CCM wamegeuka kuwa Polisi au Polisi ndio wamekua CCM?

CCM wamegeuka kuwa Polisi au Polisi ndio wamekua CCM?

Kikwete aliwaambia CCM 2015 kuwa ni muda sasa wanaccm waanze kufanya siasa na waache kuwategemea polisi. Wawajibu wapinzani hoja kwa hoja. Lakin bahati mbaya CCM ya sasaiv haina tena viongozi wa kariba ya kina Kingunge, Malecela, Kinana nk. Wamebaki kujificha ofisini na kutuma polisi wafanye kazi yao. Ndo Mwisho wa CCM sasa
 
Ya kwao wamewashinda Hawana hoja Katiba,Bado Kuna Gang haziamini kuondoka kwa mwendazake.
Screenshot_20210807-014708_1.jpg
 
Adui siyo Polisi Kuna MAHALI tumeshindwa kutumia akili zetu tunazowaaminisha watu kwamba tunazo nyingi kutambua kiini Cha tatizo ni watu wa ajabu pekee ambao wanaweza kujumuisha tabia ya mtu mmoja au wawili kwa kundi lote la Mapolisi.

Kila KAZI ina discription zake Urubani huwezi kuufananisja na ujeshi vinginevyo ingekuwa ngumu sana kwenda kupigana vita kwa kutumia Demokrasia na haki za binadamu tutawalaumu Bure lakini kwenye majeshi hakuna kuhoji mambo ambayo wewe unaamini ni ya ukosefu wa akili ingawa hujasomea mambo hayo!
 
Siku hizi wananchi Wana uwezo wa kuchambua mambo ndiyo maana kila kinachosemwa wananchi wanatulia na kutafakari kuanzia lugha inayotumika Mpaka mantiki ya hoja.

Tunapotafakari tuhuma kwamba Polisi hawana akili tunajiuliza wale wenye akili zaidi ya Polisi wametumiaje akili zao au wametumia Polisi kama nyenzo ya kuwaaminisha wananzengo kwamba wao Wana akili kubwa kuliko Polisi ILI iwe rahisi Kupata huruma?

Katika hali kama hii tungependa Polisi wafanye nini?

Kwa mazingira haya hakuna kiongozi anayeweza kukubalika na watu wote lazima Kuna kundi litamkataa jambo la muhimu ni kutafuta namna ya kuishi na kundi pinzani Katika nchi.

Siku zote ILI wapinzani waonekane kuwepo lazima wapinge tatizo ni njia wanazotumia ambazo nyingine hazifai zinadidimiza uchumi nchi nyingi kusini kwa jangwa la Sahara zikifuata Demokrasia ya kweli zitadidimia kiuchumi badala yake tujenge uwezo wa udhibiti ulio wa haki ingawa tatizo kubwa ni kuwapata watu wenye nia njema wengi wao ni wanaotetea maslahi binafsi.
Hivi CCM na Upinzanib(Chadema) nani anatetea MAslahi binafsi?

Screenshot_20210806-162944.png
 
Eti askari ambaye amepata mafunzo kabisa anatumia gari la serikali kubomoa ofisi ya chama ambacho kina usajili halali, unakosa majibu![emoji2827][emoji2984]
 
Yaani ukute rpc kahadiwa ubunge baada ya kustaafu mbona upinzani watakoma.
Chalamila,kange,magu,sabaya, bashite,Omari mahita,nk walikuwa bize kupambana na upinzani wote hawapo upinzani still ungalipo.
Hakuna mapya watakimbiza upepo nao watapita.
 
Hoja ya kupambana na ccm CHADEMA imeshinda Tangu zamani kilichobaki kwa Sasa ni kupambana na genge la polisi View attachment 1883267
Watakiona cha moto Siku ya Haki itakapotimia.Hata muda wa kushona nguo(Uniform) aliyoitatua kijinga hanao.Huu ni uzembe wake ila pia viongozi wake.Hawana Parade ya kuwakagua utimamu,na unadhifu?
 
Siku hizi wananchi Wana uwezo wa kuchambua mambo ndiyo maana kila kinachosemwa wananchi wanatulia na kutafakari kuanzia lugha inayotumika Mpaka mantiki ya hoja.

