CCM yafanya maamuzi mazito Kamati Kuu?

CCM yafanya maamuzi mazito Kamati Kuu?

Nafikiri zaidi ya asilimia 95 kuanzia viongozi wa vijiji mpaka kwa JK ni mafisadi. Wanachotofautiana ni kiwango cha kuiba.

Mkuu Mtanzania,

Kama haya maneno yako ndio ukweli basi wananchi wa Tanzania ndio tumeoza kabisa na ufisadi.
 
Wakati wa mwalimu nitasema labda policies ndio zilikuwa mbovu pamoja na capacity ndogo ya watendaji. Lakini kilichopo sasa ni culture ya ufisadi ambao imeenea kwenye jamii zetu zote na huko CCM imekomaa.

Kama yalivyo mabadiliko kwenye culture yoyote, zinaweza kutumika nguvu kwa kuwanasa wale vinara wachache na kutoa onyo kali au through kuelemisha jamii mpaka waone umuhimu.

Njia iliyorahisi na haraka ni kutumia bakora.

Hata hao wanaosema wanapinga ufisadi, ukiwafuatilia kidogo tu unakutana na harufu kali ya ufisadi.

Hapa mkuu ndio unaharibu kabisa unapojaribu kumuhusisha Mwalimu, kwa sababu Mwinyi, na Mkapa, ambao ndio chimbuko la ufisadi nchini wote walikuwa wananfunzi wa Mwalimu, na ni a matter of fact kwamba mafisadi wengi tulionao leo ni wananfunzi wa Mwalimu, I mean Kingunge ni mwanafunzi wa karibu sana na Mwalimu.

Mwalimu alishindwa kuwachapa bakora mafisadi ndio maana mpaka leo tunasua sua, atakayewanasa wengine ni nani hasa wakati tumerithi the culture ya huyu ni mwenzetu huyu kutoka Mwalimu?

Inapokuja kwenye suala la ufisadi, taifa zima tunahusika, sasa tushirikiane kulisafisha taifa letu, kwa sababu hawezekani ukasema mbele ya watu wenye akili nyingi za siasa kwamba taifa letu lina viongozi 95% mafisadi, swali la kwanza utaulizwa vipi hao wananchi waliowachagua? Utaulizwa hao wananchi mshahara wao kwa mwezi ni hela ngapi? Sasa wanawezaje kwenda kwenye mastarehe na kujenga majumba makubwa kule Mbezi na Kunduchi kama sio mafisadi?

Kama viongozi wetu 95% ni mafisadi, basi wananchi ndio tumeoza kabisa na ufisadi, na ufisadi ni ufisadi tu it has nothing to do na wakati wa Mwalimu maana wengi wa mafisadi leo walikuwa ni wananfunzi wake, Mwalimu alijua kuwa Lowassa ni fisadi then mbona hakutaka mkono wa sheria ufuate mkondo wake, una maana Mwalimu naye alikua fisadi?
 
Corruption is so pervasive is our society that you can longer say some, few or many are fisadis. Its like corrupt behavior is in our vains! Mark i use OUR due to PERVASIVE nature of corruption in Tanzania.

We have to address that............. Nawapa mfano.

Juzi nikiwa ofisini kwangu Dodoma, alikuja Mzee mmoja amedhulumiwa magari yake 63 na TRA. Kesi yake ipo wazi kabisa kwamba kaonewa na TRA miaka 10 iliyopita. Kila kiongozi anaefuatwa na Mzee huyu anaomba akatiwe kitakachopatikana. Ni mzee wa kimbulu.

Akaja kwa Dr. Slaa, suala lake likaanza kushughulikiwa na Waziri Mkuu Pinda yeye hakutaka chochote bali alifanya ufuatiliaji mzuri sana na kuagiza mzee apatiwe haki zake.

