Pre GE2025 CCM wamepita mitaani kuandikisha wapiga kura, je ni haki yao kikatiba?

Pre GE2025 CCM wamepita mitaani kuandikisha wapiga kura, je ni haki yao kikatiba?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuandikisha wapiga kura ni "JUKUMU la TUME YA UCHAGUZI" SIYO LA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA.
Mkuu Acha ubishi wa kijuha,CCM huo mchezo huufanya labda tu upande wa pili wafuatilie kwa kina kujua huwa zinatumika vipi kufanikisha ushindi.Nina case study ya Kirumba_ Mwanza 2012 ya uchaguzi mdogo wa diwani kipindi hicho Jiji la Mwanza likiwa chini ya CHADEMA kwa tofauti ya idadi ya diwani mmoja mbinu hii ilitumika sana na kampeni zilikuwa za moto sana...

CCM walijipanga mno kwa kila mbinu ili waweze kushinda kata hiyo wa balansi mzani na lengo ni warejeshe Jiji La Mwanza chini ya CCM,palikuwa na rafu nyingi mno,CHADEMA nao walijizatiti vilivyo kukabiliana na CCM na walifaulu kutetea kata hiyo huku wabunge wao waliokuwa wanaratibu kampeni Kiwia-Ilemela,Wenje-Nyamagana na Machemuli-Ukerewe wakiwa ICU baada ya kucharangwa mapanga ya haja na Greenguard wa CCM usiku wa kuamukia siku ya kupiga kura.:

Niliogopa sana nguvu ya umma kuanzia siku hiyo.CCM waliamua kabisa wa divert attention ya wapiga kura kwa kutengeneza msiba wa wa wabunge watatu kwa mpigo ili tu wapate mwanya wa kuiba ama kubatilisha matokeo,lakini umma uligoma,wana Kirumba walienda kupiga kura kwa wingi mno na kuzilinda.Usipende pia kudharau taarifa za JF hapa..
 
Wasaam,

Leo nilikua mitaa ya Vingunguti nilienda salamia jamaa zangu nikashangazwa na viongozi wa CCM kupita nyumba hadi nyumba kuandiksha wapiga kura kwa kuwapa ahadi za kuja kuwagawia pesa na mikopo mbalimbali wakati uchaguzi ukiwadia.

Kiukweli hii ni rushwa ya kisiasa kama sio kampeni kabla ya kuruhusiwa kampeni, au tuseme labda ni haki yao kikatiba?

Naamini ingekuwa ni CHAMA chengine cha siasa basi police wangeshawazingira na msajili wa vyama vya siasa angeitisha press haraka na kulaani.
CCM imefanikiwa kutengeneza taifa la wajinga wengi, hilo zoezi linafanyika mitaa yote nchi nzima na ni maandalizi ya wizi wa kura sababu wanajua wajinga nchi hii wapo wa kutosha sana
 
Nimeiona hii pia Babati -Vijijini juzi.Mfanyakazi mwenzangu alikuwa analalamika kwamba amepigiwa simu na mkewe kuwa nyumbani amefika Balozi wa CCM na watu kadhaa wamemuomba vitambulisho vya kupigia kura chake na hata cha mme wake kama amekiacha,ili waviandikishe.Jamaa alipandwa jaziba sana akamwambia --Wapatie tu na uondoke nao kabisa--.Sijui nini kiliendelea huko,ameenda likizo kwake leo ngoja akirudi nitamuuliza kilikuwa ni nini na kipi kimejiri.JF haijawahi kutindikiwa nyeti za kila nyanja.
Hili hata mimi limenitokea mkuu.
 
Duh!
Mkuu 'Drifter', hivi labda sijielezi vizuri ili nieleweke, maana unaendelea kuniuliza swali ambalo nilidhani mara nyingi sana huwa ninalijibu, na hata hapo juu nimejibu.
Hakuna la ziada wanalotakiwa CHADEMA kulifanya zaidi ya kufanya kazi na wananchi wenyewe.
CHADEMA hawana uwezo wa kuwaondoa CCM bila ya wananchi kuifanya kazi hiyo
Jambo hili hili nimeliimba miaka kadhaa sasa, na bado naulizwa maswali juu yake?

