<table class="contentpaneopen" border="0"><tbody><tr><td class="contentheading" width="100%">Dk Slaa: Chagua Chadema kwa mabadiloko </td> <td class="buttonheading" align="right" width="100%">
Send to a friend </td> </tr> </tbody></table> <table class="contentpaneopen"><tbody><tr> <td class="createdate" valign="top"> Wednesday, 20 October 2010 09:21 </td> </tr> <tr> <td valign="top"> <script type="text/javascript">digg_url = 'http://www.mwananchi.co.tz/habari/5-habari-za-siasa/5708-dk-slaa-chagua-chadema-kwa-mabadiloko'; digg_title = 'Dk Slaa: Chagua Chadema kwa mabadiloko'; digg_bodytext = ''; digg_bgcolor = '#ffffff'; digg_window = 'new';</script><script src="http://digg.com/tools/diggthis.js" type="text/javascript"></script>0diggsdigg
Sheilla Sezzy,
Mwanza
MGOMBEA urais kupitia Chadema Dk Willibrod Slaa amesema mabadiliko ya kweli yatakuja iwapo Watanzania wataichagua Chadema.
Dk Slaa aliyasema hayo wakati akijibu maswali kutoka kwa mtangazaji Ranfred Masako katika kipindi kinachorushwa na ITV cha uchaguzi 2010 baada ya kuulizwa ni wapi atapata fedha za kutoa elimu bure, afya bure na kupunguza gharama za vifaa vya ujenzi.
DK Slaa akijibu swali hilo, alisema atatumia kodi za watanzania kutekeleza huduma hizo bure na kufafanua kuwa kuna aina mbili za kodi ambazo ni ya moja kwa moja na nyingine ni siyo ya moja kwa maoja.
Alisema kila kitu ambacho mtanzania anakinunua anakuwa amekilipia kodi bila ya yeye mwenyewe kujua kuwa analipa kodi na kudai kuwa kodi hiyo ya moja kwa moja inaingizia serikali fedha nyingi sana.
Alisema Tanzania ina rasilimali nyingi za madini ambazo zinaingiza fedha nyingi na kudai kuwa zimekosa msimamizi na kusababisha fedha nyingi kupotea.
Tumejaliwa misitu yenye miti ambayo inavunwa magogo na kusafirishwa nchi za nje, hizo ni fedha za Matanzania ambazo zinapotea, tuna taarifa ya serikali ambayo inaonyesha wizi wa mabilioni ya magogo, tuna samaki wengi sana ambao wanauzwa hadi nchi za nje na watanzania wanabaki wanakula mapanki, alisema.
Akizungumzia rasilimali ya wanyama alisema kuwa Tanzania ina tembo wengi sana ambao hawana gharama zaidi ya kula manyasi hao nao wanaingiza fedha ambazo zinaongeza pato katika uchumi wa Tanzania .
Akikumbushia sakata la mafisadi Dk Slaa alisema kwamba alionekana mpiga kelele bungeni, lakini nilipo Sh 9 bilioni, zilirudishwa na mafisadi na kufafanua kuwa kiasi kilichorejeshwa ni kidogo ikilinganishwa zilizochukuliwa na mafisadi. Alisema fedha za Meremeta Sh 150 bilioni ni jasho la Watanzania ambazo pia zimepotea.
Pamoja na hayo yote alisema kuwa enzi za mwalimu kulikuwa hakuna rasilimali zote hizo, lakini watanzania walisoma bure pia walipata huduma ya afya bure kwanini leo watu wanashindwa kusoma bure pamoja na kupata huduma za afya bure,alihoji Dk Slaa.
Akitolea mfano nchi ya Kenya alisema kuwa nchi hiyo haina rasilimali kama zilizopo Tanzania, lakini elimu na afya katika nchi hiyo ni bure.
Dr Slaa aliwataka watanzania kukichagua Chadema na kusema kuwa ni tumaini jipya kwa watanzania japokuwa wapinzania wao wanawabeza na kusema kuwa hawana jipya zaidi ya ufisadi.
Nasema hivi tutaendelea kuzungumzia ufisadi pamoja na sera nyingine nyingi, tuchagueni ili tuwaonyeshe yale ambayo CCM wameshindwa kuyafanya kwa miaka 50, tupeni miaka mitano tu tuwafanyieni maendeleo ya kweli,alisema Dk Slaa.
Alisema kuwa kama wanabisha kuwa Dk Slaa hawezi kuleta maendeleo waende Karatu waone yale ambayo yalishindikana kwa CCM, lakini Chadema imeweza kuyatatua
</td></tr></tbody></table>