Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Kuna masuala yapo kiroho. Kuna mambo yanatupata leo kutokana na misingi iliyowekwa kiroho ambayo bila kuondoa mzizi mkuu kamwe hatutakuja kupata suluhisho.
CCM wanaishi kwa uongo na hii ndo dhambi kubwa itakayoendelea kulitesa hili Taifa hadi pale yatakapotokea mabadiliko kwa CCM kuondoka.
Chanzo cha haya kilianza wakati Nyerere alivyochagua kuishi kwa uongo ili kupandikiza chuki kwa Watanzania dhidi ya aliyekuwa swahiba wake na moja ya kipenzi cha watanzania Bw. Oscar Kambona( Katibu Mkuu wa kwanza wa TANU).
Matatizo mengi yanayoikumba Tanzania ya leo mzizi wake ni Nyerere kukataa ushauri wa Kambona kuhusu sera bora za kuiongoza Tanzania baada ya Uhuru.
Wakati Nyerere alitaka kuchukua sera za ujamaa na kujitegemea, Kambona alitaka kuchukua njia tofauti ambayo ingehakikisha ustawi mkubwa wa Wananchi na maendeleo kwa miaka mingi mbeleni.
Tutakumbuka utaifishaji wa viwanda, mabenki na taasisi mbalimbali halikuwa jambo lilioungwa mkono na Kambona ambapo pamoja na kutoeleweka kipindi kile alikuja kueleweka pale Watanzania waliposhindwa kuendesha viwanda na taasisi hizo hadi vilipokuja kufa kwa aibu.
Dhambi aliyoifanya nyerere ya kutengeneza propaganda dhidi ya Kambona ili kuwafanya Watanzania wapumbazwe na wasifikiri kuhusu hoja za Kambona ndo dhambi kubwa inayoendelea kulitafuna Taifa letu hadi leo.
Hadi leo CCM hawaishi kwenye ukweli, wanauchukia ukweli na ukitaka kugombana nao jaribu tu kuwaambia ukweli.
Uongo wa CCM umeendelea kuitafuna hii nchi mpaka sasa kwenye mambo mengi wananchi wameuzoea uongo. Viongozi kujifanya kukumbatia dini ili kuwafanya wanachi kuwa makondoo huku wakikikuka misingi inayowekwa na dini zenyewe kama kuiba uchaguzi limekuwq jambo la kawaida sana nchini.
Tunayoona leo kwa wanaosema ukweli dhidi ya CCM na Serikali kutukanwa, kusemwa vibaya na kudhalilishwa ni mambo aliyoyaasisi Mwl. Nyerere dhidi ya a true son of Tanganyika Oscar Kambona.
Ukiskia sijui Wastaafu wanawashwawashwa, umekula nchi sasa umestaafu kaa kimya, Sijui kwa nini usiseme kwenye vikao unaongea na waandishi wa habari jua tu hizi ni siasa za ulaghai zilizoasisiwa na CCM ya Nyerere ambazo kwa miaka mingi zimeendelea kuwa kama kansa kwa Taifa letu.
Kila siku na nitasema. Pona ya nchi yetu ni siku CCM itakapoondoka madarakani. Ni pale tutakapopata Katiba inakayoweka misingi mizuri ya kuliendesha hili Taifa.
R.I.P Oscar Kambona
You will remain to be a True Hero of Tanzania.
Siku nikiwa Rais, Nishani ya kwanza nitaitoa kwa Oscar Kambona. Ingawa najua wataipokea wajukuu wa vitukuu vyake ila lazima hili jambo litafanyika
Insha Allah!