Gentleman,View attachment 3205616
Tukiwa katikati ya mtanange mkali wa kidemokrasia wa CHADEMA ambao umetoa usawa na fursa kwenye kugombea nafasi mbalimbali hivo kupata vipaji vipya vya uongozi; CCM waliibuka na wao Dodoma kwenye mchakato wao wa kutafuta makamu mwenyekiti wa chama.
Kwa mbwembwe za msururu wa magari mapya (vinyulaa) yaliowabeba wajumbe wa CCM wakiambatana na viongozi wazito wa chama hicho, tulijua kuna jambo kubwa linaenda kutokea Dodoma ambalo halijawahi kutokea.
Kwa masikitiko makubwa, kimetokea kihoja Dodoma; mbali na nafasi ya makamu kupatikana pasipo misingi ya demokrasia ya kugawa fursa za kuchaguana kwa wote, CCM wamekuja na mzee asiyeendana na nyakati za kileo na mabadiliko makubwa ya kisiasa yanayotokea.
Nimepata huruma sana kwa wana CCM wengine ambao wao hawatoki kwenye familia za vigogo wala hawana ushawishi wowote kwenye chama; je hao watapewa lini fursa za kuonesha vipaji vyao vya uongozi kama bado kuna misingi ya demokrasia za majina ya mfukoni?
Au hawa wana CCM wengine wataishia kuwa wapagazi wa kuwabebea ma 'giants' wa CCM majembe na manyundo mpaka wanazeeka, huku wakisindikizwa na wapiga madebe akina Tlaatlaah ChoiceVariable na kamanda asiyechoka kububujika machozi Lucas Mwashambwa ?
Hii inahitaji tafakari sana, CCM msidhani kwamba kushangilia kwenu ukosefu wa misingi ya demokrasia nchini kunawanufaisha kwa chochote. Kwa misingi iliyopo ndani ya CCM wengi mtaishia kuwa wapagazi, wapambe na machawa mpaka mzeeke.
What a waste of time.
Hahahahah umenichekesha sana.. watoto wa wapagazi wakipendelewa sana ni JKTHakika panya wanajuana, watoto wa wakulima wanapelekwa jkt
Soon ubunge utampitia.Nina mshikaji wangu huyu bwana
1. Ni HR wa Halmashauri X
2. Ana Masters ya MBA in HR
3. Mpiga kazi balaa
Sasa bwana kwenye chama cha CCM ...
1. Yeye kila mwaka ana jezi mpya
2. Hakuna event ya CCM ya mkoa au wilaya asihudhurie
3. Kaenda mara kibaoo kwenye mikutano ya Chama Dodoma
Ila sasa ....
Sio kiongozi yoyote, huwa namwambjaga kuwa "braza huko unapotea na kupoteza muda, CCM ina wenyewe na walio wenyewe ni hawa wenye koo za VIP au wanaojuana na hizo koo"" ila Haelwagi
Namuoneaga huruma sanaa huyu kijana wangu.
#YNWA
#YANGA_BINGWA
Idiot....James Mbowe: Lema siyo Mchagga
Ina wenyewe na wenyewe ndio haoje hao watapewa lini fursa za kuonesha vipaji vyao vya uongozi
Naaam,Ina wenyewe na wenyewe ndio hao
Ni ile ile
Ni ile ile
Ina wenyewe
Ina wenyewe
Tusidanganyane, ndani ya CCM maji hufata mkondo.Soon ubunge utampitia.
View attachment 3205616
Tukiwa katikati ya mtanange mkali wa kidemokrasia wa CHADEMA ambao umetoa usawa na fursa kwenye kugombea nafasi mbalimbali hivo kuibua vipaji vipya vya uongozi; CCM waliibuka na wao Dodoma kwenye mchakato wao wa kutafuta makamu mwenyekiti wa chama.
Kwa mbwembwe za msururu wa magari mapya (vinyulaa) yaliowabeba wajumbe wa CCM wakiambatana na viongozi wazito wa chama hicho, tulijua kuna jambo kubwa linaenda kutokea Dodoma ambalo halijawahi kutokea.
Kwa masikitiko makubwa, kimetokea kihoja Dodoma; mbali na nafasi ya makamu kupatikana pasipo misingi ya demokrasia ya kugawa fursa za kuchaguana kwa wote, CCM wamekuja na mzee asiyeendana na nyakati za kileo na mabadiliko makubwa ya kisiasa yanayotokea.
Nimepata huruma sana kwa wana CCM wengine ambao wao hawatoki kwenye familia za vigogo wala hawana ushawishi wowote kwenye chama; je hao watapewa lini fursa za kuonesha vipaji vyao vya uongozi kama bado kuna misingi ya demokrasia za majina ya mfukoni?
Au hawa wana CCM wengine wataishia kuwa wapagazi wa kuwabebea ma 'giants' wa CCM majembe na manyundo mpaka wanazeeka, huku wakisindikizwa na wapiga madebe akina Tlaatlaah ChoiceVariable na kamanda asiyechoka kububujika machozi Lucas Mwashambwa ?
Hii inahitaji tafakari sana, CCM msidhani kwamba kushangilia kwenu ukosefu wa misingi ya demokrasia nchini kunawanufaisha kwa chochote. Kwa misingi iliyopo ndani ya CCM wengi mtaishia kuwa wapagazi, wapambe na machawa mpaka mzeeke.
What a waste of life.
Kwahio WAKAZI WEIBIRO ndio atarithi kijiti cha baba yake au sio?Observe kwa makini, ni Pyramid. Waliochini watabaki humo humo tu na wajuu ndo wapogo hapo milele.
Wasira akichoka kabisa kabisa, atampa pasi mwanae..
CCM ukitaka mafanikio uwe na kipaji cha kulamba watu makalio😂 tena wale influential. Tengeneza ujamaa na watu influential ndani ya chama uone kama hutatoboa. Ukiwa shabiki mandazi bila mahesabu ya connection utazeeka bila bila.Tusidanganyane, ndani ya CCM maji hufata mkondo.
Hata hizi nafasi za kiteuzi za Raisi kama DAS, RAS, Wakurugenzi, ETC utaona kabisa huteuliwa...
1. Wale ambao wazazi wao ni wana CCM tena hasa jumuia ya wazazi
2. Wale ambao wanajuana na koo za VIP
3. Kama ni mwanamke, utakuta mumewe ni someone serikalini.
Ila eti mwalimu wa Kiswahili kutoka halmashauri X ya ndanindanii kabisaa eti ateuliwe kuwa DAS dah badoo sanaa.
#YNWA
#YANGA_BINGWA
Hiv bado nafasi za jeshi hazijatoka? Kuna watu nataka waende jeshini, You Know 😂Hakika panya wanajuana, watoto wa wakulima wanapelekwa jkt