CCM vyeo wanagawiana familia zao na uongozi wanapeana wao kwa wao; je wanachama wengine ni wapagazi wa kubeba nyundo na majembe?

CCM vyeo wanagawiana familia zao na uongozi wanapeana wao kwa wao; je wanachama wengine ni wapagazi wa kubeba nyundo na majembe?

View attachment 3205616

Tukiwa katikati ya mtanange mkali wa kidemokrasia wa CHADEMA ambao umetoa usawa na fursa kwenye kugombea nafasi mbalimbali hivo kupata vipaji vipya vya uongozi; CCM waliibuka na wao Dodoma kwenye mchakato wao wa kutafuta makamu mwenyekiti wa chama.

Kwa mbwembwe za msururu wa magari mapya (vinyulaa) yaliowabeba wajumbe wa CCM wakiambatana na viongozi wazito wa chama hicho, tulijua kuna jambo kubwa linaenda kutokea Dodoma ambalo halijawahi kutokea.

Kwa masikitiko makubwa, kimetokea kihoja Dodoma; mbali na nafasi ya makamu kupatikana pasipo misingi ya demokrasia ya kugawa fursa za kuchaguana kwa wote, CCM wamekuja na mzee asiyeendana na nyakati za kileo na mabadiliko makubwa ya kisiasa yanayotokea.

Nimepata huruma sana kwa wana CCM wengine ambao wao hawatoki kwenye familia za vigogo wala hawana ushawishi wowote kwenye chama; je hao watapewa lini fursa za kuonesha vipaji vyao vya uongozi kama bado kuna misingi ya demokrasia za majina ya mfukoni?

Au hawa wana CCM wengine wataishia kuwa wapagazi wa kuwabebea ma 'giants' wa CCM majembe na manyundo mpaka wanazeeka, huku wakisindikizwa na wapiga madebe akina Tlaatlaah ChoiceVariable na kamanda asiyechoka kububujika machozi Lucas Mwashambwa ?

Hii inahitaji tafakari sana, CCM msidhani kwamba kushangilia kwenu ukosefu wa misingi ya demokrasia nchini kunawanufaisha kwa chochote. Kwa misingi iliyopo ndani ya CCM wengi mtaishia kuwa wapagazi, wapambe na machawa mpaka mzeeke.

What a waste of time.
Gentleman,
huna haja ya kubababika wala kumbwelambwela,

Mbona iko wazi sana,
Ukiwa CCM, kadiri umri unavyo songa ndivyo akili pia inakomaa na kupevuka vizuri zaidi, hekima na busara vinaimarika zaidi, huku umakini na nguvu za mwana CCM huyo vinakua imara mara dufu zaidi.

Tofauti na chadema,
mathalani Mzee Azaveli Lwaitama, kadiri umri unavyosonga ndivyo anakua mpiga vizinga zaidi na anachoka zaidi, kinabaki kisogo na meno tu siji mangapi yale 🐒
 
Mimi niachieni CCM yangu. Naipenda sana CCM mpaka nabubujikwa na machozi ya Furaha. Mimi na CCM ni Damu Damu na hakuna wakunitenganisha na CCM. watahama wote na kuniacha na CCM yangu nimeibeba mabegani.
 
Katika kipindi hiki cha kisiasa nchini Tanzania, kuna hisia zinazoongezeka miongoni mwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhusu jinsi viongozi wanavyogawana madaraka na rasilimali. Mchakato huu umeonekana kana kwamba umejikita zaidi katika familia na urafiki, badala ya kuzingatia uwezo na sifa za mtu binafsi.

Hali hii inatia masikitiko na mshangao katika jamii, hasa kwa wanachama wa kawaida ambao wanaonekana kama wapagazi wa kubeba nyundo na majembe, wakitumikia maslahi ya wachache.

Uongozi wa Familia

Katika CCM, ni wazi kwamba kuna mtindo wa uongozi wa familia. Wengi wa viongozi wakuu wanatoka katika familia moja au wana uhusiano wa karibu na wale walio katika madaraka. Hali hii inawafanya wanachama wengine kuhisi kuwa nafasi katika chama hazipatikani kwa juhudi na uwezo, bali kwa nasaba na uhusiano wa kifamilia.

Hii inakera, hasa kwa vijana na wanachama wapya ambao wanatarajia kupata nafasi za kuongoza kutokana na uwezo wao.

