Pre GE2025 CCM wamepita mitaani kuandikisha wapiga kura, je ni haki yao kikatiba?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuandikisha wapiga kura ni "JUKUMU la TUME YA UCHAGUZI" SIYO LA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA.
Mkuu Acha ubishi wa kijuha,CCM huo mchezo huufanya labda tu upande wa pili wafuatilie kwa kina kujua huwa zinatumika vipi kufanikisha ushindi.Nina case study ya Kirumba_ Mwanza 2012 ya uchaguzi mdogo wa diwani kipindi hicho Jiji la Mwanza likiwa chini ya CHADEMA kwa tofauti ya idadi ya diwani mmoja mbinu hii ilitumika sana na kampeni zilikuwa za moto sana...

CCM walijipanga mno kwa kila mbinu ili waweze kushinda kata hiyo wa balansi mzani na lengo ni warejeshe Jiji La Mwanza chini ya CCM,palikuwa na rafu nyingi mno,CHADEMA nao walijizatiti vilivyo kukabiliana na CCM na walifaulu kutetea kata hiyo huku wabunge wao waliokuwa wanaratibu kampeni Kiwia-Ilemela,Wenje-Nyamagana na Machemuli-Ukerewe wakiwa ICU baada ya kucharangwa mapanga ya haja na Greenguard wa CCM usiku wa kuamukia siku ya kupiga kura.:

Niliogopa sana nguvu ya umma kuanzia siku hiyo.CCM waliamua kabisa wa divert attention ya wapiga kura kwa kutengeneza msiba wa wa wabunge watatu kwa mpigo ili tu wapate mwanya wa kuiba ama kubatilisha matokeo,lakini umma uligoma,wana Kirumba walienda kupiga kura kwa wingi mno na kuzilinda.Usipende pia kudharau taarifa za JF hapa..
 
CCM imefanikiwa kutengeneza taifa la wajinga wengi, hilo zoezi linafanyika mitaa yote nchi nzima na ni maandalizi ya wizi wa kura sababu wanajua wajinga nchi hii wapo wa kutosha sana
 
Hili hata mimi limenitokea mkuu.
 
Sawa. Nimekuelewa. Katika comment yako iliyopita umesema CHADEMA wanapaswa kwenda mahakamani kupinga ujinga anaofanya Masauni. Sina cha kuongeza.

Mwaka 2015 ndio mwaka CHADEMA (na vyama vingine) walipata wabunge wengi bungeni - kupitia mwamvuli wa UKAWA. Sijui kama wadau wanatambua na kuthamini walichofanya CHADEMA wakati ule. Na kama kinakubalika tena nyakati hizi.

Well, sina cha kuongeza kwa hili pia.
 
Waje waniandikishe na mimi asee
Interested issue
 
Ila ccm!!! Mmetengeneza Taifa la wajinga wengi, ili muendelee kutawala wajinga wengi wanaishi kwa mlo mmoja.
Wakidanganywa mkidai haki zenu tu, kutakuwa na vita nao wanatulia na mnafanya mnavyotaka. Ila mjue ujinga huwa una mwisho, sasa hivi mnacheka nyinyi, mwisho wenu una siku yake.
 
