CCM wanataka Mbowe aendelee kukaa madarakani kwa sababu hizi hapa

CCM wanataka Mbowe aendelee kukaa madarakani kwa sababu hizi hapa

Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya ndugu wanaJF. Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha wala kuwapotezea muda. Baada ya CCM kumpigia Mbowe kelele kwa muda mrefu kwa sababu za kuchakachua katiba ya CHADEMA ili akae madarakani milele, ghafla wamebadilisha gea angani na kuanza kumuunga mkono Mbowe dhidi ya Tundu Lissu. Sababu kuu za kuchukua uamuzi huu, ni kama ifuatavyo:

Tundu Lissu akiingia madarakani machawa na mafisadi wote watanyongwa hadharani
Mafisadi wa CCM pamoja na chawa wao wanahaha kumzuia Tundu Antipas Mugway Lissu asiingie madarakani kwa kuwa Lissu akikwaa madaraka ya uenyekiti na kisha akagombea urais na kushinda, hatakuwa na simile na mafisadi pamoja na chawa wao walioigeuza hii nchi kuwa shamba la bibi yao. Fikiria mafisadi hawa wamezoea kula bila kunawa na chawa wao wanawanyonya kila siku bila shida yoyote, halafu atokee mtu jasiri na makini anayejali maslahi ya wanyonye, awakamate mafisadi wote awanyongee mbali, unadhani watakubali kirahisi? La hsha! Sio mafisadi wala chawa watakaokubali kitendo cha aina hii.

Ndege wa mbawa moja huruka pamoja
Ung’anganizi wa madaraka wa CCM ambao wamekaa mamlakani tangu mwaka 1960 hadi leo na bado hawaonyeshi dalili yoyote ya kuachia madaraka kwa gharama yoyote ile, unafanana kwa asilimia 100% na ung’ang’anizi wa madaraka wa Mbowe ambaye amekalia kiti hicho kwa muda wa miaka 20 na bado haonyeshi dalili yoyote ya kukiachia.

Hivyo, basi CCM wanatamani Mbowe aendelee kukaa madarakani ili atumike kama rejea pale wanapohojiwa kuhusu ung’ang’anizi wa madaraka. Ukiwauliza watakujibu: “Mbona Mbowe yeye hataki kuachia madaraka?”.

Walishindwa kumuua kimwili sasa wanataka kumuua kisiasa
Lissu alinusurika kifo baada ya kupigwa risasi 26 na kikosikazi cha watu wasioujulikana. Hata baada ya kupigwa risasi hizo, bado alirudi kukabiliana na watesi wake mwaka 2020 akizunguka nchi nzima licha ya kuwa mwili wake umejaa vyuma kila mahali kufuatia upasuaji aliofanyiwa huko Ubelgiji. Na si kuzunguka tu bali alikuja na moto mkali kama aliokuwa nao mwaka 2015. Ndipo CCM baada ya kuona wanaenda kuangukia pua, wakaamua kuiba uchaguzi wote kwa maslahi finyu ya matumbo yao yasiyoshiba kamwe.

Kwa hali kama hii na kwa ujasiri usiotetereka wa Lissu, CCM hawawezi kukubali kamwe kumuachia mwamba huyu aingie madarakani ndani ya CHADEMA na hatimaye awe rais wan chi hii. Lazima wahahe huku na huku kama fisi wenye njaa kumzuia asisogelee ikulu kwani wakimuachia aingie madarakani, wamekwisha!

When confronted with two evils, choose the least
Waingereza wanasema kwamba ukikutana na vikwazo viwili, utachagua kikwazo kilicho rahisi zaidi. Hapa CCM wameona afadhali waende na Mbowe kwa kuwa wanammudu kuliko Tundu Lissu, mfupa ambao ulimshinda Magufuli.

