CCM: Wananchi hawajawahi kudai Katiba mpya bali hilo ni takwa la wanasiasa kwa maslahi yao binafsi

CCM: Wananchi hawajawahi kudai Katiba mpya bali hilo ni takwa la wanasiasa kwa maslahi yao binafsi

Paf

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2021
Posts
1,703
Reaction score
3,307
Akiongea na waandishi wa habari Leo 11/8/2021 ametoa maelekezo mwenye halmashauri na kisha kukaribisha maswali.
Moja ya swali ilikuwa Katiba mpya.
Muuliza swali amejenga hoja kwa kubalance vizuri sana.

Majibu yake ni Kwamba Katiba mpya ni hitaji la wanasiasa na Si wananchi kwakuwa mabango ya kudai Katiba ni yakutafuta madaraka tu.

Amemhoji umewaona wananchi wakiwa namabango wakidai katiba?

Swali langu,

1. Mwananchi ni yupi?

2. Mwanasiasa ni yupi?

3. Kudai katiba kunahalalisha vipi kuwa huyu ni mwanasiasa?
 
Katibu mkuu wa CCM ndugu Chongollo amehoji kama kuna siku wananchi wamewahi kubeba mabango wakidai katiba mpya?!

Kadhalika Chongollo amehoji Tume huru ya uchaguzi inamsaidia nini mwananchi wa kawaida hadi aidai?

Kimsingi katiba mpya ni dai la wanasiasa kwa maslahi yao na siyo hitaji la wananchi kwa sasa a esisitiza Chongollo

Source: Channel ten

My take; Nakubaliana na Katibu u
 
Kwahiyo itapatikana siku wa kiifuata manjiani sio?
 
Katibu atakuwa Genius. Nia ya swali ndo jibu. Na Ukweli wa maisha yetu Ndo dira. Tell me. Mwaka Jana uchaguzi. Nchi maskini Sasa ni kazi tu. Katiba mimi inanisaidia Nini kwa Sasa katika kupunguza changamoto zangu za maisha ? Kwa Sasa. Baada ya uchaguzi mwaka Jana.

Lini watanzania tutatulia na kuwaza maendeleo. Katiba katiba. Then what. Mambo haya yatakuja tu.
 
"Wapi uliona wananchi wamedai katiba mpya, dai la katiba mpya ni letu sisi wanasiasa, hivi kupitia kupatikana kwa katiba mpya itawaletea wananchi unga? Katiba mpya inayodaiwa na wanasiasa ni kwa ajili ya kutengeneza nafasi za uongozi na madaraka"

Daniel Chongolo,Katibu Mkuu wa CCM
 
Katibu mkuu wa CCM ndugu Chongollo amehoji kama kuna siku wananchi wamewahi kubeba mabango wakidai katiba mpya?!

Kadhalika Chongollo amehoji Tume huru ya uchaguzi inamsaidia nini mwananchi wa kawaida hadi aidai?....
Hivi hawa CCM mbona wanaongea upumbavu sana. Tangu lini wanasiasa sio wananchi?
 
Back
Top Bottom