CCM yaachwa solemba

CCM yaachwa solemba

Kumbe habari hii imeripotiwa na Gazeti la Mwananchi la leo kwenye Ukurasa wa 26. Iko hivi: Kabudi: Kinachoweza kutuokoa ni Serikali tatu. Asante sana Mwenyezi Mungu. Wakuumbuka watakuwa wameumbuka. Mimi niliripoti nilichokiona na kukisikia mwenyewe Kisarawe jana
 
utakoma na ujinga wako. msimamo wenu ni serikali nyingi, sisi tunasiamamia kwenye serikali mbili. twendeni kwenye hoja.

usiseme nyingi, tunataka tatu, Tanganiyka yetu, hizo mbili zenu ni ipi na ipi?
 
Kuhusu katiba mpya ccm wameshaachiwa manyoya lakini wanasahau katiba ni ya wananchi kwa sababu ya kulewa madaraka.
 
Usitake kuharalisha hoja yako kwa kujinasibisha kama wewe ni mwanaCCM na unafanya kazi ofisi ndogo ya makao makuu ya CCM, Lumumba.

Kila mara unaleta uwongo na uzandiki hapa JF kutaka kuwaaminisha wanaJF.

Tunakufahamu vizuri sana ila sheria za JF hazituruhusu kuwambia wanaJF uhalisia wako.

Uwongo siyo nguzo imara na uwongo mara nyingi huwa ni siraha ya muda mfupi.

Endelea kuwadanganya wanaJF.

Go hang i-dio.tum
 
CCM ina msimamo wake rasmi juu ya Rasimu ya Katiba mpya.Msimamo huo unahusu hasa kupinga kwa nguvu zote uwepo wa Serikali Tatu. Msimamowa cahama chetu ni kutaka Serikali mbili. Si tatu kama Rasimu inavyopendekeza.

Pamoja na kutoa msimamo kichama,CCM inategemea makada wake walioko kwenye Tume ya Katiba iliyochini ya Jaji Joseph Sinde Warioba ili kuchukua msimamo huo wa chama kama'maoni ya wananchi wengi'. Mambo sasa ni tofauti. Wajumbe karibu wote wa Tume ya Warioba wanaupinga hadharani msimamo wa CCM-wa Serikali mbili na kutetea Serikali tatu.

Ningetarajia wengine wote waunge mkono 'usaliti' kwa chama lakini si Prof. Palamagamba J. A. M. Kabudi. Lakini jana,Prof.Kabudi,akiwa Kisarawe, amesema wazi kuwa Serikali tatu hazikwepeki. Naujua msimamo dhabiti wa Prof.Kabudi katika utetezi wa sera na misimamo ya chama na Serikali yake. Mfano wa hivi karibuni ni kuunga mkono katazo la mgombea huru katika kesi ya Mwanasheria Mkuu dhidi ya Mchungaji Christopher Mtikila iliyokuwa na kuamuliwa na Mahakama ya Rufani Tanzania.

Huu wa jana ni mpya. Naye ameamua kuicha solemba CCM.Ameikatalia. Prof.Kabudi amesema kitu pekee kitakachosaidia kuwapo kwa maridhiano kati yetu kama watanzania ni Serikali tatu tu. Si vinginevyo. Baada ya hapo,Wajumbe karibu wote wa Baraza la Katiba Wilaya ya Kisarawe walikubaliana naye.

Wakabadili msimamo wao.Wakalaumu 'kulishwa kasa' kwa mambo muhimu kama haya;tena na chama tawala.Wajumbe hao wakaendelea kuchangia Rasimu kwa bashasha na utulivu.Wakauweka msimamo wa CCM kando. Wakaupuuza. Prof.Kabudi apaswa kwenda kwinginepo pia kuisambaratisha picha isiyovutia ya msimamo wa CCM.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Mateo Qares aliyekuwa waziri wa CCM na Mkuu wa Mkoa, naye kapigilia msumari hoja ya Prof Kabudi.
Mwananchi wameiripoti vizuri sana
 
Ni wajibu wako kutoa maoni yako ya serikali tatu hata tano ukitaka, naheshimu sana mawazo yako. mimi maoni yangu ni serikali mbili tu, hakuna sababu ya kuwa na miserikali miiingi, huo ni uroho wa madaraka na ni mzigo kwa walipa kodi
Kama una mawazo ya kupunguza idadi ya serikali kwa ninj usije na wazo la serikali moja tu.unafikiri kuwa na nchi mbili zenye serikali mbili...kuna muungano hapo au ni jina tu.
 
