Kadoda nguku
JF-Expert Member
- Apr 22, 2019
- 332
- 475
CCM wamekuwa wakijinasibu kwamba watashinda kwa kishindo,lakini mbinu pekee wanayofikiria kuitumia ni hii ya mawakala.
Zipo namna mbili za kutumia, mosi ni kuwatimua mawakala wote na vituoni wabaki mawakala wa ccm tu kwa kila kituo, hii mbinu ikifanikiwa matokeo yake hayatakuwa tofauti na yale ya serikali za mitaa, na kwa kuwa CCM hawana chembe ya aibu wataitangazia dunia kwamba wameshinda uchaguzi mkuu kwa kishindo na baada ya hapo maisha yanaendelea kama kawaida ijapokuwa kutakuwa na matukio mengi ya visasi kama mnavyojua Jiwe ni mtu anayependa hayo.
Njia ya pili ni kutoruhusu mawakala kutopata nakala ya matokeo. Ili wapinzani washindwe kwenda hata mahakamani kwa kukosa uthibitisho.
Wapinzani wakifanikiwa kudhibiti hayo maeneo 2 CCM hawatafikisha hata 45% nimefanya utafiti kwa makundi mbalimbali ya wafanyakazi, machinga, wafanyabiashara na wakulima wameendelea kusisitiza kwamba hawajasahau Yale yaliyofanyika miaka 5 ,na wanasema kura nu siri, na maamuzi yako mioyoni mwao.
Kwa sababu kila kona ya nchi hii watu wameagizwa kuhakikisha chama kinashinda kwa kishindo kwa zaidi ya 81% kila eneo na kuna baadhi wameahidiwa na hyo mbinu ya mawakala ndio itakayotumika ni vema upinzani kuhakikisha inakuja na mbinu mbadala ya kukabiliana na hiyo mbinu haramu.
Wapinzani wakifanikiwa hayo ni dhahiri kwa Mara ya kwanza kizazi hiki kinaingia katika historia ya kushuhudia chama kilicholeta uhuru kinaondoka madarakani, na hii historian ya kudumu
Suluhu nzuri ni Chadema kuweka mawakala wengi. Mfano, kila eneo mawakala wa ACT, Chauma wanakuwa ni watu toka chadema ili wakiwazuia wachadema bado anabaki yule wa chauma na ACT, Wakimtoa wa chadema na ACT, anabaki wa chauma. Na kama kuna sehemu vyama vingine vinashangaa shangaa unampa barua mtu wa chadema unagonga mhuri wa katibu wa nccr wilaya anaenda kuwa wakala wa NCCR anachoma ndani anakwenda kufanya kazi ya kumtetea mgombea wa Chademà.