Pre GE2025 CCM wanatengeneza "elite clique"?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hiki ulichoandika kilikuwepo Bangladesh hadi Waziri wake Mkuu Sheikha Hasina alipofurushwa mwaka jana kwa sababu hiyo hiyo.

Wao Bangladesh walienda mbali waliweka kwenye sheria zao za nchi kuwa ni lazima watoto wa viongozi waliopigania uhuru watengewe ajira kwa asilimia 5 kwa ya ajira zote zinazopatikana nchini humo. Hata hapa CCM wanaweza kuweka huo utaratibu maana wameonesha kwa vitendo tayari kuwa huwezi kupata kazi kama wewe siyo mwanachama wa ccm
CCM kila siku tabaka lao la watawala hupiga propaganda kuwa yanayotokea Kwa wengine hapa haiwezi kutokea.

Tabaka la watawala wanaamini wamemdhibiti kila mtu na wanaona wamefanikiwa kutengeneza "zombies" wanaotetea tabaka la watawala bila ya kujijua.
 
Watu mnaojua kiingereza mnaweza kunisahihisha kama neno nililolitumia siyo sahihi. Kiranga na Nyani Ngabu msaada tutani.

Kwa mtazamo wa kijuujuu huwezi kuona kinachotengenezwa na CCM hasa viongozi wake wa juu.

CCM inatengeneza aina fulani hivi ya usultani ndani ya chama hicho na Kwa nchi kwa ujumla.

Sasa hivi kwa mfano mtu anaweza kudhani viongozi wa CCM hutoka kusikojulikana na kuwa viongozi wa chama hicho. Lakini ukweli wa mambo wenye chama chao ndiyo huamua nani ashike nafasi ipi ndani ya CCM.

Nimewaza kuwa kama John Nchimbi akifanikiwa kuwa Makamo wa Rais na baadae kuwa Rais wa Tanzania, nini kitazuia Ridhiwani Kikwete kuwa Waziri Mkuu wakati huo?

Mtoto wa Mwigulu Nchemba, huko mbele ya safari si ndiyo anatayarishwa kurithi ubunge wa baba yake?

Mifano ni mingi itoshe tu kusema kuwa ndani ya CCM kunatengenezwa kizazi Cha kisultani ambacho bila kuwa sehemu yake ama kukubaliwa na wao, itakuwa ni ngumu kwa mtu mwingine nje ya koo hizo teule ndani ya CCM, kuwa kiongozi.

Nawaza Kwa mfano bunge likiisha, Ridhiwani na Salma Kikwete watapeleka kwenye familia Yao kiinua mgongo cha shilingi ngapi?

Bila kusahau kuwa Salma Kikwete alipendekeza Bungeni kuwa wake wa waliokuwa viongozi wakuu nao pia wapewe kiinua mgongo. Akipewa atakuwa na ngapi?

Akirudi nyumbani anakutana na Mzee naye analipwa kila kitu sawa na 80% ya aliyeko madarakani.

Nenda Kwa kina Hussein Mwinyi, kina Amani Karume, kina Nyerere na wengineo.

Sijui kama kina Lucas Mwashambwa ChoiceVariable na kaka yao johnthebaptist watanielewa.

CCM
Kalamu Nguruvi3
Usisahau, JPM alitaka kuvunjilia hii kitu, ila masikini wengi hawakumwelewa.
 
ASINGEWEZA!!

Wenye chama chao kama unavoona wameshafanya mazingaombwe yao huko Dodoma.

Mnoa kisu siyo mwenye kisu😂
 
Mkuu umegusa mlemle. Hawa majitu ya CCM bila kuwa mwanaukoo au chawa, utasubiri sana kuingia kwenye mfumo.
 
Alishindwa mpaka kifo. Usisahau Afande RPC Nchimbi alikuwa kigogo wa CCM ukumbuke na sasa kijana wake anakuwa Makamu wa Rais.
 
Kuna misukule Yao haijastuka. Utasikia yule Mkuu wa mkoa fulani mbona hana ukoo na waliokuwa viongozi?

Wanajisahaulisha kuwa hata hao wengine wanapewa nyadhifa walizo nazo Kwa kujikomba, kuwa wapambe, kukubali utumwa wa fikra, na zaidi ya yote kukubali kuwa daraja la pili la watu ndani ya CCM.
 
Alishindwa mpaka kifo. Usisahau Afande RPC Nchimbi alikuwa kigogo wa CCM ukumbuke na sasa kijana wake anakuwa Makamu wa Rais.
Tena nimesoma kitabu chake kimoja kikielezea mambo ya falsafa. Zama hizo.

Wenyewe CCM watasema maji hufuata mkondo.
 
Ulaya kulikuwa na malkia mmoja alikuwa mjinga hivi. Aliulza ni kwa nini watu wa nchi yake wanaandamana, wasaidizi wake wakamwambia ni kwa kuwa hawana mikate. Yule malkia mjinga akajibu kirahisi tu, "si wale keki?"

