Pre GE2025 CCM wanatoa wapi fedha za kununulia msululu huu wote wa Mabasi, kama sio Kodi za Wananchi ni nini?

Pre GE2025 CCM wanatoa wapi fedha za kununulia msululu huu wote wa Mabasi, kama sio Kodi za Wananchi ni nini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu,

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Jokate Mwegelo ame-share video hii ya Mabasi (Yutong Bus) ya CCM katika msafara ukielekea Dodoma kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa unaotarajiwa kufanyika Tarehe 18-19 Januari, 2025.

Soma: CCM kufanya mkutano mkuu Januari 18 na 19 Dodoma, kumpata mrithi wa Kinan

CCM inapaswa kuelekeza fedha kwenye miradi ya maendeleo inayogusa moja kwa moja maisha ya wananchi, kama vile afya, elimu, na miundombinu, badala ya kutumia fedha kwa maslahi ya kisiasa. Hii inaonyesha upotevu wa kipaumbele, ambapo maslahi ya watu wa kawaida yanapuuziliwa mbali, bila kuangalia ustawi wa jamii.
 
Nadhani hawa wamiliki wa mabus huwa wanapokea barua za kuombwa magari kwaajili ya hizo shughuli.

Kwa hii nchi ilivyo ni lazima watoe. Kwanza wamiliki ma bus wengi ni majizi ya ccm tu.

Wanachokifanya tu hapo ni kwenda kuyabandika mabango ya kijani kijani. Shughuli ikiisha yanarudi barabarani kuendelea na biashara.
 
Huenda hiyo ni chenji tu ya ile hongo baada ya mama kuuza mbuga na bandari za watanganyika.
Kumbuka tu, kifuta jasho kutoka uarabuni kilikuwa ni kupewa pikipiki zaidi ya elfu 50 na mabasi ya kisasa yasiyopungua 50 bureee.

CCM Oyeee!
Tanganyika ziiiiiiiii.
 
Nadhani hawa wamiliki wa mabus huwa wanapokea barua za kuombwa magari kwaajili ya hizo shughuli.

Kwa hii nchi ilivyo ni lazima watoe. Kwanza wamiliki ma bus wengi ni majizi ya ccm tu.

Wanachokifanya tu hapo ni kwenda kuyabandika mabango ya kijani kijani. Shughuli ikiisha yanarudi barabarani kuendelea na biashara.
Nani kakudanganya Mzee ingia page za mabus utaona hizo bus zime anza kupoatiwa Toka zikiwa China mpaka Zina shushwa bandarini oder ya kijani ime Toka Moja kwa Moja China
 
Nadhani hawa wamiliki wa mabus huwa wanapokea barua za kuombwa magari kwaajili ya hizo shughuli.

Kwa hii nchi ilivyo
Nani kakudanganya Mzee ingia page za mabus utaona hizo bus zime anza kupoatiwa Toka zikiwa China mpaka Zina shushwa bandarini oder ya kijani ime Toka Moja kwa Moja China
Duh basi nchi ngumu hii
 
Wakuu,

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa chama hicho (UWT), Jokate Mwegelo ame-share video hii ya Mabasi (Yutong Bus) ya CCM katika msafara ukielekea Dodoma kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa unaotarajiwa kufanyika Tarehe 18-19 Januari, 2025.
Kodi yako ewe mtanzania wakuitae MNYONGE.
 
Bongo bwana, yaani huyo jokate kwa influence na umaarufu alionao ilibidi awe katulia na mabiashara yake kama akina rihana huko. Ila kabanwa kwenye kazi ya kujitoa ufahamu na kubaki kusifia kama kasuku.
Huko alipo mdio kwenye buyu la asali sijui unawaza nini wewe..!
 
Back
Top Bottom