CCM wametoa wapi vifaa vya NEC vya kupigia Kura?

Mkuu Kuna NEC ya CCM
 
Nchi bila katiba mpya itaendelea kuwa nchi mfu, kwenye nchi zinazojitambua hapa hapa Africa, zenye NEC huru hili jambo lisingekua la kustaajabisha maana chaguzi zote za vyama vya siasa vingekua vinaendeshwa na NEC, (ili kuleta ile neutrality kwa wagombea)na tuelewe vyama vya siasa vinatakiwa vijisajili na viwajibike kwa NEC sio uchafu wetu wa msajili wa vyama, lini hili litatokea kwetu time will tell ila kwa sasa na generation yetu ya uzuzu huu, ccm wataendelea kutuburuza
 
Wenyewe wanakuambia ni kuwa sababu ni chama dola. Ukiwauliza hizo ofa za kuwa chama dola zipo kisheria? Ukihojiana nao inatakiwa yee mbali nao,hawakawii kutumia ushauri wa Dr Tuli
Wa kukushughulikiaπŸ˜„
 
Sasa nimeanza kuelewa Usemi wa Freeman Mbowe(Mwenyekiti wa CHADEMA) aliposema Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) ni Tawi la Chama cha Mapinduzi.
Umechelewa Sana kuelewa hili
 
TUME YA UCHAGUZI ni Tume ya CCM ikiwa inasimamiwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu ndio inakuwa TUME YA TAIFA ya UCHAGUZI na Wajumbe ni Wale wale
ndio maana Tunataka KATIBA MPYA yenye TUME HURU sio Ujinga kama huo
 
Kuna kitu watanzania hawakukielewa waliposema Chama cha mapinduzi kimeshika hatamu za uongozi hayo yote yanayotokea ni sehemu ya sera hiyo kwa serikali na wala haijawahi kuondolewa wala kukanushwa na serikali. CCM = Government, vyama vingine are either followers or opposition.
 
Samahani mkuu naomba uniulizie bei ya kukodisha sanduku na makaratasi yake nina kauchaguzi kidogo hapa kwenye parokia yangu 😎😎😎😎😎
 
hivi vifaa huwa vinakaa/vinabaki kwenye ofisi za kata baada ya uchaguzi , hakuna dhambi hapo ni kuchukua na kutumia tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…