M O N S T E R
JF-Expert Member
- Sep 26, 2022
- 8,825
- 20,941
Mpinzani wako(hasa anayeshindana na upande wenu kwa hila na kwa kuwaua) anaposifia jichunguze unapokosea lakini pale anapokuwa anakusama na kuchukia mbinu na mipango yako basi endelea kukaza hivyohivyo.Katibu wa NEC Organaizesheni ya Chama cha Mapinduzi CCM Paul Matiko Chacha amesema kwa sasa nchini hakuna upinzani wenye nguvu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma akitolea mfano wa upinzani wa Agustino Lyatonga Mrema(aliyewahi kuwa mgombea Urais kupitia NCCR Mageuzi) Freeman Mbowe, Dkt. Wilbroad Slaa na Maalim Seif Shariff Hamad
Soma Pia: Mwanahalisi: Ya Lissu yavuja; agoma kutumika kama kete ya maridhiano
Kauli hiyo ya Chacha ameitoa leo Agosti 1, 2026 alipopokelewa jijini Dar es Salaam mara baada ya kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Julai 29, 2026.
Mbowe waliyemuweka ndani wakidai ni gaidi kichekesho mara tu baada ya kununulika na kusaliti mapambano amekuwa si gaidi tena bali mtu bora kabisa(kwa CCM).