Katika barua ambayo msaidizi wa Waziri Mkuu alimwandikia Mzee huyu akawa amekosea (sijui kama ni kwa makusudi) na kuagiza TRA wasajili upya magari ya mzee huyu na kupewa magari yake. Magari haya yamekaa yadi miaka 10 bila kutembea kufuatia maamuzi mabaya ya TRA, hivyo yameoza na hakuna magari tena. Uamuzi sahihi ni mzee huyu kupewa magari mapya na kulipwa fidia ya kutofanya kazi miaka 10.

Mzee akanikuta ofisini, akanieleza tatizo lake na nikaanza kulifanyia kazi mara moja maana tayari Dr. Slaa alikuwa amekwisha nieleza tatizo hili. Nikiwa ninachukua kalamu ili kudraft barua kwenda kwa Waziri Mkuu (ilii ichapwe na sekretari wa Dr. Slaa), mzee akainama na kuniambia,

' Mheshimiwa Zitto (ninamquote hapa maana sipendi kuitwa mheshimiwa) kama ukifanikiwa kunisaidia suala hili, nitakujengea nyumba nzuri Kigoma'

Kalamu ilianguka kwa kutetemeka kwa hasira......... Mratibu wa Ofisi yetu alikuwa ananiangalia na akitarajia (he knows me so well) kuachana na Mzee huyu....... Nilimtazama Mzee huyu na kumwambia 'Baba, hii ni haki yako huna haja kuinunua. Mimi pia hii ni kazi yangu, ninalipwa kuifanya. Sitaki nyumba yako. Sitaki chochote kutoka kwako.'

Mzee hakuelewa, akashangaa. Akasema, wenzako wameniomba nyingi, wewe ninakumba nyumba unakataa. Mimi siwaelewi wewe na Slaa. Mtakufa masikini.

Sikumjibu kitu, nikamaliza kazi yake na kuipeleka kwa Pinda.

Hii inadhihirisha kuwa upande wa wananchi pia ni tatizo. Wao ni chanzo cha Ufisadi.

Kuna haja ya kufanya 'overhaul' ya jamii nzima kuhusiana na suala hili. Wakati mwingine Tanzania suala la Rushwa huwa ni nani kapata. Mafisadi wanaonena wivu, asiepata anamsema aliepata. Yeye akipata kesho, anasemwa na aliepata jana. Tumefika hapo.
 
Prof. Chachage aliwahi kusema, ' Jamii inapata viongozi wa aina ya jamii husika, kama viongozi ni wala rushwa, basi jamii ni ya wala na watoa rushwa pia'

By the way leo ni Birthday ya CHACHAGE mdogo, mtoto wangu.
 
Naam mheshimiwa Zitto huo ndiyo ukweli wa mambo. Ndani ya CCM na serikali kumejaa mafisadi walioweka mbele maslahi yao badala ya yale ya Watanzania na ni makosa makubwa kutaka kuonyesha kwamba mafisadi ndani ya chama na serikali ni 'wachache' tu. Happy Birthday to Chachage mdogo, may he live to blow 101 candles.
 
Kama walivyoongea wachangiaji wengi hapo juu ni kweli kuwa jamii yetu ya watanzania ndio tatizo la ufisadi linakoanzia. Mifano ni mngi lakini nikizungumzia michache kama ifuatavyo hapa chini.

Wengi wetu tunajua jinsi mtu ukijaribu kufanya kazi zako na kutumikia wananchi kwa uadilifu na haswa ukiwa kwenye kitengo/idara/shirika n.k panapojulikana kuwa kuna njia za urahisi kupata hela(rushwa, 10% etc ). Kama utafuata sheria na kupinga kujiingiza kwenye mauzauza yao utaitwa majina yote LOFA, MSHAMBA, BWEGE, WAKUJA n.k. na kiasi kikubwa cha watu wanaokufahamu kama ndugu, marafiki, wafanyakazi wenzio n.k.

Ukija kwenye ndoa na familia setu za siku hizi tena na watu wengi walivyo kuwa 'materialistic' utapata presha kubwa kutoka kwa familia na mara nyingine hata mkeo kuwa - 'hacha kulemaa unaona majirani zetu wanajenga, wananunua mashamba etc sisi tunashangaa tu na umri unakwenda'.

