CCM yafanya maamuzi mazito Kamati Kuu?

Hizo ndio siasa zinavyokwenda.usipozijua utafikiri ni usani.elewa ccm ni chama cha siasa sio NGO
 

Mkuu BAK heshima kwako,
Una uthibitisho ya hayo uliyoyasema?
Ndugu yangu waswahili tunasemaga hivi: "Mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni".
Mie bado ninaamini na ninauhakika kuwa JK ni mtu safi.
 

Mkuu BAK, heshima mbele.
Haya unayoandika na kuzungumza una weza kututhibitishia?
"Mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni"
 
Hizi ni kufuru na kejeli juu ya M/Mungu na Masihi wake..

Nafikiri inabidi mkemewe sasa, naona inakuwa too much..Msilete mifano ambayo inatukwaza tafadhali

Mkuu Mtindio wa Ubongo,
Bado hujakemea tuu hadi sasa?
Kwa majaliwa ya mola, Mh. JK ataendelea kuwa Rais wako hadi 2015
 

FMES, kwa maoni yangu kama haya mabadiliko kweli yamefanyika basi ni mabadiliko madogo sana ambayo hayataleta mabadiliko makubwa ndani ya CCM. Kwa maoni yangu Makamba alipewa nafasi hiyo na Kikwete nadhani miaka karibu mitatu iliyopita baada ya kuchaguliwa kama Rais na pia mwenyekiti wa CCM. Kumuondoa Makamba in less than 3 years inaonyesha Kikwete kutokuwa makini katika kuchagua viongozi wa kumsaidia ndani ya chama na serikali. Kama utakumbuka amekwishafanya mabadiliko ya baraza la mawaziri mara mbili lakini bado serikali yake imegubikwa na kashfa mbali mbali ambazo Watanzania hatujaridhika na jinsi zinavyoshughulikwa.

Labda kumuondoa Makamba kutapunguza kelele kwa muda ndani ya CCM, lakini tatizo kubwa ndani ya CCM kwa sasa ni Kikwete. Mpaka hapo wanachama wa CCM watakapoamua kumwambia ukweli Kikwete kwamba inabidi aanze kufunga virago maana hawana mpango wa kumuweka yeye kama mgombea wa CCM 2010, chama hicho na serikali vitaendelea kugubikwa na kashfa kila kukicha hasa katika masuala ya mafisadi, mikataba ya madini, na gharama kubwa za uendeshaji serikalini.
 
Ladslaus Modest,Mpita Njia,

..hivi uhusiano wa Kinana na wale Waarabu wa Loliondo uko vipi?

..halafu inasemekana Kinana ndiyo kiungo kati ya kampeni za CCM za Uraisi na pesa chafu za mafisadi.

NB:

..tatizo ni Raisi Kikwete. huyu hana tamaa ya kujilimbikizia mali, lakini ana tamaa kubwa sana ya madaraka.

..kosa kubwa kabisa la Kikwete ni ku-corrupt CCM Presidential primaries.

..tangu mwaka 95 alipoutamani Uraisi, basi kampeni za Uraisi wa CCM zimeingiliwa na fitina,majungu,kuchimbana, kununua waandishi na vyombo vya habari, hongo kwa kutumia pesa chafu, na ufisadi wa kila aina.

..hayo mnayoyaona ktk kampeni za UV-CCM ni muendelezo wa mbinu za kampeni za kimtandao. vijana wa CCM wameiga tu toka kwenye "campaign play book" ya Kikwete.

..tunaweza kujiliwaza na kujidanganya kwamba Kikwete ni msafi, lakini hebu jiulize ameingia madarakani akiongozana namafisadi wangapi? mafisadi wangapi wamesaidia kampeni yake kwa fedha?

..itatuchukua miaka mingi sana kuondokana na athari za political and presidential ambitions za Kikwete.
 
Last edited:
GAZETI LA MWANANCHI
Date::11/2/2008
Siasa ndani ya CCM, hatimaye Nape Nnauye amalizwa
Na Saa Mohamed

KAMATI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imechukua maamuzi mazito baada ya kupangua majina ya wagombea wa nafasi za uongozi wa ngazi ya taifa wa jumuiya zake, ukiwemo Umoja wa Vijana (UV-CCM) katika jitihada za kurejesha mshikamano.