Tunapotafakari tuhuma kwamba Polisi hawana akili tunajiuliza wale wenye akili zaidi ya Polisi wametumiaje akili zao au wametumia Polisi kama nyenzo ya kuwaaminisha wananzengo kwamba wao Wana akili kubwa kuliko Polisi ILI iwe rahisi Kupata huruma?

Katika hali kama hii tungependa Polisi wafanye nini?

Kwa mazingira haya hakuna kiongozi anayeweza kukubalika na watu wote lazima Kuna kundi litamkataa jambo la muhimu ni kutafuta namna ya kuishi na kundi pinzani Katika nchi.

Siku zote ILI wapinzani waonekane kuwepo lazima wapinge tatizo ni njia wanazotumia ambazo nyingine hazifai zinadidimiza uchumi nchi nyingi kusini kwa jangwa la Sahara zikifuata Demokrasia ya kweli zitadidimia kiuchumi badala yake tujenge uwezo wa udhibiti ulio wa haki ingawa tatizo kubwa ni kuwapata watu wenye nia njema wengi wao ni wanaotetea maslahi binafsi.
Bila shaka We we utakuwa ni polis . policcm. Kuna polis mwenzenu huko arusha amewahi kuita " ccm oyee " kwenye mkutano wa ccm akiwa na mijezi ya polis. Ukijua polis hawana akili hawajui hata kama katiba nzuri ni kwa maendeleo ya taifa kizazi cha sasa na baadaye. Nasikia kuna polis alimwambia Mbowe "we we ndo unajifanya unaijua katiba mya sasa tuta kufundisha" polis kama huyo siyo tu ni mjinga, pia ni mpumbavu maana inaelekea hata hajui katiba ni mini. Pamoja na kwamba kuna wachache werevu huko polis ila wengi four failure.
 
Kuna mambo ya ajabu sana yanafanyika hadi unakosa majibu.

Eti askari ambaye amepata mafunzo kabisa anatumia gari la serikali kubomoa ofisi ya chama ambacho kina usajili halali, unakosa majibu!

Polisi mwenye akili timamu kabisa anajitokeza hadharani na kumbambikia kesi ya Ugaidi kiongozi wa chama cha siasa! Unakosa majibu

Unangalia kwa mshangao Askari mwenye akili timamu anamshika kalio mwanamke kisa tu kuilinda CCM. Unajiuliza hawa ni askari au ni malaika wa uharibifu?

Askari timamu kabisa (kwa nje) anawakamata wanachama wa chama halali wakiwa kwenye mkutano halali unasema wamekutwa kwenye pagala! Unajiuliza huyu askari anawaza kwa kutumia kiungo gani cha mwili??

Sometimes, unakuta askari mwenye familia kabisa anashindwa kutoafutisha Mambo yaa kimahakama na Tuhuma zake za kubumba, unajiuliza, "Kama huyu ndio IGP mwenye ako narrow minded kiasi hiki, vipi kuhusu anaowaongoza?" Unakaa kimya tu.

Askari kabisa na akili zake, hata kama ni chache, ni zake! Anakukamata kisa uko mahakamani! Unajiuliza, huyu ana akili kweli au kaziacha nyumbani?

Polisi acheni siasa kwenye mambo ya msingi
Policcm ni aibu
 
Katiba mpya itawaepusha police kupewa maagizo ya hovyo na ccm,au kumpigia saluti raia mfano DC,RC,waziri.salute ni salamu ya kijeshi hao tajwa sio wanajeshi,eti vitoto kama jokate,nasari, lijuakali navyo vinapigiwa saluti na askari sawa na baba au babu yao.
Police watakuwa huru watafata Sheria na sio maagizo.Unatumwa unabomoe ofisi ya chama kisa boss wako anapalilia ubunge akistaafu inabidi uende usipoenda Kazi huna. Panapo katiba mpya unyanyasaji kama huu hautokuwapo
 
Hata kukiwa na Katiba mpya bado inahitajika utashi wa watu Katika kutekeleza matakwa ya katiba HUSIKA.

Sheria zilizopo ni nzuri kabisa tatizo ni utashi wa kuzifuata KAZI ya Polisi ni kuisimamia Sheria zilizopo hata kama hazikidhi vigezo.
 
Back
Top Bottom