JF ni taasisi inayoheshimiwa sana lkn tukiacha maandiko kama haya yatawale humu wote tutaonekana mahayawani!

Hata uhuru wa kuongea una mipaka yake

Hukulazimishwa kuja jf, mseme msemavyo serikali tatu lazima, pumbaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaavu
 
Ni wajibu wako kutoa maoni yako ya serikali tatu hata tano ukitaka, naheshimu sana mawazo yako. mimi maoni yangu ni serikali mbili tu, hakuna sababu ya kuwa na miserikali miiingi, huo ni uroho wa madaraka na ni mzigo kwa walipa kodi
Mawaziri 50 ndio mzigo kwa walipa kodi, lkn sio serikali 3 mawaziri wachache.
 
Ni wajibu wako kutoa maoni yako ya serikali tatu hata tano ukitaka, naheshimu sana mawazo yako. mimi maoni yangu ni serikali mbili tu, hakuna sababu ya kuwa na miserikali miiingi, huo ni uroho wa madaraka na ni mzigo kwa walipa kodi
Yote hayo ni ubatili mtupu suluhisho la mgongano huu ni kuwa na Serikali moja wanaotaka Serikali mbili ni walafi, wanafiki na mafisadi. Huwezi kuogopa Serikali tatu halafu useme unataka Serikali mbili kwa sababu ya kuogopa gharama!
 
Hukulazimishwa kuja jf, mseme msemavyo serikali tatu lazima, pumbaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaavu

lazima? Una akili sawa sawa ww? Kwa taarifa yako, muundo wa muungano wa serikali mbili haubadiliki. Kawaambie na mabwana zako
 
Asante kwa taarifa mkuu , magamba yote yatapukutika hata kwa upepo , Poor Magamba !

Bandugu msihofu vilabu vya mpira vina rais na kuna raisi wa shirikisho na mpira wetu unakuwa katika viwango vya fifa. Acha tuwe na maserekali hata maraisi watano
 
lazima? Una akili sawa sawa ww? Kwa taarifa yako, muundo wa muungano wa serikali mbili haubadiliki. Kawaambie na mabwana zako

Magamba kama hamutaki kubadilika basi wakati utakubadilisheni.
 
Mkuu hii si mada.Hii ni habari

mkuu vuta nkuvute. hamna kitu kinachonichefua kama chama chako kupinga TUNU na UWAZI zisiwekwe kwenye ktb badala yake eti zitungiwe sheria. why,why,why. mzee tupatupa hii ni nchi sio chama. chama kinakufa lkn sio nchi. tell your pals to be serious na waliflect tz ya miaka 100 ijayo. heshima kwako mkuu tena.
 
Msimamo unaoitwa wa ccm ni wa viongozi wa juu (wenye ccmyao); walitaka kuwalisha wanachama wao msimamo wa kupinga serikali tatu.Ninavyojua, wananchi mmoja mmoja walishatoa maoni yao na hayo ndiyo tumeiliyaweka kwenye rasimu; hivyo kamati kuu ya ccm yenye watu labda 50 haikupaswakusema ccm yote inapinga serikali tatu; ni wao tu wanapinga kwa maslahi yao nasi maslahi ya taifa.

Halafu ccm naona wanapotosha ili tusione matatizo katikavifungu vingine, wanataka tubakie kujadili serikali tatu na kusahau ubovumwingine unaohitaji kurekebishwa:
Kwa mfano kuna sababu gani ya msingi ya spika kuwasilishaorodha ya mali zake kwa rais na si kwenye tume ya maadili kama watakavyofanyaviongozi wengine?
Uteuzi wa mhimili wa tatu - -mahakama wote uko mikononimwa rais; je uhuru wake utatoka wapi? Mnaweza kupitia thread ifuatayo https://www.jamiiforums.com/katiba-mpya/464510-rasimu-ina-matatizo-mengi-yarekebishwe-haraka.html
 
Sisemi kitu leo.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
lazima? Una akili sawa sawa ww? Kwa taarifa yako, muundo wa muungano wa serikali mbili haubadiliki. Kawaambie na mabwana zako

Pendelea asubuhi kunywa chai badala ya mnazi.
 
Baadhi ya viongozi wetu ccm ni wabinafsi sana wanazani nchi ni mali yao binafsi
"Vox popoli vox dei"
 
Back
Top Bottom