Wanachama Wengine: Wapagazi?

Kwa upande mwingine, wanachama wa kawaida wa CCM wanajikuta wakifanya kazi kama wapagazi wa kubeba nyundo na majembe. Wanaweka juhudi kubwa katika kampeni na shughuli za chama, lakini matokeo ya kazi yao hayana maana kwa sababu hawana sauti katika maamuzi.

Hii inawafanya wajisikie wakiwa katika hali ya kutengwa, huku viongozi wakitumia nguvu zao kujiimarisha na kujenga mtandao wa watu walio karibu nao. Wanachama hawa wanajikuta wakitenda kazi kwa bidii, lakini wanashindwa kuona matokeo ya juhudi zao, hali inayoweza kusababisha kukata tamaa na kujiondoa katika shughuli za chama.

Mshangao wa Wanachama

Masikitiko haya yanafuatiwa na mshangao mkubwa. Wengi wanajiuliza: Je, ni kweli kwamba viongozi wa CCM wanadharau juhudi za wanachama wao? Je, kuna nafasi yoyote kwa wale ambao si sehemu ya familia au mtandao wa viongozi?

Maswali haya yanazidi kutafakariwa na wanachama, huku wakijaribu kuelewa mwelekeo wa chama chao. Wanaona kuwa uongozi wa chama unageuka kuwa mali ya kifamilia, na hii inahatarisha msingi wa demokrasia ndani ya chama.

Athari za Uongozi wa Familia

Uongozi wa familia unapoingia katika siasa, unaleta madhara makubwa. Kwanza, unashindwa kuleta mabadiliko yanayohitajika katika jamii. Wanachama wa kawaida wanaweza kukosa nafasi za kuonyesha uwezo wao, na hivyo, chama hakitafaulu katika kutekeleza sera zake. Pili, kuna hatari ya kuzalisha viongozi wasio na uwezo. Wakati viongozi wanapochaguliwa kutokana na uhusiano wa kifamilia badala ya uwezo, chama kinakosa ufanisi na uongozi bora.

Mwelekeo wa Baadaye

Ili kurekebisha hali hii, kuna haja ya CCM kuangalia upya mchakato wa uteuzi wa viongozi. Ni muhimu kuwapa wanachama wa kawaida nafasi ya kushiriki katika maamuzi na kuwa na sauti. Hii itasaidia kujenga chama chenye umoja na nguvu, ambacho kitaweza kusimama imara katika kukabili changamoto za kisasa. Wanachama wanahitaji kuona kuwa juhudi zao zinatambuliwa na thamani yao inastahili kupigiwa debe.

Hitimisho

Katika muktadha huu, ni dhahiri kuwa CCM inakabiliwa na changamoto kubwa ya ushirikishaji wa wanachama wake wa kawaida. Uongozi wa kifamilia unahitaji kufutwa ili kuwezesha uongozi bora na wa haki. Wanachama wanapaswa kuwa na sauti na nafasi katika kuamua mwelekeo wa chama chao.

Vinginevyo, CCM itajikuta ikikabiliwa na upinzani kutoka ndani na nje, na hatimaye itakosa uhalali miongoni mwa wananchi. Huu ndio wakati wa kubadilisha mtindo wa uongozi na kuhakikisha kuwa kila mwanachama anakuwa na nafasi na thamani katika chama.
 
Nina mshikaji wangu huyu bwana
1. Ni HR wa Halmashauri X
2. Ana Masters ya MBA in HR
3. Mpiga kazi balaa

Sasa bwana kwenye chama cha CCM ...
1. Yeye kila mwaka ana jezi mpya
2. Hakuna event ya CCM ya mkoa au wilaya asihudhurie
3. Kaenda mara kibaoo kwenye mikutano ya Chama Dodoma

Ila sasa ....
Sio kiongozi yoyote, huwa namwambjaga kuwa "braza huko unapotea na kupoteza muda, CCM ina wenyewe na walio wenyewe ni hawa wenye koo za VIP au wanaojuana na hizo koo"" ila Haelwagi

Namuoneaga huruma sanaa huyu kijana wangu.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Soon ubunge utampitia.
 
