Elections 2010 CCM wapata wabunge 10 kabla ya uchaguzi mkuu

Elections 2010 CCM wapata wabunge 10 kabla ya uchaguzi mkuu

Hata CCM wangeanza kwa kupata majimbo 100 bado Rais wakati huu atakuwa Slaa tu. Kama Watanzania hawataibiwa kura zao, lazima wengi wao watamchagua Dr Slaa badala ya Kikwete.

Watanzania wana uhakika wa kuendelea na hali hii mbaya waliyonayo kama hawatafanya mabadiliko makubwa ya utawala. Si wajinga. Watafanya hayo mabadiliko.

Wakati kampeni zitakapopanda moto na makundi makubwa yakajitokeza kumsikia Slaa akizungumzia UFISADI, CCM watahaha na kutaka kufanya fujo zao za kawaida. Watazuia viwanja wakidai ni vyao. Hapo huenda kukawa na vurugu za kweli, kwani wakati huu nadhani hata Polisi wa CCM hawataweza kuthubutu kupiga risasi kwenye umati mkubwa. Mauaji ya Pemba yalitosha.

Ukiritimba wa madaraka wa CCM utakwisha wakati huu. Ni vema wakaacha kuwe na amani badala ya kuondoka kwa vurugu.


Hii mbinu ya kujaribu kuidanganya akili yako(sio ya mwezako), yani yako mwenyewe. Ndicho kigezo mhimu kitakachoiweka CCM madarakani kwa milingo kadhaa.
 
Back
Top Bottom