Duru za habari za kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam zinasema aliyekuwa mgombea wa nafasi ya mwenyekiti wa UV-CCM, Nape Nnauye, ametupwa nje.


Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu, wagombea uenyekiti wa UV-CCM ambao waligawanya wanachama wa CCM, wameenguliwa na badala yake nafasi hiyo imekwenda kwa Wazanzibari, wakati katika Jumuiya ya Wazazi, wakili maarufu, Nimrod Mkono ameenguliwa.


Majina yaliyopendekezwa yatawasilishwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu kilichopangwa kufanyika Dodoma Novemba 8 na 9 .


Alisema majina yaliyopitishwa kwenye nafasi ya mwenyekiti wa UV-CCM ni Hamad Masauni, Suleiman Hajji na Adila Vuai ambao wote wanatokea zanzibar.


Katika nafasi ya makamu mwenyekiti, waliopitishwa ni Beno Malisa, Hussein Bashe na Zainabu Kawawa wakati Nape Nnauye ameachwa kwa kigezo cha umri ambao imeelezwa kuwa hadi Novemba 26 atakuwa anatimiza umri wa miaka 31.


Kwa mujibu wa kanuni za UV-CCM, mgombea anatakiwa asizidi umri wa miaka 30.


Nape aliingia kwenye malumbano makubwa na vigogo wa CCM wakati alipoingia kwenye kinyang'anyiro cha uenyekiti kwa kuwarushia tuhuma baadhi ya vigogo kwa ufisadi na moto aliouanzisha ulizimwa na mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati.


Nape alisababisha tafrani hiyo baada ya kutuhumu kuwa mkataba wa uwekezaji kwenye jengo la makao makuu ya UV-CCM haukuwa na manufaa kwa umoja huo na kwamba haukupitishwa na vikao halali vya jumuiya hiyo.


Kauli yake, ambayo pia ilishambulia baadhi ya vigogo, akiwemo waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa na mwenyekiti wa umoja huo, Emmanuel Nchimbi, ilisababisha mvutano na baadaye mwanasiasa huyo akavuliwa uanachama katika kikao cha Baraza Kuu la UV-CCM, jambo ambalo lilikuwa kama kutia mafuta kwenye moto.


Kwa mujibu wa habari kutoka kwenye kikao hicho, maamuzi hayo yanaweza kurudisha amani iliyoanza kutoweka miongoni mwa wajumbe wa Halmashauri Kuu, wakiwemo wanasiasa vigogo ambao walishaeleza kuwa wanasubiri suala la Nape liwasilishwe kwenye kikao hicho ili walishughulikie.


"Ni kweli hata mimi nimefurahi kwani hali ya kisiasa ndani ya chama chetu ilikuwa inaelekea kuwa mbaya kwa sababu ya mvutano ndani ya jumuiya zetu," alisema mtoa habari wetu.




Mtafaruku katika jumuiya nyingine ni ule baina ya wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa UWT, Sophia Simba na Janeth Kahama ambao waliripotiwa kugombana kwa maneno wakati wa kikao cha Umoja wa Wanawake cha mkoa jijini Dar es salaam.


Habari zinasema kuwa majina hayo mawili pamoja na la Joyce Masunga yamepitishwa katika kugombea nafasi ya uenyekiti huku Halima Mamuya, ambaye aliwahi kuwa katibu wa jumuiya, akitolewa katika kinya'ganyiro hicho.


Kutokana na uamuzi huo, nafasi ya mwenyekiti inatarajiwa kuwa na upinzani mkali na hivyo kufanya kikao cha Halmashauri Kuu kuwa kwenye wakati mgumu wakati wa kujadili suala hilo.


"Nina wasiwasi wakati wa uchaguzi wa UWT kwa sababu kila mmoja anajiona ni zaidi ya mwenzie," alisema mtoa habari wetu. "Lakini kutakuwa na kinyang'anyiro kikali."


