Tetesi: CCM wanaoutamani urais 2025 Wakinyimwa kugombea kutimkia upinzani na kujaza fomu za kugombea Urais

Kuna wimbi limeanza kujinadi kuchukua fomu ya kugombea Urais kupitia CCM na kundi hilo linakubalika.

Iwapo fomu ya kugombea Urais kupitia ccm itatolewa fomu moja ni wazi kuwa wagombea hao wataamua kuchukua fomu za kugombea urais kupitia upande wa pili.

Wananchi walio wengi wamekumbwa na taharuki ya kupanda kwa maisha kupita kiasi ambapo wanatarajia kufanya mabadiliko ya kiuongozi 2025.

Pia kuna kila dalili wabunge wengi wa ccm kukutana ha upinzani mkubwa ndani na nje ya ccm kwani wameshindwa kutafsiri au kuelezea hali ngumu ya maisha iliyopo majimboni mwao.

Baadhi ya wananchi mfano Jimbo la monduli wananchi wanapata mlo mmoja kwa siku na hakuna msemaji wa ccm amefika kujionea au kuwafariji wananchi hao
May b tuongelee 2030 lakini 2025 Rais Samia Suluhu atapita bila kupingwa maana amefanya maendeleo makubwa sana Tanzania
 
Tupambanie KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.
Nakubaliana nawe kwamba tunahitaji katiba mpya, lakini isiwe ile rasimu ya tume ya Warioba.

Kama umewahi kuipitia ile ni takataka. Katiba bora haiwezi kuandikwa na wanasiasa wenye maslahi na katiba wanayoiandika.
 
Ukiachana na kuwa mwanasiasa, Warioba ni mwanasheria anayeheshimika sana kitaifa na kimataifa
 
Nakubaliana nawe kwamba tunahitaji katiba mpya, lakini isiwe ile rasimu ya tume ya Warioba.

Kama umewahi kuipitia ile ni takataka. Katiba bora haiwezi kuandikwa na wanasiasa wenye maslahi na katiba wanayoiandika.
Takataka ni Ile ilopelekwa Bunge maalum wakajazana wanaccm na kupelekea CHADEMA kujiondoa.

Tunataka Tuanzie pale Warioba alipokamilisha KAZI.

Tujadiliane nani watuwakilishe ktk Bunge la Katiba. Ameeeen
 
Kuna wimbi limeanza kujinadi kuchukua fomu ya kugombea Urais kupitia CCM na kundi hilo linakubalika.

Iwapo fomu ya kugombea Urais kupitia ccm itatolewa fomu moja ni wazi kuwa wagombea hao wataamua kuchukua fomu za kugombea urais kupitia upande wa pili.

Wananchi walio wengi wamekumbwa na taharuki ya kupanda kwa maisha kupita kiasi ambapo wanatarajia kufanya mabadiliko ya kiuongozi 2025.

Pia kuna kila dalili wabunge wengi wa ccm kukutana ha upinzani mkubwa ndani na nje ya ccm kwani wameshindwa kutafsiri au kuelezea hali ngumu ya maisha iliyopo majimboni mwao.

Baadhi ya wananchi mfano Jimbo la monduli wananchi wanapata mlo mmoja kwa siku na hakuna msemaji wa ccm amefika kujionea au kuwafariji wananchi hao
Una chuki na lowassa wewe, sasa wananchi kula mlo mmoja mbunge atazuiaje? Agawe milo mingine ambayo watu hawana? Suala la umasikini halipo monduli tuu.
 
Pazia la hekalu lazima lichanike. Mafisadi huku na wazalendo huku. Liwalo na liwe, ikibidi iwe hivyohivyo itakavyokua tu, hii nchi sio ya vikongwe kadhaa vya pwani. hatukubali ng'o!
 
Iwapo fomu ya kugombea Urais kupitia ccm itatolewa fomu moja ni wazi kuwa wagombea hao wataamua kuchukua fomu za kugombea urais kupitia upande wa pili.
Kama unaijua CCM, issue ya iwapo haipo!. 2025 zinatolewa fomu mbi tuu za urais, moja ni urais wa JMT na pili ni ya urais wa ZnZ!.

Kama ni mwana CCM wa ukweli, hili wote wanalijua, na akitokea mwana CCM amepa ga kugombea urais 2025, huyo atakuwa sii mzima !.

Kama kuna mwana CCM atahama CCM ili agombee urais wa JMT kupitia upinzani, huyo atakuwa sio tuu sii mzima!, huyo atakuwa ni ... kabisa maana Kuwa kichaa sio mpaka kuokota makopo! Je, Tanzania tuna vichaa wengi kuliko tunavyojidhania?
P
 
Ni Mama Samia mpaka 2030, acha kupiga ramli zako hapa na kupima upepo, Wana CCM tuna Imani na mama Samia na ndio Nahodha wa kutuvusha mpaka hiyooo 2030, Kauli yetu Ni moja tu kuwa Ni mama tu
 
Pia ieleweke kuwa Hapa nchini Hakuna chama Wala mtu yeyote awezaye kuitikisa CCM, hayupo mtu huyo na Wala bado hajazaliwa , Na hakuna mtu yoyote mwenye Akili Timamu anayeweza kutoka na kuihama CCM halafu atarajie kupata na kuwa Rais wa Tanzania kupitia upinzani, Nasema mtu huyo atakuwa anajidanganya maana watanzania wote Wana Imani na CCM na Wana amini kuwa Rais Bora ni lazima awe na atoke CCM ,
 
Takataka ni Ile ilopelekwa Bunge maalum wakajazana wanaccm na kupelekea CDM kujiondoa.

Tunataka Tuanzie pale Warioba alipokamilisha KAZI.
Kilichopelekwa bungeni ni tofauti na rasimu ya tume ya Warioba?!

Nani alifanyia mabadiliko! Angalia usiwe mzushi.
 
Ilopelekwa original, ilipofika bungeni mazombie wakaanza kuchomoa ya muhimu na kuchomekwa mapuuza.
 
Kuna wimbi limeanza kujinadi kuchukua fomu ya kugombea Urais kupitia CCM na kundi hilo linakubalika.

Iwapo fomu ya kugombea Urais kupitia CCM itatolewa fomu moja ni wazi kuwa wagombea hao wataamua kuchukua fomu za kugombea urais kupitia upande wa pili.

Wananchi walio wengi wamekumbwa na taharuki ya kupanda kwa maisha kupita kiasi ambapo wanatarajia kufanya mabadiliko ya kiuongozi 2025.

Pia kuna kila dalili wabunge wengi wa ccm kukutana ha upinzani mkubwa ndani na nje ya CCM kwani wameshindwa kutafsiri au kuelezea hali ngumu ya maisha iliyopo majimboni mwao.

Baadhi ya wananchi mfano Jimbo la monduli wananchi wanapata mlo mmoja kwa siku na hakuna msemaji wa ccm amefika kujionea au kuwafariji wananchi hao
Watajisumbua bure tu, kwa Katiba hii, na NEC hii ni sawa na kujilisha upepo tu. Sanduku la kura siku hizi halina thamani tena.
 
Back
Top Bottom