Kama haya uliyo eleza hapa yana ukweli wowote, hata theluthi moja tu ya ukweli (na sina sababu ya kukuhoji juu yake); ule unaoitwa "UJINGA" wa waTanzania unaanzia hapa hapa kuruhusu haya yaendelee kuwepo.
Lakini, kama nilivyo wahi kueleza, huu siyo "ujinga" wa waTanzania; bali ni sehemu ya mwendelezo wa "UTEKAJI" wa waTanzania na genge hili ndani ya CCM.
Hii ndiyo hatua inayotakiwa kukataliwa kwa nguvu zote na wote wanaojiamini wao siyo wajinga wala mateka.
Kuruhusu upuuzi wa namna hii kuendelea kuwepo ni dhambi kubwa sana waTanzania wa leo wanayoitendea nchi yao.
Inabidi nieleze uhusiano wa zoezi hili na "utekwaji" wanaofanyiwa waTanzania bila wao kujitambua.
Waziri wa Mambo ya Ndani (Msabuni, ndiyo najua jina lake); hivi karibuni amenukuliwa akihimiza wajumbe wa nyumba kumi kuwafikia wananchi kwa zoezi hilo; na kajitapa kwamba yeye ndiye mkuu wa "mapolisi".
Sasa kinacho shangaza, vyama vya upinzani, hususani CHADEMA ni kama hawaelewi kinachozungumzwa na mtu kilaza kama huyo.
CCM tayari wamo kazini kuvuruga uchaguzi wa serikali za mitaa, kwa maandalizi ya kuvuruga uchaguzi mkuu!
Halafu kila mtu anajifanya kama hajui chochote kinacho endelea!