Majina ambayo yamependekezwa na Kamati Kuu ya wagombea uenyekiti wa Wazazi ni Abdallah Bulembo, Athumani Muhina na Ester Nyawaza, wakati Nimrod Mkono akiachwa katika kinya'ganyiro hicho.


Chanzo chetu kilisema pia kuna hatihati ya kujadiliwa kwa agenda ya uchaguzi wa udiwani na ubunge wa Jimbo la Tarime baada ya CCM kuangushwa vibaya na Chadema.

MPAKA TUWE WAKINA TOMASO??
 
Kama ni kweli, Kinana ni Mtu safi atatusaidia sana CCM.


..kinana is a good guy aka "king maker"...lakini not that clean..huko nyuma tulishapata kumjadili kwa kina....ninapata kigugumizi kama mafisadi wakiamua ku hit back...kashfa zake hazitamfanya naye aonekane hafai...na kujeuzwa kama actions zake zinatokana na kisasi chake kwa lowassa....tangu kwenye siasa za kule arusha ambako wote wanatoka....kuna inside story hapo.....
 
Hivi mkono si alikuwemo kwenye list ya mafisadi ya Dr. Slaa, au? Halafu si alisema anaenda mahakamani kumshitaki Dr. Slaa kwa sababu ya ile list hivi alijaishia wapi?

inwezekana yumo kwenye tuhuma, lakini ni mtu mwenye msimamo kwenye mambo abayo, hayaendani na utashi wa mwenyekiti eg kukemea OIC, sasa hao wengine sifikiri watakuwa na uwezo huo etc.
 

Strongly supported, unajua naamini kuwa JF ni family, pale tutakapofikia kuwa tuwe tunaangalia mambo in 3D, huku kila mmoja akichukulia kuwa anachoambiwa ni kwa faida ya wote, bila kumlaumu kwa alichokifanya tutakuwa tunaoperate KAMA JESHI LA WAKOVU KWA WATANZANIA

Mkuu BAK heshima kwako,
Una uthibitisho ya hayo uliyoyasema?
Ndugu yangu waswahili tunasemaga hivi: "Mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni".
Mie bado ninaamini na ninauhakika kuwa JK ni mtu safi.

I doubt, kama unaweza ukasimama katikati ya wagonjwa hospitali za Amana na mwananyamala na ukazungumza the same

I doubt kama unaweza ukasimama mbele ya wamachinga kariakoo na kusema ulichosema

Kama JK safi ila aliingia ikulu kwa fedha za kifisadi, bado vinamfanya kuwa safi.

Ladslaus hata kama umevaa suti nyeupe, nikapita na gari ni kakumwagia maji machafu bado utaitwa msafi?? na utafurahia na hali hiyo hiyo?

waberoya
 


Mwenyekiti ameahidi kuusimamia mwenyewe huu uchaguzi, na imeshafahamika wazi kwamba Bi Kawawa ndiye chaguo lake, !

...umaarufu wa kikwete kama mwenyekiti wa chama utakuwa kikaaongoni iwapo mgombea kama huyu anayemtaka hatapata kura za kuridhisha..it will be like a face snab to him..................

..hakafu huyu zainab kawawa anapewa hii kazi na kikwete ..kama fadhila kwa mzee kawawa kumuunga mkono kikwete kwenye mchakato 2005 ...au ni uwezo.....lazima ajidhihirishe kuwa anao uwezo wa kusimama peke yake...........

.....nadhani kama jf ..hembu tujaribu kufungua faili la zaibab kawawa ..tuangalie kuna nini ndani........detail please!
 

Zainab Kawawa tena katokea wapi? au Zain Kawawa na pengine Zamaradi.
 
"Mkuu FMES pia nadhani ulisema hapo awali kuwa waliamuwa kuwateuwa wagombea kutoka Zanzibar kutokana na mgogoro wa kina Beno Malissa...Sasa Beno ndiyo bado mgombea Umakamu...Je si kutatuwa na tatizo hapo?
Kama sijaelewa naomba unieleweshe mkuu.....Kwasababu Nape na yeye si angewekwa kwenye huo uteuzi wa Umakamu?
Kwasababu nadhani kama kulikuwa na mgogoro kwenye uenyekiti...Umakamu nao inaweza kuwa the same maana kuwapa hao wazenji ni kanyaboya tu...Kazi za Bara watazifanya wenye utaalam na bara...This time makamu.
I stand corrected."


