Pre GE2025 CCM wanatoa wapi fedha za kununulia msululu huu wote wa Mabasi, kama sio Kodi za Wananchi ni nini?

Pre GE2025 CCM wanatoa wapi fedha za kununulia msululu huu wote wa Mabasi, kama sio Kodi za Wananchi ni nini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakuu,

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa chama hicho (UWT), Jokate Mwegelo ame-share video hii ya Mabasi (Yutong Bus) ya CCM katika msafara ukielekea Dodoma kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa unaotarajiwa kufanyika Tarehe 18-19 Januari, 2025.

Soma: CCM kufanya mkutano mkuu Januari 18 na 19 Dodoma, kumpata mrithi wa Kinan

CCM inapaswa kuelekeza fedha kwenye miradi ya maendeleo inayogusa moja kwa moja maisha ya wananchi, kama vile afya, elimu, na miundombinu, badala ya kutumia fedha kwa maslahi ya kisiasa. Hii inaonyesha upotevu wa kipaumbele, ambapo maslahi ya watu wa kawaida yanapuuziliwa mbali, bila kuangalia ustawi wa jamii.
Ni pesa zetu, hakuna lolote
 
Kumbe Ina pesa za kufanya hayo yote? Ila kujenga vyoo tu huko mshuleni na kupeleka huduma ya maji kwenye vitongoji vya hapa hapa dar haiwezi hadi ipate misaada kutoka Kwa wamarekani??
Jaribu kutenganisha fedha za ruzuku zinazotolewa kwa vyama vyote vya siasa na fedha za serikali.
 
Back
Top Bottom