Ndugai alipotoa TAHADHARI kwa serikali ya wamu ya 6 kuwa nchi yetu itapigwa mnada endapo itaendelea kukopa fedha hovyo toka nje, CCM na jumuiya zake zote walimjia juu. Na hata siku anamwapisha mrithi wa Ndugai mama aliwashukuru wanaccm wa ngazi zote wakiongozwa na wenyeviti wa mikoa kwa kumpigania.
Hali imekuwa tofauti sana kwa Dr. Bashiru. Hatuoni matamshi ya kitaasisi, bali watu binafsi wanaosukumwa na ama kujipendekeza, njaa au chuki binafsi.
Hapa ndipo najiuliza kwann hali hii? Je:-
(a) CCM imemchoka mama?
(b) Dr. Bashiru Ally ana watu (kama mzee Mpili) kiasi cha kumtisha mama na chawa wake?
(c) Dr. Bashiru ni akili kubwa kiasi kwamba viongozi wa ccm wameufyata?
1. Rais amejionea mwenyewe alipofanya ziara kwenye mikoa ya Manyara na Arusha hivi karibuni kwamba alichokiongea Dr Bashiru ni kweli tupu ijapokuwa kuna vikaragosi vya vyombo vya habari pamoja na mwenezi kumpamba sana kwamba kapokelewa na umati wa watu mpaka wanakanyagana wakigombea kumwona bila kujua walikuwa wanataka kujionea wenyewe ni nani huyo anayesifiwa sana wakati maisha yao yanakuwa duni kila kukicha
2. Wala rushwa, waharifu na dhulumati ndani ya hicho chama wanatumia mbinu ya kijeshi (piga saluti sana, tembea kwa ukakamavu, jibu ndio kila kitu hata kwa kisichowezekana ili kuzuia kuhojia zaidi wakubwa wakagundua madudu ndio maana wanasifia hata kinyesi kuwa karibu na chakula kilichotengwa kwa mlo ndio shida ilipo
3. Kwa uongozi wa CCM ulioanza kujipanga kwa sasa rais ajihadhari wanaweza kumdhuru ili mtu wanayemtaka kufanikisha mambo ya kiharifu anakichukua kiti kinyume na matarajio yake
4. Usalama wa taifa waache kuegemea zaidi kuilinda CCM na watendaji wa serikali kuliko kuibua maovu kutoka katika jamii ya watanzania wote wenye itikadi tofauti
5. Ni wakati wake sasa hivi kusimama hadharani kukemea namna anavyodhalilishwa hayati JPM vuinginevyo yajayo yanasikitisha kwa kukumbatia waliokuwa wanamhujumu sasa hivi wakinyemelea vyeo vya juu kabisa ili wafanikishe ajenda zao
6. Rais anatakiwa awe anasikiliza wanaomkosoa kwa kujenga kuliko kuegemea mtizamo ya kisiasa; Dr Bashiru alikuwa katibu mkuu wa CCM, mageuzi aliyoyafanya hadi imani ikaanza kurejea wasifikiri chama kinapendwa hapana; wananchi wanatazama aina ya kiongozi aliyepo madarakani na anamwelekeo upi kwao
Waimba pambio walitakiwa wawe wamekoma tangu kipindi cha Lugora lakini hawakomi mpaka JPM alipochukua hatua kuwawajibisha kwa makosa waliyokuwa wanajifichia kwa kusifia sifia bila tija yoyote.
Sasa hivi kuna wasomi waliobobea eti nao wanasifa bila kuzingatia viwango vya mwelekeo kama una jenga au hapana!!!
"Tujisahihishe", JK Nyerere