Huyo Waziri wa Mambo ya ndani (Masabuni), anajuwa wapi pa kwenda kuwalaghai wananchi; huko mitaani kwao, nyumba kwa nyumba. Itakuwaje CHADEMA wasijue pa kwenda ili kukomesha ujinga wa kiongozi kama huyo!

Kazi ya CHADEMA safari hii ni nyepesi zaidi kuliko nyakati zingine zozote ilizo wahi kupambana na CCM. Historia nayo inaonyesha wazi kwamba chama hicho kinapojipanga na kukataa hujuma za CCM hupata mafanikio makubwa. Rejea mwaka ambao CHADEMA ilifanikiwa kuwa na wabunge wengi zaidi Bungeni. Wengi wa wabunge hao walipatikana kwa kukataa hujuma za CCM.

Sasa utanilaumu, kwa kukumbushia kazi nzuri iliyowahi kufanyika huko siku za nyuma, lakini ikawa kama historia hiyo haipo tena!
Sawa. Nimekuelewa. Katika comment yako iliyopita umesema CHADEMA wanapaswa kwenda mahakamani kupinga ujinga anaofanya Masauni. Sina cha kuongeza.

Mwaka 2015 ndio mwaka CHADEMA (na vyama vingine) walipata wabunge wengi bungeni - kupitia mwamvuli wa UKAWA. Sijui kama wadau wanatambua na kuthamini walichofanya CHADEMA wakati ule. Na kama kinakubalika tena nyakati hizi.

Well, sina cha kuongeza kwa hili pia.
 
Waje waniandikishe na mimi asee
Interested issue
 
Ila ccm!!! Mmetengeneza Taifa la wajinga wengi, ili muendelee kutawala wajinga wengi wanaishi kwa mlo mmoja.
Wakidanganywa mkidai haki zenu tu, kutakuwa na vita nao wanatulia na mnafanya mnavyotaka. Ila mjue ujinga huwa una mwisho, sasa hivi mnacheka nyinyi, mwisho wenu una siku yake.
 
Tatizo ni CCM, tusijaribu kuvuruga mwelekeo tunao ujua sote.

Ndiyo, matumaini makubwa kwa sassa hivi ni CHADEMA zaidi ya chama kingine chochote cha siasa, na hili halihitaji maelezo, hasa kwa mtu kama wewe.

"Matarajio kwa CHADEMA"? Kuna asiyejuwa yanayofanywa na CCM kuvuruga chaguzi? Huu ni uhalifu. Uvunjifu wa sheria.
Mahakama iliyo wazi ni ya wananchi wenyewe, wapiga kura, ambao kura zao tayari mipango inafanyika kuziharibu.
Bado unaniuliza nataka CHADEMA wafanye nini? Waende mahakamani na mahakama itaamua yenyewe ifanye nini.

Mkuu 'Drifter', kila tunapokutana unakuwa 'defensive' sana kuhusu wajibu wa CHADEMA kwa wananchi wa nchi hii.

Masauni kuanza kuwatumia wajumbe wa nyumba kumi kumi huko mitaani; CHADEMA kweli hawana jibu juu ya upumbavu wa aina hiyo? Sasa watafanya kazi gani CHADEMA na wawe na mategemeo gani kwenye chaguzi hizi kama njia zilezile zinazofahamika miaka yote zinaendelea kutumika kuvuruga chaguzi.
Hebu wewe nieleze matumaini ya CHADEMA hasa yapo wapi?
Ndugu....umeongea kwa hisia sana na hapa tu CHADEMA ndipo wanatakiwa wapafanyie kazi kwa kweli,ni jambo lisilofichika kwamba wanaungwaji mkubwa mno wa watu tukiweka pembeni unazi wa kichama na huwa wa wazuri mno hata kimikakati ya kampeni kwenye chaguzi mpaka CCM huwa wanapoteana na hata kuchanganyikiwa mpaka na kulia kabisa.Nakumbuka Mukama katibu Mkuu wa CCM mpaka aliehuka kabisa kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge Igunga akilalamika CHADEMA wameingiza silaha za maangamizi ni magaidi akaitisha mpaka mkutano na wanahabari akathibitisha ugaidi wa CHADEMA kwa kuonyesha kipisi fulani cha kisu kama moja ya silaha za maangamizi zilizoingizwa Igunga na CHADEMA, sasa sijui kilikuwa na muhuri wa au nembo ya CHADEMA?!ITV nao wakarusha hivyohivyo!!.Lakini uhalisia ni kwamba CHADEMA walikaba mpaka inya kabisa za CCM,chama dola wakiwa na kila aina ya nyenzo wakipelekwa puta na Suzani Kiwanga,Kasulumbai a.k.a Mungu wa Maswa na Lwakatare.Ilikuwa ni vituko tupu mara banda la kuku za mwana CCM lichomwe moto na kuku wote waungue karatasi yenye maandishi -SISI NDIYO CHADEMA ibaki isiungue?!Sijawqhi kuwa na mashaka ya CCM kuchomoka ni wepesi mno bila janja janja na hasa Polisi kutoingilia wakakae kati kabisa....Ma..nina ni mapema tu CCM mbele ya CHADEMA wanachomoka.Ni mekuwepo field mara kadhaa....ni wepesi mno
 