Soon ubunge utampitia.
Tusidanganyane, ndani ya CCM maji hufata mkondo.
Hata hizi nafasi za kiteuzi za Raisi kama DAS, RAS, Wakurugenzi, ETC utaona kabisa huteuliwa...
1. Wale ambao wazazi wao ni wana CCM tena hasa jumuia ya wazazi
2. Wale ambao wanajuana na koo za VIP
3. Kama ni mwanamke, utakuta mumewe ni someone serikalini.

Ila eti mwalimu wa Kiswahili kutoka halmashauri X ya ndanindanii kabisaa eti ateuliwe kuwa DAS dah badoo sanaa.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
View attachment 3205616

Tukiwa katikati ya mtanange mkali wa kidemokrasia wa CHADEMA ambao umetoa usawa na fursa kwenye kugombea nafasi mbalimbali hivo kuibua vipaji vipya vya uongozi; CCM waliibuka na wao Dodoma kwenye mchakato wao wa kutafuta makamu mwenyekiti wa chama.

Kwa mbwembwe za msururu wa magari mapya (vinyulaa) yaliowabeba wajumbe wa CCM wakiambatana na viongozi wazito wa chama hicho, tulijua kuna jambo kubwa linaenda kutokea Dodoma ambalo halijawahi kutokea.

Kwa masikitiko makubwa, kimetokea kihoja Dodoma; mbali na nafasi ya makamu kupatikana pasipo misingi ya demokrasia ya kugawa fursa za kuchaguana kwa wote, CCM wamekuja na mzee asiyeendana na nyakati za kileo na mabadiliko makubwa ya kisiasa yanayotokea.

Nimepata huruma sana kwa wana CCM wengine ambao wao hawatoki kwenye familia za vigogo wala hawana ushawishi wowote kwenye chama; je hao watapewa lini fursa za kuonesha vipaji vyao vya uongozi kama bado kuna misingi ya demokrasia za majina ya mfukoni?

Au hawa wana CCM wengine wataishia kuwa wapagazi wa kuwabebea ma 'giants' wa CCM majembe na manyundo mpaka wanazeeka, huku wakisindikizwa na wapiga madebe akina Tlaatlaah ChoiceVariable na kamanda asiyechoka kububujika machozi Lucas Mwashambwa ?

Hii inahitaji tafakari sana, CCM msidhani kwamba kushangilia kwenu ukosefu wa misingi ya demokrasia nchini kunawanufaisha kwa chochote. Kwa misingi iliyopo ndani ya CCM wengi mtaishia kuwa wapagazi, wapambe na m
1737229532727.jpg
achawa mpaka mzeeke.

What a waste of life.
 
Tusidanganyane, ndani ya CCM maji hufata mkondo.
Hata hizi nafasi za kiteuzi za Raisi kama DAS, RAS, Wakurugenzi, ETC utaona kabisa huteuliwa...
1. Wale ambao wazazi wao ni wana CCM tena hasa jumuia ya wazazi
2. Wale ambao wanajuana na koo za VIP
3. Kama ni mwanamke, utakuta mumewe ni someone serikalini.

Ila eti mwalimu wa Kiswahili kutoka halmashauri X ya ndanindanii kabisaa eti ateuliwe kuwa DAS dah badoo sanaa.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
CCM ukitaka mafanikio uwe na kipaji cha kulamba watu makalio😂 tena wale influential. Tengeneza ujamaa na watu influential ndani ya chama uone kama hutatoboa. Ukiwa shabiki mandazi bila mahesabu ya connection utazeeka bila bila.

Jiulize Steve Nyerere alikuwa anajuana na nani kabla ya kuanza kujikomba CCM. Ila kiherehere na shobo kwa wazee wa chama kambi ya Msoga ndio kimemfanya kapata recognition.
 
CCM bana...chama gani cha siasa hakina shamlashamla - hakuna ushindani kwenye uongozi, watu ni walewale tu - yaani mtu mmoja anaenda na kajina kake mfukoni halafu watu zaidi ya 2000 wanakubali tu - Wana- CCM ni kama kondoo vile - wapole, vichwa chini, hawalalamiki, wameambiwa hakuna kuchukua form kumchallenge mama - wanakubali tuuuu...
CDM wanachangamka sasa hata kama wanapitiliza ni kama Mbuzi - wanahangaika..yaani hata mtu akishinda anasema naam..cha moto nimekiona..
CCM ndo picha halisi ya Watz wengi -
 
Back
Top Bottom