Reflection ya hii mifano ni kuwa kwa kiasi kikubwa jamii yetu imeharibika na ndio hiyo inayotoa viongozi kutuongoza, sasa cha zaidi tutegemee nini kutoka kwa hao viongozi zaidi ya kutafuta njia zozote nyingi zikiwa si halali kujitajirisha. Kwa hiyo tuyaonayo kwa viongozi wetu ni reflection ya jamii yetu kwa ujumla ilivyo. Jamii ambayo mkwepa kodi, mdokozi wa mali ya umma na 'siku hizi (ugonjwa mpya) mdhulumu wa foreign parterners in business' anaonekana mjanja na shujaa mbele yetu na wengi wakitaka kujifunza kutoka kwake ili wafanikiwe kirahisi rahisi.

Kama tusipobadilika tutafikia hali mbaya zaidi muda si mrefu na kuanza kutafunana wenyewe kwa wenyewe ikiwa ni reflection ya 'the highest morals decay the society has ever reached'.
 
Quote: Zitto

Prof. Chachage aliwahi kusema, ' Jamii inapata viongozi wa aina ya jamii husika, kama viongozi ni wala rushwa, basi jamii ni ya wala na watoa rushwa pia'

Naam mheshimiwa Zitto huo ndiyo ukweli wa mambo. Ndani ya CCM na serikali kumejaa mafisadi walioweka mbele maslahi yao badala ya yale ya Watanzania na ni makosa makubwa kutaka kuonyesha kwamba mafisadi ndani ya chama na serikali ni 'wachache' tu.

Mkuu Zitto,

Hapo juu tupo ukurasa mmoja, wananchi wote tuna damu ya ufisadi.
 
Hapa mkuu ndio unaharibu kabisa unapojaribu kumuhusisha Mwalimu, kwa sababu Mwinyi, na Mkapa, ambao ndio chimbuko la ufisadi nchini wote walikuwa wananfunzi wa Mwalimu, na ni a matter of fact kwamba mafisadi wengi tulionao leo ni wananfunzi wa Mwalimu, I mean Kingunge ni mwanafunzi wa karibu sana na Mwalimu.

Mwalimu alishindwa kuwachapa bakora mafisadi ndio maana mpaka leo tunasua sua, atakayewanasa wengine ni nani hasa wakati tumerithi the culture ya huyu ni mwenzetu huyu kutoka Mwalimu?

Inapokuja kwenye suala la ufisadi, taifa zima tunahusika, sasa tushirikiane kulisafisha taifa letu, kwa sababu hawezekani ukasema mbele ya watu wenye akili nyingi za siasa kwamba taifa letu lina viongozi 95% mafisadi, swali la kwanza utaulizwa vipi hao wananchi waliowachagua? Utaulizwa hao wananchi mshahara wao kwa mwezi ni hela ngapi? Sasa wanawezaje kwenda kwenye mastarehe na kujenga majumba makubwa kule Mbezi na Kunduchi kama sio mafisadi?

Kama viongozi wetu 95% ni mafisadi, basi wananchi ndio tumeoza kabisa na ufisadi, na ufisadi ni ufisadi tu it has nothing to do na wakati wa Mwalimu maana wengi wa mafisadi leo walikuwa ni wananfunzi wake, Mwalimu alijua kuwa Lowassa ni fisadi then mbona hakutaka mkono wa sheria ufuate mkondo wake, una maana Mwalimu naye alikua fisadi?

Nyerere aliwahi kusema kwa kutoa mfano kuwa,nukuu isiyo rasmi "Ukila chakula kizuuri SANA basi matokeo yake ni mavi yanayonuka".Kwa hili Nyerere tusimlaumu.Haya ni matokeo ya chakula ambapo tumepeta Mavi.Sidhani kma mwl aliwafundisha hawa mabwana ufisadi.
 
Corruption is so pervasive is our society that you can longer say some, few or many are fisadis. Its like corrupt behavior is in our vains! Mark i use OUR due to PERVASIVE nature of corruption in Tanzania.

We have to address that............. Nawapa mfano.

