CCM waanza mchakato wa kumshughulikia Luhanga Mpina, awasili mbele ya kamati ya maadili CCM

Mpina hana cha maana kakosa Uwaziri ndio maana ana hasira sio kwamba ni mtu bora kivile.

Watu wameishi nae huko akiwa na cheo wanamfahamu ni mtu wa hovyo pia
 
Kweeli CCM imekaribia...........................
Yaani mtu anaewasaidia kujirekebisha mnamfukuza!?!
Yaani wanataka machawa ya kusifia tu!
Ukiwa na akili ndani ya ccm wewe huwafai, hawana tofauti na kanisani, ukianza kuhoji mambo ya mbinguni utafukuzwa kanisa, umeelewa hujaelewa we nenda utaelewa jpili ijayo.
 
Wakati wa utawala wa Kayafa NI huyu Mpina ndio alichoma nyavu za Wavuvi.

Sasa Mungu anajibu maombi.,
 
Hapa lazima kuna kikundi cha mafisadi kinatumiwa na chawa kumuandama kwa maslahi ya matumbo yao mapana kama mapakacha yasiyoshiba kamwe.
 
Mpina hana cha maana kakosa Uwaziri ndio maana ana hasira sio kwamba ni mtu bora kivile.

Watu wameishi nae huko akiwa na cheo wanamfahamu ni mtu wa hovyo pia
Una ushahidi mkuu? Hata kama yupo hivyo ndio akose uhuru wa kutoa maoni yake kutetea rasimali za taifa zinazotafunwa na machawa na mafisadi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…