Ila ccm!!! Mmetengeneza Taifa la wajinga wengi, ili muendelee kutawala wajinga wengi wanaishi kwa mlo mmoja.
Wakidanganywa mkidai haki zenu tu, kutakuwa na vita nao wanatulia na mnafanya mnavyotaka. Ila mjue ujinga huwa una mwisho, sasa hivi mnacheka nyinyi, mwisho wenu una siku yake.
Mimi nawachukia mno CCM ni wanyama na wamejaa uchu wa madaraka ambayo kwayo ni bora kuliko hata uhai:Nilikuwepo pale Kata ya Ludete_Katoro-Geita kwenye uchaguzi mdogo wa diwani:CHADEMA wakampangia Marehemu Alphonse Mawazo akaratibu kampeni:CCM walipaniki na hapo huwa siwaelewi hofu kwa mtu mmoja ambaye hata kura hatapiga huwa inatoka wapi?Akaviziwa siku ya mwisho ya kampeni akitoka kwenye kikao cha mwisho cha mikakati ya ushindi wakampasua fuvu kama kuni,mji ikajaa simanzi watu wakasusia kupiga kura na mapema tu CCM wakajitangaza washindi tena wakishindo.
 
Kama una ushahidi wa usemayo, ama nenda wewe mwenyewe kuripoti Tume ya Uchaguzi; au wasilisha tuhuma zako kwenye Chama chako upendekeze wafanye hivyo badala yako.

Aidha, kama uyasemayo ni kweli, hapo kuna makosa mawili; kwanza kufanya kampeni hivi sasa hairuhusiwi kwa kuwa haijatangazwa kampeni zianze. Pili, hata kama tayari kampeni zingekuwa zimeidhinishwa, hakuna chama binafsi kinachoruhusiwa kuandikisha wapiga kura.

Ni Tume ya Uchaguzi pekee inayofanya kazi hiyo. Hivyo, kushinda kwa suala lako likifika mahali panapohusika ni asilimia 100. Labda tu ushindwe kuthibitisha kwamba unayoyatuhumu kweli yalitokea.
Kaka nimeshudia kwa macho yangu hata mimi walijaribu kunishawishi nikawaambia warubuni hao wasiojitambua.
 
Wasaam,

Leo nilikua mitaa ya Vingunguti nilienda salamia jamaa zangu nikashangazwa na viongozi wa CCM kupita nyumba hadi nyumba kuandikisha wapiga kura kwa kuwapa ahadi za kuja kuwagawia pesa na mikopo mbalimbali wakati uchaguzi ukiwadia.

Kiukweli hii ni rushwa ya kisiasa kama sio kampeni kabla ya kuruhusiwa kampeni, au tuseme labda ni haki yao kikatiba?

Naamini ingekuwa ni CHAMA chengine cha siasa basi police wangeshawazingira na msajili wa vyama vya siasa angeitisha press haraka na kulaani.
Ukiwapa namba ya nida, watatengeneza KAZI feki zitakazotumika kutengeneza vituo hewa Ili wizi wa kura uendelee.

Mkiweza kuwapigia ukunga wakatawanyika ni Bora sana.

Si wa kuwachekea hao.
 
