Elections 2010 CCM wameshashinda uchaguzi huu

silver25

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
743
Reaction score
44
Mimi sikifagirii chama hiki cha CCM... lakini situation inaonesha kimeshashinda, kwasababu Zenj wamesha vunjwa mbavu kwa kumsimamisha Dr. Shein, na kumleta huku bilali ni saikolojia kubwa sana kwani kura zoooteee za CUF zimesha nyang, anyway na CCM kutoka Zenj

Majimbo zaidi ya kumi sasa yameshakuwa Confirmed kuwa yapo chini ya CCM,, Source THE GUARDIAN 21STAUGUST2010,, SASA KUTOKANA NA MAJIMBO HAYO AMBAYO UKITAKA HABARI KAMILI NENDA THE gUARDIAN tayari CCM wamesha pata kura kadhaa ambazo wao kwa sasa wanahitaji kuongea tuu kidogo ili wajihakikishie ushindi,,

Navilaumu sana Vyama Pinzani kwa kuto simamisha wagombea katika baadhi ya majimbo kwani kwa staili hiyo maana yake wamekubali CCM wachukue tena nchi yetu waendelee kuiharibu kwa ufisadi...

Mimi inaniuma sana
 
Wewe ndiyo mbumbumbu kabisa unajua kinachoendelea zanzibar kama wewe ni mgeni na siasa za huko ni bora kunyamaza. Halafu kuchukua majimbo 10 siyo kigezo cha kushinda kwanza jiulize wameyachukuaje, mengine ni kwa kutumia mahakama na wasimamizi hizo ni kura mbili tu na si za wananchi.

Mimi nahesabu wameshinda kwa kura ya msimamizi na ya mahakama basi.
 
CCM wametumia mbinu chafu kwa kutumia wale makada wao ambao ni wasimamizi wa Tume ya uchaguzi, hakuna pingamizi lililokua jepesi kumvua ugombea kama la yule aliefoji majina kule nzega, kwa biaseness yao hawakuona hilo, wamekuja kumtangaza yule aliekatiwa rufaa na Masha kuwa si raia , wakati kazaliwa nchi hii, na baba Mtz, kwa hiyo kwa mazingira hayo, ndo maana basi kuna majimbo wana[pita bila kupingwa na sikweli kuwa wamepata kura za kutosha .
 
Mi nafikiri wewe umekosa mawazo kabisaaa,, wewe unamuona mwenzako kakuzidi Mbio lakini bado unajipa moyo,, sasa hayo ndio mawazo ya wasio na akili na kukosa Knowledge ya Competition,, Campaign ni competition,, na ukisha ZIDIWA HATA MAJIMBO MAWILI you are the looser,,

Zanzibar hakuna chochote kinachofanyika zaidi ya changa la macho la selikali ya mseto,, huyo Seif munaye mtegemea ni kada wa CCM sasa wewe unakaa eti unajitutumua kutangaza sijui siasa inavyo endelea hapa nchini we unafikiria nini kwa sasa,,

kana Slaa amesha kubali kuwa kunastep wamebugi who are you friend,, nenda KABRUSH KICHWA KISHA NJOO JAMIINI...
sAFARI IJAYO TUNATAKIWA KUWEKA WAGOMBEA NA KUANZA ZA CHINI CHINI MAPEEEMAAAAAA
 

Mkuu sometimes ukichoka inabidi ukalale, otherwise unaweza kukumbwa na yaliyomkuta JK.
 
Hizi thread nyengine hazina kichwa wala miguu!!!!!!!!!
 
Ni kweli CCM wameshashinda kabla ya kupiga kura. Issue ni by how much? Kwa nini wameshashinda? Kwanza Tume ya Uchaguzi ni taasisi ya CCM kiaina kama ilivyo UWT. Uongozi wote wa NEC ni makada wa CCM. Wanaubiri maji mchana usiku wanakunywa mvivyo (wine). Mwandishi Tegambwage ameadika makala akisema yale maadili ya NEC waliosaini vyama vyote ni kulinda maslahi ya chama tawala. Kampeni hazipaswi kuikosoa CCM ila kusema wewe utafanya nini kwa watanzania. What a mockery!

Wote tunamuona Msajili wa nyama Judge Tendwa alivyo shabiki mkubwa wa CCM na hili halina ubishi.
Kilichotokea kwa wagombea wa vyama vya upinzani kuenguliwa mapema ni sawa na kupiga kipenga kwenye mbio za riadha mchezo ukatishwe huku ukiruhusu wengine waendelee na mbio. Hata kama NEC itabadilisha matokeo na kuruhusu wagombea waigie kwenye kinyanganyiro tayari kuna ushindi wa Kisaikolojia kwa CCM. Binafsi naona kheri uchaguzi wa 2005. Safari ni upuuzi mtupu!
 
Wewe sasa umekuja upande wangu,, mimi navishangaa sana hivi viinstitutions ambavyo still vipo chini ya chama na kusahau kufanya majukum ya kinchi,, mi nadhana itafikia hatua jeshi liokoe jahazi la nchi hii inayokenda mrama
 
Tafuta thread nyingine halafu utafakari kabla ya kui-post.
 
Sheikh yahaya katabiri au.Halafu just be specific ni wataalamu gani maanake usijekuta ni wapiga ramli unawaita watalamu manake mzee unatisha 90+15+5=110...Duh! Hongera mzee
 
wana JF tumsamehe huyu mtu maana hajui alisemalo
90 + 15 + 5 = 110%??????!!!!!
 
Sijui ni side effect ya bange?
 
braza hesabu ya kujumlisha inakupiga njenga nini
 
wataalam wameona uchaguzi wa mwaka huu inaweza ukawashangaza
wengi mana dalili zinaonesha JK atashinda kwa 90% akifatiwa na Dr Slaa 15%

Hii itakuwa ushindi wa kishindo

Mpaka sasa Dr Slaa hajaanza kampeni anaogopa aanzie wapi

Jeykey unanifurahisha mno. Naona hesabu ulipata 0%. Is 90% +15% + 5% = 100%?? Sishangai maana hata matokeo ya urais Zanzibar mwaka 95 walibabaika mpaka wakatangaza asilimia za uongo!! Kweli nyie mnajua kuchakachua. Subiri ligi October 31st!!! Umelipwa kiasi gani cha kuja kutudanganya hapa?? Hizi kura ni lazima wagawane tena kwa kunyang'anyana!!! Subiri next week Kampeni za Chadema zianje, wanasubiri kufukia mashimo!!!! Tena ikiwezekana Chadema subirini kwanza ssm wapasue anga kwa asilimia 75% halafu mkamalizie kazi!

 
Nadhani ana ndoto ya kumwibia kura, alidhani atapata 80% lakini akaona JK apate tena 80% ngoja nimwongezee kidogo, wizi mtupu! na hivyo ndivyo wanataka kufanya
 
wataalam wameona uchaguzi wa mwaka huu inaweza ukawashangaza
wengi mana dalili zinaonesha JK atashinda kwa 90% akifatiwa na Dr Slaa 15%

Hii itakuwa ushindi wa kishindo

Mpaka sasa Dr Slaa hajaanza kampeni anaogopa aanzie wapi

Pole sana mkuu maana hizi shule za chini ya mbuyu na za kata ndio madhara yake !! Na bado unataka ziendelee tu na kizazi chako kije kupitia hukohuko !!! Hata hesabu za % kwako ni sifuri kabisa !!!!

JK 90% Slaa 15% Lipumba 5% = JeyKey !!!
 
mbona watu wanalalamika sana kila kukicha ...sasa sijui huwa utafiti unafanyikaje na kwa akina nani.............
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…