Ukubwa siyo mwisho kujifunza, endelea kujifunza utaelewa maana ya dhana y
a dola na matawi yake (vyombo). CCM tunazo kanuni zinazotuongoza kwa wanachama wanaotaka kuchaguliwa au kuteuliwa na chama kwenda kufanya kazi ya uongozi ktk vyombo vya dola.
Kwa lugha nyingine kikanuni tuko sawa kabisa kusema
i) FOMU ya maombi ya kugombea uongozi ktk vyombo vya dola
AU
ii) FOMU ya kugombea Urais Zanzibar /Tanzania
Tofauti ni kwamba namba moja imeandikwa kwa ujumla zaidi maana haijataja hata nafasi ya uongozi ambayo inaenda kugombea mfano Urais, Ubunge au udiwani nk
Lakini namba mbili imekuwa mahsusi 'specific' zaidi, yaani imetaja nafasi ambayo inagombewa (nafasi ya uongozi na eneo) ili kupata nafasi ya uongozi husika ktk vyombo vya dola, kwa miaka mingi fomu za kugombea urais zilikuwa zikiandikwa hivi.
Kwahiyo zote ( i) na (ii) ziko sawa kikanuni, tatizo huenda tumezoea uandishi wa aina flani kwa miaka mingi kwahiyo uandishi ukibadilika kidogo wengine wanaona kuna ajenda flani na kuanza kupotosha, lakini kila kitu kiko sawa kabisa kikatiba na kikanuni.
Mwisho, nimegundua baadhi ya wengi wanaojaribu kupinga au kutoa tafsiri hasi hawajui maana ya DOLA, huenda kuna haja watu wajifunze nini maana ya dola, na wajifunze Chadema inaposema mkituchagua tukashika dola tutahakikisha wanafunzi wanasoma bure mpaka chuo kikuu au tutawaletea maendeleo huwa wanamaanisha nini, huenda wakijua hilo itawasaidia kujuua wanapinga nini.
Nitumie meseji Whatsapp inbox ili nikutumie nakala ya 'soft copy' ya Kanuni ya uteuzi wa wagombea uongozi ktk vyombo vya dola ili upate maarifa.