Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yeyote mwenye kuweza tukimpa ufalme au umalkia sio mbaya.. kwani tunachotaka si haki na maendeleo?🤔Kwamba wao tu ndio wanaweza?
Narudia tena, maendeleo yanaweza kuletwa na hao hao? Maana kama ni haki hiyo hakuna.Yeyote mwenye kuweza tukimpa ufalme au umalkia sio mbaya.. kwani tunachotaka si haki na maendeleo?🤔
Hebu usitupigie kelele bwanaKwani Familia ya Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete ndio Imejaza nafasi zote za uwaziri,ukuu wa Mkoa,wilaya,ukurugenzi wa halmashauri,Ma Das,Ma Ras,wabunge zaidi ya mia 3, Madiwani ,ma DSO na wengine wengi tu. Nafasi ngapi zipo hapa Nchini? je hiyo Familia ya Kikwete Imejaza nafasi hizo zote?
Kwani Mtela Mwampamba ambaye ni DAS huko Songea ni mtoto wa Kikwete? Juliana Shonza ambaye ni mbunge naye ni mtoto wa Kikwete?
Acheni mawazo ya kijinga na ubaguzi.acheni wivu wa kijinga jinga hapa..Mimi ni CCM na sioni ubaya mtoto wa kiongozi kuwa kiongozi ikiwa ana sifa zote zinazohitajika katika nafasi husika . Kuwa mtoto wa kiongozi hakumzui yeye kuwa kiongozi wala kupambania nafasi fulani ya uongozi.
Ndio Maana unaona George Bush alikuwa ni Rais wa Marekani miaka michache tu baada ya baba yake naye kuwa Rais. Mtoto wa mchungaji hazuiliwi kusomea na kuwa mchungaji ikiwa ana wito huo na kaitwa na Mungu kwa kazi hiyo.
Kikubwa ni lazima ufahamu uongozi ni Karama,ni kipawa ni kibali kutoka kwa Mungu. Siyo kila mtu anaweza kuwa kiongozi au kuongoza watu. Kuongoza watu ni kazi ngumu yenye kuhitaji akili,busara,hekima ,umakini na utulivu wa kiakili. Siyo kazi ambayo kila mmoja anaweza kuifanya.
Ama kweli watu tunatofautianaNarudia tena, maendeleo yanaweza kuletwa na hao hao? Maana kama ni haki hiyo hakuna.
Hujakosea na mizengo pinda naye ana mtoto mbunge na nadhani ni Naibu waziri wa katiba na Sheria kama sijakosea.Mbunge wa namtumbo Vita kawawa ni mtoto wa Mzee Rashid Kawawa?
Hii nayo inafikirisha😁Na ndiyo maana kina Doto Magari wanatamba wanakwambia elimu yako wewe imekusaidia nini wakati kila kukicha ni madeni..huna kitu.
Tuna uwezo huo?Naamini kilichotokea Moza kinaweza kufika hapa siku moja.
Ndiyo, uwezo upo ila muda wetu haujafikaTuna uwezo huo?