojiuliza hii sio movie? Maana CCM washatujulia watanzania!
Mkuu una mawazo likewise, yaani ukute kuna jambo wanatupoteza as issue ya mgao wa Maji, Umeme, Chakula.

Walikuja na issue ya dogo wa uokozi, dogo alipoingia chuo wakaibuka na bashiru.

Yaani hii nchi kama haupo makini unashangaa mara mwaka umeisha na viongozi ni wale wale!
 
Back
Top Bottom