Mkuu J. Mushi

Hii ni Strategic decision ya JK. Nia ni kuhakikisha wagombea kutoka bara watahangaikia umakamu, ambao kwa UVCCM ni ceremonial position. Vita yoote ile ilikua ni kwa ajili ya uenyekiti ambao unampa fursa ya mshindi kuwa mjumbe wa CC na NEC moja kwa moja. Kwa maana nyingine kupata ticket ya kuingia jikoni wakati ajenda nyeti za NEC na Vikao mbalimbali hupikwa. Kwahiyo hata kama Malisa(kijana wa akina EL) akiukwaa umakamu, haitowasaidia sana kupenyeza mambo yao jikoni(atleast kutakua na one supporter less) kwenye CC. It seems JK pamoja na kumfungia Kubenea...lakini anafanyia kazi hoja zake (za kisiasa!).
 
Zainab Kawawa tena katokea wapi? au Zain Kawawa na pengine Zamaradi.

....hapana ninavyojuwa zamaradi kawawa ..alikuwa ripota wa uhuru.baadaye..akapata kazi ya uandishi STAR TV...then majuzi kavutwa ..ofisi ya makamu wa rais....

..kuna HABIBA KAWAWA.alisomea degree ya sheria india baada ya kukosa credits za kuingia mlimani..aliporudi tu akapewa kazi ya u attoney pale city council dsm...hawa wanalingana lingana,,,,huyu ni mwanasheria ...

...zainab?
 
Fashion ya wanahabari na CCM iliingia mf Amina Chifupa (RIP), Shy Rose, Violet Mzindakaya...sijui imeshapitwa na wakati.
 

Kinana si ndiye mwenye ile Artumus yeye na Mrope?
Na wao si wanachimba mafuta uko Mtwara?
Ama nimekosea?
 

Zainab Kawawa yeye alikuwa pale Kibosho Girls mimi nikiwa pale Umbwe...Alikuwa ni mtu mzuri tu sijui sana kuhusu maisha yake baada ya high school na huko kwenye siasa....Ila alikuwa sociable na mwelewa.
 

Mkuu haya yako ni moja ya mawazo elfu nyingi sana kufuyatia huu mkutano wa CC, na haina maana kwamba ndio ukweli wa kilichotokea, binafsi ninakitizama kikao hiki na maamuzi yake kama Tanzania, nchi ya third world na sio kama USA na Europe, na kwamba kinachofanyika huko ndani ya CCM under current powers ndio tulichonacho na bado wako kwenye power for the next two years, mpaka uchaguzi utakapofanyika tena, sasa in the meantime siwezi kutegemea anything out of hawa viongozi tulionao sasa, na ndio maana nimefurahi kuona something ambacho sikukitegemea kama hichi.


Aliyesema mafisadi wamepigwa chini ni mimi, sio CCM wala serikali na nimesema hivyo kutokana na kazi nzito niliyoshirki kuifanya katika kupigana na mafisadi ili wasipewe tena nafasi ya kugombea uenyekiti wa UV-CCM. Leo mafisadi wamenyimwa nafasi hiyo sasa sielewi ungetegemea niseme nini hasa kwa mawazo yako ambayo siku zote ndio yenye ukweli na ufasaha zaidi, maana sisi wengine siku zote hua hatuna uwezo kuona ukweli zaidi yako?

Naomba kurudia point yangu kwamba ninaamini kwa 100%, kwamba kwakunyimwa kugombea uenyekiti wa UV-CCM, mafisadi waliotumia millions of shillings kumtoa Nape, wamepigwa chini. Ndivyo ninavyoamini.



