Idimulwa
JF-Expert Member
- May 27, 2011
- 4,944
- 2,459
Mkuu Acha ubishi wa kijuha,CCM huo mchezo huufanya labda tu upande wa pili wafuatilie kwa kina kujua huwa zinatumika vipi kufanikisha ushindi.Nina case study ya Kirumba_ Mwanza 2012 ya uchaguzi mdogo wa diwani kipindi hicho Jiji la Mwanza likiwa chini ya CHADEMA kwa tofauti ya idadi ya diwani mmoja mbinu hii ilitumika sana na kampeni zilikuwa za moto sana...Kuandikisha wapiga kura ni "JUKUMU la TUME YA UCHAGUZI" SIYO LA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA.
CCM walijipanga mno kwa kila mbinu ili waweze kushinda kata hiyo wa balansi mzani na lengo ni warejeshe Jiji La Mwanza chini ya CCM,palikuwa na rafu nyingi mno,CHADEMA nao walijizatiti vilivyo kukabiliana na CCM na walifaulu kutetea kata hiyo huku wabunge wao waliokuwa wanaratibu kampeni Kiwia-Ilemela,Wenje-Nyamagana na Machemuli-Ukerewe wakiwa ICU baada ya kucharangwa mapanga ya haja na Greenguard wa CCM usiku wa kuamukia siku ya kupiga kura.:
Niliogopa sana nguvu ya umma kuanzia siku hiyo.CCM waliamua kabisa wa divert attention ya wapiga kura kwa kutengeneza msiba wa wa wabunge watatu kwa mpigo ili tu wapate mwanya wa kuiba ama kubatilisha matokeo,lakini umma uligoma,wana Kirumba walienda kupiga kura kwa wingi mno na kuzilinda.Usipende pia kudharau taarifa za JF hapa..