Ujinga hauna kwao kila mahali upo.
Sasa huo mfano wa kijinga kabisa umegusia lolote kuhusu swali husika la hoja zenu chadema ni zipi haswa?!!! Maana naona mnakesha mitandaoni humu kupiga kelele zisizoeleweka......yaani nyie ni kelele tu. Mi nawazungumzia chadema ambao ni kama laki 7 hiv kwa sasa nchi mzima, siwazungumziii wananchi ambao wako busy kutafuta mikate yao ya Kila siku kupitia miundombinu na mifumo imara ya kiuchumi liyowekwa na mama Samia, The Mother of Modern Tanzania
 
Hao CHADEMA laki saba siyo wananchi? Nyie ndiyo wale mnaopendwa na tabaka tawala. Mko kama Nyuki wa mashineni.
 
Kwani Familia ya Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete ndio Imejaza nafasi zote za uwaziri,ukuu wa Mkoa,wilaya,ukurugenzi wa halmashauri,Ma Das,Ma Ras,wabunge zaidi ya mia 3, Madiwani ,ma DSO na wengine wengi tu. Nafasi ngapi zipo hapa Nchini? je hiyo Familia ya Kikwete Imejaza nafasi hizo zote?

Kwani Mtela Mwampamba ambaye ni DAS huko Songea ni mtoto wa Kikwete? Juliana Shonza ambaye ni mbunge naye ni mtoto wa Kikwete?

Acheni mawazo ya kijinga na ubaguzi.acheni wivu wa kijinga jinga hapa..Mimi ni CCM na sioni ubaya mtoto wa kiongozi kuwa kiongozi ikiwa ana sifa zote zinazohitajika katika nafasi husika . Kuwa mtoto wa kiongozi hakumzui yeye kuwa kiongozi wala kupambania nafasi fulani ya uongozi.

Ndio Maana unaona George Bush alikuwa ni Rais wa Marekani miaka michache tu baada ya baba yake naye kuwa Rais. Mtoto wa mchungaji hazuiliwi kusomea na kuwa mchungaji ikiwa ana wito huo na kaitwa na Mungu kwa kazi hiyo.

Kikubwa ni lazima ufahamu uongozi ni Karama,ni kipawa ni kibali kutoka kwa Mungu. Siyo kila mtu anaweza kuwa kiongozi au kuongoza watu. Kuongoza watu ni kazi ngumu yenye kuhitaji akili,busara,hekima ,umakini na utulivu wa kiakili. Siyo kazi ambayo kila mmoja anaweza kuifanya.
siyo kazi ambayo Kila mmoja anaweza ifanya.
 
Hivi Waziri wa mambo ya nchi za nje ni mtoto wa Marehemu Sheikh Thabit Kombo?
 
Kwani Familia ya Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete ndio Imejaza nafasi zote za uwaziri,ukuu wa Mkoa,wilaya,ukurugenzi wa halmashauri,Ma Das,Ma Ras,wabunge zaidi ya mia 3, Madiwani ,ma DSO na wengine wengi tu. Nafasi ngapi zipo hapa Nchini? je hiyo Familia ya Kikwete Imejaza nafasi hizo zote?

Kwani Mtela Mwampamba ambaye ni DAS huko Songea ni mtoto wa Kikwete? Juliana Shonza ambaye ni mbunge naye ni mtoto wa Kikwete?

Acheni mawazo ya kijinga na ubaguzi.acheni wivu wa kijinga jinga hapa..Mimi ni CCM na sioni ubaya mtoto wa kiongozi kuwa kiongozi ikiwa ana sifa zote zinazohitajika katika nafasi husika . Kuwa mtoto wa kiongozi hakumzui yeye kuwa kiongozi wala kupambania nafasi fulani ya uongozi.

Ndio Maana unaona George Bush alikuwa ni Rais wa Marekani miaka michache tu baada ya baba yake naye kuwa Rais. Mtoto wa mchungaji hazuiliwi kusomea na kuwa mchungaji ikiwa ana wito huo na kaitwa na Mungu kwa kazi hiyo.

Kikubwa ni lazima ufahamu uongozi ni Karama,ni kipawa ni kibali kutoka kwa Mungu. Siyo kila mtu anaweza kuwa kiongozi au kuongoza watu. Kuongoza watu ni kazi ngumu yenye kuhitaji akili,busara,hekima ,umakini na utulivu wa kiakili. Siyo kazi ambayo kila mmoja anaweza kuifanya.
 
Attachments

  • IMG_8869.jpeg
    IMG_8869.jpeg
    53.9 KB · Views: 1
Hapo nimeandika kwa ufupi sana huku nikiwa shambani
Ni kweli maana siku hizi chawa mlioko kwenye ofisi za ccm huwa mnasema mko shambani, na sababu hasa ni fedha za kuuza bandari mnarushiwa makombo ili mtetee majizi.
 
Back
Top Bottom