Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
DK. ANTONY DIALO NI MNAFIKI SANA, MPUUZENI
Na Bollen Ngetti
NINAANDIKA makala haya nikiendelea na matibabu ya Covid-19 kwa siku ya 9 lakini nina amini nitapona. Upekee wa virusi hivi ni kwamba vinaathiri mfumo wa upumuaji lakini si nishati ya ubongo. Kwa mantiki hiyo nina akili safi ninapoandika juu ya unafiki na woga wa Diallo.
Niharakishe kusema kwamba "Uncle Tony" ni baba yangu kiumri. Ni rafiki yangu wa karibu. Kwa mara ya kwanza nilimfahamu 2015 baada ya kutambulishwa kwake na Bernard Membe wakati wa mchakato wa kumpata mgombea Urais ndani ya CCM.
Dk. Diallo alipewa fedha nyingi na Membe ili kushawishi wajumbe wa Kanda ya Ziwa wa Mkutano Mkuu kuja kumpitisha Membe. Mara nyingi tulifanya vikao nyumbani kwake Dodoma. Lakini binafsi tulikutana mara kadhaa kuweka mambo sawa kwa mgombea wetu. Hii ni kuonesha kuwa ninamfahamu vizuri Dk. Diallo ambaye hata hivyo PhD yake ina utata sawa na uraia wake.
Uncle Tony ni mtu wa maslahi zaidi kuliko utumishi kwa umma. Nimesikiliza mahojiano yake kupitia television yake ya Star. Baadaye akafanya maigizo ya kurekebisha aliyoita "makosa" lakini wanasaikolojia tunaamini sentensi au maelezo ya kwanza ndio yaliyo na ukweli.
Diallo anasema tuliwachagua watu wenye rekodi ya kutibiwa Mirembe kuchukua nchi hivyo tuwe makini tuendako. Wakati huo huo akiponda utawala wa awamu ya 5 ya Magufuli. Nani alichukua nchi kama si Magufuli? Waziri Mkuu anachukua nchi? Makamu wa Rais au baraza la Mawaziri wanachukua nchi? Sisi si watoto wa chekechea! Hakuna alitafsiri vibaya lakini kauli ilimnyooshea kidole Marehemu Magufuli.
Sasa, hoja yangu ni hii! Kwa nini alimfanyia kampeni kichaa ilhali akijua? Pili, Tony atoa mkataba aliyoingia na CCM kwamba Magufuli akishinda "atapoozwa" kwa malipo kwa kazi ya kampeni kupitia Star Tv. Kama hana akaye kimya aache unafiki.
Tatu, kwa nini kipindi hicho cha Mwendazake hakujitokeza iwe sirini au hadharani kukosoa hali ya mambo ndani ya chama na Serikali? Kwa nini alikaa kimya huku ni kiongozi tena wa Mkoa? Mbona wengine (nikiwemo) tulikosoa chama chetu hadharani bila kuogopa kutekwa, kuteswa na hata jela?
Nikukumbushe wewe Dk. Diallo unakumbuka ni wewe ulinipigia simu ukiniambia niache kumkosoa Magufuli maana una taarifa Vetting yangu imekamilika na soon nitateuliwa U-DC? Hii si kwamba ulimkubali Magufuli ambaye leo unamwita kichaa? Ieleweke simtetei Marehemu isipokuwa napinga unafiki wa Uncle Tony anayejua kwamba linapokuja suala la kusema ukweli hata malaika nitamwambia. Nitausema.
Nikukumbushe tena Dialo, unakumbuka 2017 siku ulipoitwa Ikulu ya Magogoni na JPM saa nne asubuhi ukapewa maelekezo ya namna ya kummaliza kisiasa Bernard Membe? Unakumbuka ilipofika saa 11 jioni ulimpigia simu Membe na kumuomba muonane nyumbani kwako giza likiingia? Unakumbuka Membe alikukatalia baada ya kuwa na taarifa kuwa ulishinda Magogoni na Mwendazake? Ukamsihi sana aje saa tano usiku kwa "Uber" na si gari lake? Hivi unajua mchezo wote tuliufahamu kwamba Membe angekuja kingetokea nini?
Hivi unajua kwa kushindwa kwako kummaliza kisiasa Membe ndicho kilichokugombanisha na Ngosha na kukuona huna maana? Hivi unakumbuka ulivyomtimua kazi Mtangazaji Yusuf Kamote na kumnyima stahiki zake kisa tu ni rafiki wa Membe kwa maagizo kutoka mawinguni?
Leo unalia lia na kuuficha ukweli uliokodoa macho hadharani. Huu ni unafiki na woga usio na maana kwa umri wako. Umesema utagombea tena uenyekiti mwakani. Nitashangaa sana kama wana CCM makini wa Mwanza watakurejesha madarakani mtu wa aina yako sawa na ninavyoshangaa Uhamiaji kukukalia kimya kuhusu uraia wako.
Ushauri wangu kwako baba yangu, rafiki yangu kaa kimya. Usijipendekeze kwa Rais Samia Suluhu Hassan ili usogelee meza ndefu ya chakula. Tulia ulelee wajukuu hizi sio enzi za unafiki tena. Ahsante kwa leo!
Maoni: 0683 226539
#MguseMamaNinuke