Elections 2010 CCM wameshashinda uchaguzi huu

Wakuu,
Siko mbali sana kutoka kwenye jiko la Chama Cha Mapinduzi (CCM) ofisi ndogo a hata makao makuu kwenyewe. Hii nimeipata muda huu kuwa mikakati iliyokuwa imepangwa kupata ushindi wa kishindo wa asilimia 89% imekwama na sasa inasukwa namna ya kupata ushindi wa 83%.
Hatua hiyo inatokana na kutishwa na ujio wa Dk. Slaa katika kinyang'anyiro, amewatisha.
Mbinu zitakazofanyika kupata ushindi huo zinapangwa sasa na jamaa wakiongoziwa na wazee wa riging; ambao wanajua kazi zao.
Ntawajulisha muda
 
Waganga wa kienyeji na wagaguzi mtakuja wengi sana !
 

Kuna jamaa leo alitujia na data hizi eti ssm 95%, Chadema 15% na CUF 5%?? Jumla 110%. We had unbalanced balance sheet!!! Anyway tupe mikakati yao ikiwezekana PM Dr. Slaa usimwage hapa!!
 
unaweza ukawa shekh yahaya wewe....naamini ndiye...endelea kupiga ramli kj kakusikia tafuta wale wapambe wake nawe ukajichotee chako mapema eeehhhh...tuko pamoja ili kuimarisha ufisadi nchini.
 
kama sio upumbavu kwani 83% sio ushindi wa kishindo??//...au shida darasa au madrasa?
 
ungesema imeshinda kwa asilimia 38 ningekuelewa

Nadhani ana maana ktk ule uchaguzi wao ambao chama pekee cha upinzani kilichoshiriki kilikuwa ni TAKUKURU,ambacho kiliambulia viti vichache sana kimojawapo kikiwa ni cha Iringa Mjini!!!!
 
Nadhani ana maana ktk ule uchaguzi wao ambao chama pekee cha upinzani kilichoshiriki kilikuwa ni TAKUKURU,ambacho kiliambulia viti vichache sana kimojawapo kikiwa ni cha Iringa Mjini!!!!

Hivi awa TAKUKURU hawajaweka pingamizi kwa wagombea viti maalum CCM DC machangu na Mama 6 WALIOGOMBEA NAO TABORA NA kmanjaro
 

MS acha habari za Uswazi!
 
Kama uhuru wa kuongea ndiyo hivi basi JF na Mods hawajui maana yake.
 
Kama uhuru wa kuongea ndiyo hivi basi JF na Mods hawajui maana yake.

Mkuu kama watendaji wa CCM akili zao ni kama hizi za hawa sniffers walioletwa hapa, nchi inahitaji mapinduzi ya kweli. Wakiamka akina Mpambalyoto watashangaa sana wao walipambana na risasi za Mjerumani sisi tunashindwa ha kupambana na ujinga wa wanasiasa
 
MODS izi msg zilizochakachuliwa zinafanya nini kwenye Jukwaa la great thinkers?
 
Wewe unafikiri viongozi wa CCM wanatofauti gani na watu kama hawa, viongozi wanajua madudu wanayoyafanya kwa makusudi kwa kiwango chao huko waliko na hawa waliotumwa humu wanafuata maelekezo ya viongozi hao hao huku wakijua wanafanya kwa makusudi. Kwa hiyo hakuna tofauti wanachozidiana ni viwango na sehemu za kazi tu. Kinana na Makamba wanatumia jukwaa kusema Kikwete alianguka kwa saumu hawa wanatumia umember wa JF kusema kitu kile kile.
 
wAKATI KAMA HUU 2005 WALIKUWA NA VITI VYA KUTOPINGWA 60. UPINZANI UMEZIDI KUKOMAA NA KUIMARIKA ON THE CONTRARY
 

Mkuu nakubalina nawe kabisa, kwa kura CCM hawatapata na sasa wanapanga mbinu za KIbaki, na kwa sababu wanajua Watanzania ni waoga hakuna kitakachotokea. Kwa kweli watapindua tu matokeo kama ambavyo wamekuwa wakifanya Zanzibar. Watanganyika tuamke tukatae kabisa , kwanza tuwazidi kwa kura halafu tutamgeukia Jaji Makame, hakuna kulala mpaka kieleweke. Lazima CCM mwaka huu iende kaburini ka KANU ama UNIP
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…