Juzi nimesoma kwenye mtandao wa twitter kwenye akaunti ya Maria Sarungi ameandika mambo haya: “Ukitaka kumuua Tundu Lissu, utakufa wewe utamuacha Lissu anaendelea kuishi”. Hii kauli ya Maria imenikumbusha tukio la mwaka 2017 ambalo Lissu alilonusurika kufa kwa risasi 26 na tukio la mwaka 2020 lililomuingiza Rais Samia madarakani baada ya kuhudumu kama Makamu wa Rais kwa kipindi kifupi.

Kwa sababu hii, kila mwanaCCM sasa anamhara Tundu Lissu na hawataki kabisa aingie madarakani kwa kuhofia kuwa huenda Lissu akalipiza kisasi, licha ya kuwa Lissu sio mtu wa kulipiza visasi. Visasi hulipizwa na watu waoga, waovu na wasiomjua Mungu. Na watu wa aina hii wamejaa tele ndani ya CCM.

Hitimisho
Kabla ya Lissu kuonyesha nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA inayoshikiliwa na Mbowe kwa kipindi cha miaka 20, CCM walikuwa wanapiga kelele kubwa sana na kumuita Mbowe kuwa ni dikteta na king’ang’anizi wa madaraka. Hadi walifikia hatua ya kumtumia kada maarufu wa CCM (msajili wa vyama vya siasa) aingilie kati apangue katiba ya CHADEMA kuondoa kifungu kinachoondoa ukomo wa mwenyekiti wa chama kukaa madarakani.

Hata humu JF baadhi ya makada wa CCM, wakiwemo MamaSamia2025, Lucas Mwashambwa na ChoiceVariable, walikuwa mstari wa mbele kumbrand Mbowe majina ya ajabu na kumuita dikteta. Wakati CCM wanamsakama Mbowe kwa kung’ang’ania madaraka kwa miaka 20, Profesa Lipumba amekuwa mwenyekiti wa CUF kwa kipindi cha miaka 33 lakini hawajawahi kumlaumu wala kumuuliza kitu chochote!

Baada ya Lissu kuonyesha nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti, ghafla Mbowe amegeuka kuwa malaika sasa wanamsifu na kumpamba wakitaka aendelee kukaa madarakani hadi Yesu atakaporudi. Hivi ndivyo unafiki wa miCCM ulivyo. Hii mijamaa ni minafiki kuliko popo. Umalaika wa Mbowe umetoka wapi ghafla hivi? Yakhe hamna khaya! MiCCM ina ujasiri wa kujifunika shuka moja na nyoka ilmradi tu wawe na maslahi na nyoka huyo.

Nawasilisha
Duuh
 
tundu-lissu-the-presidential-candidate-of-tanzanias-main-opposition-chadema-party-speaks-to.jpg

Tundu Lissu is a Tanzanian politician, lawyer, and human rights advocate, known for his outspoken criticism of the government and his advocacy for democracy and good governance. He is a prominent member of the Chadema (Party for Democracy and Progress), the main opposition party in Tanzania.

Lissu gained international attention for his role as a Member of Parliament (MP) for Singida East and his vocal opposition to the policies of former President John Magufuli. He was particularly critical of the government's approach to political freedoms, human rights, and press freedom, as well as its handling of the economy and its authoritarian tendencies.

In 2017, Lissu was shot multiple times in a targeted assassination attempt outside his home in Dodoma, Tanzania's capital. He survived the attack but was critically wounded and spent several months in medical treatment in Belgium. The shooting raised suspicions that it was politically motivated, as Lissu had been a vocal critic of the government. Despite this, the Tanzanian government did not take significant action to investigate the attack.

Lissu returned to Tanzania in 2020 after recovering and again ran for the presidency against John Magufuli in the 2020 general elections. His candidacy was marked by claims of election irregularities and a highly contested result, with the government of Magufuli being accused of suppressing opposition and restricting the freedom of the press.

After Magufuli's death in 2021, Lissu continued to be a key figure in Tanzanian politics, advocating for political reforms, democracy, and justice in the country.
 
Naona kabisa CCM wanakaribia kuiua CHADEMA kwa kumsapoti Mbowe aibe kura na kisha team Tundu Lissu kuhamia ACT
 
Back
Top Bottom