Ndugu....umeongea kwa hisia sana na hapa tu CHADEMA ndipo wanatakiwa wapafanyie kazi kwa kweli,ni jambo lisilofichika kwamba wanaungwaji mkubwa mno wa watu tukiweka pembeni unazi wa kichama na huwa wa wazuri mno hata kimikakati ya kampeni kwenye chaguzi mpaka CCM huwa wanapoteana na hata kuchanganyikiwa mpaka na kulia kabisa.Nakumbuka Mukama katibu Mkuu wa CCM mpaka aliehuka kabisa kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge Igunga akilalamika CHADEMA wameingiza silaha za maangamizi ni magaidi akaitisha mpaka mkutano na wanahabari akathibitisha ugaidi wa CHADEMA kwa kuonyesha kipisi fulani cha kisu kama moja ya silaha za maangamizi zilizoingizwa Igunga na CHADEMA, sasa sijui kilikuwa na muhuri wa au nembo ya CHADEMA?!ITV nao wakarusha hivyohivyo!!.Lakini uhalisia ni kwamba CHADEMA walikaba mpaka inya kabisa za CCM,chama dola wakiwa na kila aina ya nyenzo wakipelekwa puta na Suzani Kiwanga,Kasulumbai a.k.a Mungu wa Maswa na Lwakatare.Ilikuwa ni vituko tupu mara banda la kuku za mwana CCM lichomwe moto na kuku wote waungue karatasi yenye maandishi -SISI NDIYO CHADEMA ibaki isiungue?!Sijawqhi kuwa na mashaka ya CCM kuchomoka ni wepesi mno bila janja janja na hasa Polisi kutoingilia wakakae kati kabisa....Ma..nina ni mapema tu CCM mbele ya CHADEMA wanachomoka.Ni mekuwepo field mara kadhaa....ni wepesi mno
 
Mimi nawachukia mno CCM ni wanyama na wamejaa uchu wa madaraka ambayo kwayo ni bora kuliko hata uhai:Nilikuwepo pale Kata ya Ludete_Katoro-Geita kwenye uchaguzi mdogo wa diwani:CHADEMA wakampangia Marehemu Alphonse Mawazo akaratibu kampeni:CCM walipaniki na hapo huwa siwaelewi hofu kwa mtu mmoja ambaye hata kura hatapiga huwa inatoka wapi?Akaviziwa siku ya mwisho ya kampeni akitoka kwenye kikao cha mwisho cha mikakati ya ushindi wakampasua fuvu kama kuni,mji ikajaa simanzi watu wakasusia kupiga kura na mapema tu CCM wakajitangaza washindi tena wakishindo.
 
Kaka nimeshudia kwa macho yangu hata mimi walijaribu kunishawishi nikawaambia warubuni hao wasiojitambua.
 
Ukiwapa namba ya nida, watatengeneza KAZI feki zitakazotumika kutengeneza vituo hewa Ili wizi wa kura uendelee.

Mkiweza kuwapigia ukunga wakatawanyika ni Bora sana.

Si wa kuwachekea hao.
 
Sawa. Nimekuelewa. Katika comment yako iliyopita umesema CHADEMA wanapaswa kwenda mahakamani kupinga ujinga anaofanya Masauni. Sina cha kuongeza.
"Mahakama" nisiyo kuwa na shaka nayo hata kidogo, ni hiyo moja tu ya "wananchi".
Kwa hiyo ni mahakama hiyo ndiyo niliyo ilenga katika maandishi yangu.
Hizi nyinginezo, pamoja na Bunge na polisi na taasisi mbalimbali, zote ni nyenzo zinazotumiwa na CCM "kuwateka" waTanzania
Ndiyo sababu tumefikia hapa tulipo sasa.
 
Hukuelewa, niliposema jukumu la kuandikisha wapiga kura ni la tume ya uchaguzi, vyama vinaweza kuhamasisha wananchi tu.
Sikusema CCM hawakufanya, hao dunia nzima inawaelewa ni wezi na hawakubaliki popote, hata wao hawajikubali.
 
Tunampa fisi jukumu la kuilinda mbuzi wetu, kisha tunajiuliza kwanini kila siku wanapungua.
 
Na walliokubali kuandikishwa watakuwa na ugonjwa ambao haujapata jina!
 
Hapa ndio najaribu kufikiria kuwa huenda CCM huwa wanashinda kihalali.Kwa Sababu wakati vyama vingine vipo bize na shughuli nyingine wao wapo mtaa Kwa mtaa kutafuta wapiga kura loyal.Wanaandikisha wanachama wapya.Wanatumia pia faida ya kuwa chama tawala kuwalaghai wananchi na wananchi wanajaa.
 
Inaandikisha wapiga kura au wanachama wapya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…