Hayo sisi hayatuhusu tunaopiga vita ufisadi, tunapigana na silaha tulizonazo na katika mazingara yanayoieleweka yakoje kisiasa na kisheria, EPA ni EPA na UV-CCM havina anything to with each other, mafisadi wamenyimwa kugombea uenyekiti wa UV-CCM nafasi ambyo wameitumia kwa muda mrefu sana kupata uongozi wa juu, this is the end of Nchimbi huko UV-CCM sasa say what you want ni haki yako, lakini kwa wale tuliopigania haya this is good kwetu na sasa tutaendelea kujipanga, pole pole na the rest of the ishus, kibaya kuliko yote ni kama mafisadi wangeachiwa free kufanya wanayotaka, hapa wamekumbushwa kuwa sasa wawe macho maana hata wale waliokuwa wakiwalinda pia wameanza kuchoka, katika siasa makubwa huanza na madogo kama haya, lakini bado ni haki yako kuamini unavyotaka, lakini na sisi tutaendelea kuamini tunachokiona kwamba mafisadi hapa wamepigwa chini puuu!.


Hao wote uliowataja hakuna mjumbe wa CC, kwa hiyo hoja ni mufilisi, nguvu ya mafisadi haiwezi kuwepo kwenye umoja wa kina Mwakyembe ambaye sasa hata watoto wake wanatishiwa maisha yao na mafisadi, sasa inakuwaje mtu yumo kundi lao halafu wanamtishia watoto wake? Mkuu unaongela siasa za bongo au USA na Europe?


Sidhani kama kuna aliyekulazimsha kuiona hii ishu tofauti na unavyotaka, sina sababu ya kua muangalifu of anything kwa sababu ninapigana na mafisadi na hizi ndio results, kwamba wamepigwa bao hawata gombea hiyo nafasi ya uenyekiti wa UV-CCM, sasa niwe muangalifu wa nini tena? Eti kwa sababu wewe hukubaliani na mawazo yangu basi niwe muangalifu maana unachoona wewe tu ndio sawa, mimi sina uwezo wa kuona wala kufikiri ya ninayoyaona, duh mkuu una akili sana na I wonder in the last 45 ya uhuru wetu umelifanyia mangapi taifa letu maana it seems ni wewe tu mwenye akili na macho sisi wananchi wa Tanzania wengine wote hatuna kabisaa!

Hivi ni lini huko nyuma mwenyekiti wa CCM au wa chama chochote cha siasa nchini aliwahi kuwakataa wagombea wote wa chama na ikakubalika? Eti ninatumiwa na wajanja na wewe unatumwia na nani? Yaani nimempigania Nape wee hapa na kutukanwa matusi kushoto na kulia kuhusiana na huu uchaguzi wa UV-CCM, leo wale wote walikuwa hawamtaki Nape wamepigwa chini, unasema kuona kuna ushindi on my part ni kutumwa na wajanja? Duh! mkuu unaonekana unajua ninapokuwa ninafikiri bila kutumwa na ninapokiri kwa kutumwa ni wapi tena niliwahi kufikiri kwa kutumwa na wajanja mkuu? na ni wapi sikuwa kuifikiri kwa kutumwa na hao wajanja wako bro?

In the future weka hoja zako bila kunihusisha na mimi maana wananchi hapa sasa wanaanza kuchoka sana na hizi acts zako mkuu, I understand kwamba sasa una "new strong supporters" lakini naomba uheshimu sana haki yangu ya kuwepo hapa na kusema maoni yangu kama wengine, maana mimi ninaheshimu ya kwako, kama una shida na hoja yangu ikate hoja sio kunizushia maneno ya mimi kutumiwa na wajanja kwa sababu tu hukuabliani na hoja zangu, sio ustaarabu hata kidogo bro! maana sio lazima niwe na uhusiano wowote nje ya fourm na anybody ila kuweka mawazo yangu hapa, mimi mtu huru na mawazo yangu ni huru sina ubia na yoyote hapa, heshima ni tabia yangu lakini sio uoga, na heshima yangu isichukuliwe kama ninamuogopa mtu hapa, tunaheshimiana tu!
i
Kwa hiyo naomba kuendelea kusherehekea ushindi huu mkuu, maana leo nimenunua cigars kibao ninagawa tu toka jana, na leo ninajitayarisha kupiga mvinyo saafi ingawa huwa sinywi, lakini kwa leo tu nitajitahidi angalu nipitishe fundo moja tu koooni!

ES wazee wa sauti ya umeme!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…