Sawa. Nimekuelewa. Katika comment yako iliyopita umesema CHADEMA wanapaswa kwenda mahakamani kupinga ujinga anaofanya Masauni. Sina cha kuongeza.
"Mahakama" nisiyo kuwa na shaka nayo hata kidogo, ni hiyo moja tu ya "wananchi".
Kwa hiyo ni mahakama hiyo ndiyo niliyo ilenga katika maandishi yangu.
Hizi nyinginezo, pamoja na Bunge na polisi na taasisi mbalimbali, zote ni nyenzo zinazotumiwa na CCM "kuwateka" waTanzania
Ndiyo sababu tumefikia hapa tulipo sasa.
 
Mkuu Acha ubishi wa kijuha,CCM huo mchezo huufanya labda tu upande wa pili wafuatilie kwa kina kujua huwa zinatumika vipi kufanikisha ushindi.Nina case study ya Kirumba_ Mwanza 2012 ya uchaguzi mdogo wa diwani kipindi hicho Jiji la Mwanza likiwa chini ya CHADEMA kwa tofauti ya idadi ya diwani mmoja mbinu hii ilitumika sana na kampeni zilikuwa za moto sana...

CCM walijipanga mno kwa kila mbinu ili waweze kushinda kata hiyo wa balansi mzani na lengo ni warejeshe Jiji La Mwanza chini ya CCM,palikuwa na rafu nyingi mno,CHADEMA nao walijizatiti vilivyo kukabiliana na CCM na walifaulu kutetea kata hiyo huku wabunge wao waliokuwa wanaratibu kampeni Kiwia-Ilemela,Wenje-Nyamagana na Machemuli-Ukerewe wakiwa ICU baada ya kucharangwa mapanga ya haja na Greenguard wa CCM usiku wa kuamukia siku ya kupiga kura.:

Niliogopa sana nguvu ya umma kuanzia siku hiyo.CCM waliamua kabisa wa divert attention ya wapiga kura kwa kutengeneza msiba wa wa wabunge watatu kwa mpigo ili tu wapate mwanya wa kuiba ama kubatilisha matokeo,lakini umma uligoma,wana Kirumba walienda kupiga kura kwa wingi mno na kuzilinda.Usipende pia kudharau taarifa za JF hapa..
Hukuelewa, niliposema jukumu la kuandikisha wapiga kura ni la tume ya uchaguzi, vyama vinaweza kuhamasisha wananchi tu.
Sikusema CCM hawakufanya, hao dunia nzima inawaelewa ni wezi na hawakubaliki popote, hata wao hawajikubali.
 
Tunampa fisi jukumu la kuilinda mbuzi wetu, kisha tunajiuliza kwanini kila siku wanapungua.
 
Wasaam,

Leo nilikua mitaa ya Vingunguti nilienda salamia jamaa zangu nikashangazwa na viongozi wa CCM kupita nyumba hadi nyumba kuandikisha wapiga kura kwa kuwapa ahadi za kuja kuwagawia pesa na mikopo mbalimbali wakati uchaguzi ukiwadia.

Kiukweli hii ni rushwa ya kisiasa kama sio kampeni kabla ya kuruhusiwa kampeni, au tuseme labda ni haki yao kikatiba?

Naamini ingekuwa ni CHAMA chengine cha siasa basi police wangeshawazingira na msajili wa vyama vya siasa angeitisha press haraka na kulaani.
Na walliokubali kuandikishwa watakuwa na ugonjwa ambao haujapata jina!
 
Wasaam,

Leo nilikua mitaa ya Vingunguti nilienda salamia jamaa zangu nikashangazwa na viongozi wa CCM kupita nyumba hadi nyumba kuandikisha wapiga kura kwa kuwapa ahadi za kuja kuwagawia pesa na mikopo mbalimbali wakati uchaguzi ukiwadia.

Kiukweli hii ni rushwa ya kisiasa kama sio kampeni kabla ya kuruhusiwa kampeni, au tuseme labda ni haki yao kikatiba?

Naamini ingekuwa ni CHAMA chengine cha siasa basi police wangeshawazingira na msajili wa vyama vya siasa angeitisha press haraka na kulaani.
Hapa ndio najaribu kufikiria kuwa huenda CCM huwa wanashinda kihalali.Kwa Sababu wakati vyama vingine vipo bize na shughuli nyingine wao wapo mtaa Kwa mtaa kutafuta wapiga kura loyal.Wanaandikisha wanachama wapya.Wanatumia pia faida ya kuwa chama tawala kuwalaghai wananchi na wananchi wanajaa.
 
Back
Top Bottom