CCM wametoa wapi vifaa vya NEC vya kupigia Kura?

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Salaam Wakuu,

Sasa nimeanza kuelewa Usemi wa Freeman Mbowe(Mwenyekiti wa CHADEMA) aliposema Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) ni Tawi la Chama cha Mapinduzi.

Hivi sasa CCM inafanya uchaguzi wa ndani nafasi mbalimbali. Nimeshangaa kuona wanatumia Karatasi na Masanduku ya kupigia kura ya NEC. Vifaa vya tume ya Uchaguzi kwenye uchaguzi wa CCM na ndani ya Ofisi za CCM. Kweli?

Viongozi Serikali wanaona sawa tu.

Demokrasia Tanzania ipo wap?

Sanduku la NEC kwenye uchaguzi wa CCM

Kumbe Masanduku na Karatasi za kupigia kura za NEC vinapatikana kirahisi hivi? Asante sana Rais Samia na Taasisi yako ya Uraisi

Asante Tume ya Uchaguzi, asante Jeshi la Polisi, Asante Mahakama na wote Mnaohusika kwa Kuruhusu hili litokee ili Dunia ijue Tanzania ni Nchi ya namna gani kwenye maswala ya Vyama vingi.
 
Wamevikodi 😝😝
 
Kumbe Masanduku na Karatasi za kupigia kura za NEC vinapatikana kirahisi hivi? Asante sana Rais Samia na Taasisi yako.

Asante Tume ya Uchaguzi, asante Jeshi la Polisi, Asante Mahakama na wote Mnaohusika kwa Kuruhusu hili litokee ili Dunia ijua Tanzania ni Nchi ya namna gani kwenye maswala ya Vyama vingi.[emoji23][emoji23]
 
Iko Siku Mahera atakamatwa na kufungwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…