CCM waibuka kidedea Bungeni


Mwenyekiti wa bunge la katiba hatakua na nafasi ya kucheza rafu

Anayo nafasi nzuri sana ya kucheza kuifurahisha CCM lakini

Anayo pia fursa sahihi ya kuonyesha watanzania ikiwa ni pamoja na wapinzani umahiri wake wa kufanya maamuzi kwa maslahi ya taifa bila upendeleo na itakua karata yake ya turufu kuwania nafasi ya urais 2015
 
Ni heri kuwa umetoa msimamo wa kimtazamo wako mapema. Hii itawasaidia sana wale wa upande wa pili kujiweka sawa kukabiliana na hilo. Kumbuka kuwa upo UWAKA.
 

CCM ni nani? nani kawapeleka pale?,nani kampeleka lisu,mnyika,mbowe,Mhagama,kapten komba,nk hawa wote wamepelekwa na wananchi na kama ni wananchi basi wananchi wanao support ccm ni wengi kuliko wanaosupport vyama pinzani,mitaani wana ccm ni wengi na bungen wana ccm ni wengi huwezi kwepa kwa sasa,wait your time
 
acha kupotosha watu
 
Ongera sana kwa ushindi huo wa mezani
Tunawasubiri huku kasarani.
 
CCM Oyeeeee......! Hakikisheni katiba inapita ikiwa na ibara nyingi zenye mlengo wa kukipa Chama tawala ushindi kwa chaguzi zote zijazo siku za mbele...! Tehe...teh...teh...!
 

Hivi hii katiba ya ccm siyo?!
 
Mzee tupa tupa huwa unajitahidi kuleta hoja ila hii ya leo umesimplify sana. It is not that much straight hii issue bhanaaa
 
CHADEMA na cuf wanataka siri ili ikifikia Yale mambo museveni ameyakataa wawezepiga kura bila kuffahamika hovyo kweli kura iwe ya wazii
Ulichoongea hapo ni utumbo kwa asilimia 100, how comes ulinganishe muswada wa kupinga ushoga alioupitisha Museveni na upitishwaji wa kifungu hadi kifungu, kwa kura ya wazi na siri!!

Nyinyi maCCM hila zenu siku zote zinaeleweka na umma wa watanzania, rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Warioba imeandaliwa vizuri sana kwa maslahi mapana ya nchi yetu, lakini kwa kuwa nyinyi CCM mlikuwa mkipeta katika chaguzi zote zilizopita kutokana na kubebwa na Katiba iliyopo, mnataka kuwadhibiti wabunge wenu wa magamba ambao lengo lao ni kuweka maslahi muwadhibiti kwa kura za wazi, ili muwaone wale wanaoweka maslahi ya nchi mbele, na kuyaweka maslahi ya chama tawala kapuni!!!
 

You have a point. Hasa kama mwenyekiti akiwa Mama Makinda, Jennista Mhagama, Pindi Chana au watu wengine wenye mlengo mzito wa kichama. Sitta mwenyewe haeleweki sana, ana element kubwa ya kutanguliza maslahi yake kwanza.
 
Wapinzani wa nchi hii ni "legelege" na kwangu sitoshangaa hilo likitokea.

Hakuna watu waliozaliwa wapinzani hivyo hao legelege wewe unaweza kuwa ndio zaidi hata ya ulege lege!Jipiganie usitegemee wanaume wengine wakupiganie halafu wakishindwa unawaita lege lege!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 

Kwa kweli mimi nilikuwa na nia ya kujiunga na CCM lakini nimehairisha maamuzi hayo baada ya kuona ubeberu unaoendelea kule Dodoma. Unapitisha kanuni za kuendesha bunge la katiba bila kupitisha kanuni ya jinsi ya kufanya maamuzi! Sijawahi kuona watu wenye akili za wendawazimu namna hiyo. Natamani jambo ili liingie kwenye kitabu cha kumbukumbu cha Dunia.
 

Halafu unaona wajumbe wanaotetea ukiwaangalia.vizuri nafsi zao zinawasuta
 
CHADEMA na cuf wanataka siri ili ikifikia Yale mambo museveni ameyakataa wawezepiga kura bila kuffahamika hovyo kweli kura iwe ya wazii

Hakunq kipengele cha ushoga katika rasimu ya katiba mpya nadhani unapenda sana ushoga au nawe ni mmoja wao!
 
Kumbe ww unachezea mzee 6 hana cha sisiem wala CHADEMA, Kitu mstari. Afu naomaba aendelee (na imani atapita) hadi budget ya mwaka 2014/15, Makinda na Job walipwe tu posho zao wakiwa wametulia kimya.
 
Halafu unaona wajumbe wanaotetea ukiwaangalia.vizuri nafsi zao zinawasuta

Sijui kama hao wanaotetea hoja ya ajabu namna hiyo kama wana familia. kama ningezaliwa katika familia ya baba au mama wa namna hiyo nadhani ningetamani ardhi ipasuke inifunike nisione aibu kubwa namna hiyo. Hata dhamira zao zimekufa ama kweli watu wakishaingiwa na ushetani wa kujitumikia wao wenyewe basi upofu wao ni mkubwa na akili zao huingia giza kiasi kwamba hata wakiwa uchi wanadhani wamevaa nguo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…