Briefly More dataz kutoka CC, Dar:-
1. Kikao cha CC kilianza leo na kitaisha kesho, kesho kitaanza saa tano mchana na kuisha jioni.
2. Kikao kwa kauli moja kimeamua kuwafuta wagombea wote wa uchaguzi wa uenyekiti wa UV-CCM kutoka bara, na kama alivyoomba rais kuwaachia nafasi hiyo wagombea watatu wa kutoka Visiwani.
3. Mwenyekiti wa kikao rais wa jamhuri, mapema aliomba kupitihswa kwa hoja, aksiema wka uchungu mkubwa sana kwamba kampeni za uchaguzi huo zilikwua zimeharibiwa sana na rushwa na hisia nzito zilizomhusisha hata mtoto wake, akaomba kuepusha mgawanyiko zaidi kwa kuwafuta wagombea wote wa kutoka bara, CC wameipitisha tayari.
4. Kamati kuu imeamua kupiga marufuku mtindo wa kutoa alama kwa viongozi wa Jumuiya zake, kwa mantiki hiyo kikao hicho kimeamua kuibatili alama ya E aliyopewa mmoja wa wagombea wa uenyekiti wa UV-CCM ndugu Nape, na pia kimeondoa alama ya E aliyopewa mgombea mmoja wa nafasi ya mwenyekiti wa UWT Bi Mamuya, na kuwapa alama ya A.
- Lakini CC imeamua kwamba hataruhusiwa kugombea nafasi hiyo, yaani Bi Mamuya, kuhusu Nape, CC imeamua kuukataaa kabisa uamuzi wa UV-CCM uliotolewa dhidi ya Nape, na kwamba rufaa yake itasikilizwa tena huko NEC, tarehe 8 na 9.
5. Kikao hicho pia kimepitisha majina matatu ya wagombea wa uenyekiti wa UWT, yaani Mama Janet Kahama, Mama Sophia Simba, na Mama Masunga, pia kimeyakubali majina ya wagombea uenyekiti wa wazazi, ambako mbunge Mkono anatazamiwa kunyakua nagfasi hiyo bila ushindani mkubwa.
6. Baadhi ya Wabunge wamependekeza, kuondolewa mara moja wka katibu mkuu wa sasa wa CCM, ili kukinusuru chama na bunge na wakataka Pinda na Spika, wapewe nafasi ya kuandaa kikao cha dharura na kuto mapendekezo ya kuinusuru CCM huko bungeni.
7. Mafisadi ambao wameonekana wakitoka kwa hasira sana ndani ya kikao hicho, sasa hivi ninapoandika wanakutana kwa siri "sehemu" kuandaa mkakati wa kupambana na hii situation ambyo hawakuitegemea na agenda kubwa huko ni namna ya kumshika mgombea mmoja wa huko Zanzibar.
- Lakini pia kuna habari za rais kukutana na baadhi ya wajumbe muhimu wa CC, majuzi "somewhere" ambako aliwataka kufikiria namna ya kukabiliana na hii ishu ya ugombea na uongozi wa UV-CCM kwa ujumla, ambapo aliwashauri kuwa wawatoe viongozi wote wa sasa na kuchaguz wapya with mandate ya mabadiliko, ambapo pia anamtaka kiongozi mmoja mashuhuri sana kutoka bara (jina ninalihifadhi kwa sasa) kushika nafasi ya katibu mkuu.
Samahani wakuu kwa uchelewesho, mawasiliano yalikua magumu mno, lakini in the meantime bado tunaendelea kukusanya more dataz na tutaendelea kuhabarishana as soon as tukizipata.
Masahihisho kidogo ni kwamba kikao kipo Dar na sio Dodoma, Mods wanaweza kutusaidia kurekebisha hapo juu.