Juzi nikiwa ofisini kwangu Dodoma, alikuja Mzee mmoja amedhulumiwa magari yake 63 na TRA. Kesi yake ipo wazi kabisa kwamba kaonewa na TRA miaka 10 iliyopita. Kila kiongozi anaefuatwa na Mzee huyu anaomba akatiwe kitakachopatikana. Ni mzee wa kimbulu.

Akaja kwa Dr. Slaa, suala lake likaanza kushughulikiwa na Waziri Mkuu Pinda yeye hakutaka chochote bali alifanya ufuatiliaji mzuri sana na kuagiza mzee apatiwe haki zake.

Katika barua ambayo msaidizi wa Waziri Mkuu alimwandikia Mzee huyu akawa amekosea (sijui kama ni kwa makusudi) na kuagiza TRA wasajili upya magari ya mzee huyu na kupewa magari yake. Magari haya yamekaa yadi miaka 10 bila kutembea kufuatia maamuzi mabaya ya TRA, hivyo yameoza na hakuna magari tena. Uamuzi sahihi ni mzee huyu kupewa magari mapya na kulipwa fidia ya kutofanya kazi miaka 10.

Mzee akanikuta ofisini, akanieleza tatizo lake na nikaanza kulifanyia kazi mara moja maana tayari Dr. Slaa alikuwa amekwisha nieleza tatizo hili. Nikiwa ninachukua kalamu ili kudraft barua kwenda kwa Waziri Mkuu (ilii ichapwe na sekretari wa Dr. Slaa), mzee akainama na kuniambia,

' Mheshimiwa Zitto (ninamquote hapa maana sipendi kuitwa mheshimiwa) kama ukifanikiwa kunisaidia suala hili, nitakujengea nyumba nzuri Kigoma'

Kalamu ilianguka kwa kutetemeka kwa hasira......... Mratibu wa Ofisi yetu alikuwa ananiangalia na akitarajia (he knows me so well) kuachana na Mzee huyu....... Nilimtazama Mzee huyu na kumwambia 'Baba, hii ni haki yako huna haja kuinunua. Mimi pia hii ni kazi yangu, ninalipwa kuifanya. Sitaki nyumba yako. Sitaki chochote kutoka kwako.'

Mzee hakuelewa, akashangaa. Akasema, wenzako wameniomba nyingi, wewe ninakumba nyumba unakataa. Mimi siwaelewi wewe na Slaa. Mtakufa masikini.

Sikumjibu kitu, nikamaliza kazi yake na kuipeleka kwa Pinda.

Hii inadhihirisha kuwa upande wa wananchi pia ni tatizo. Wao ni chanzo cha Ufisadi.

Kuna haja ya kufanya 'overhaul' ya jamii nzima kuhusiana na suala hili. Wakati mwingine Tanzania suala la Rushwa huwa ni nani kapata. Mafisadi wanaonena wivu, asiepata anamsema aliepata. Yeye akipata kesho, anasemwa na aliepata jana. Tumefika hapo.

Huyu si mzee Tango kweli huyu?
Anyways...Kwa kweli ni story ya nguvu sana kwani ni mfano halisi kabisa wa tabia yetu sisi watanzania, na kuna wengine kweli wanaweza kukuona kama huna akili nzuri kwa kukataa nyumba...Hapo utaona kuwa rushwa imekuwa kama utamaduni wetu watanzania na waafrika kwa ujumla.....Wanasema mkono mtupu haulambwi.

Hata hivyo ndugu Zitto ikitokea situation kama hiyo next time basi unamwambia mtu huyo kama ni kweli ana furaha basi akejenge shule ama zahanati ama chochote cha kuwasaidia wananchi..Either Kigoma,Mbulu ama popote pale pengine atakapokuwa ametokea mtu huyo.

Mzee huyo naye ajifunze kutokana na kukasirika kwako kwasababu aelewe kuwa hata matatizo ya magari yake kukwama TRA kwa miaka kumi ni kwasababu ya Rushwa....Sasa hapo alitakiwa aone hilo....Na sisi pia tunatakiwa tujifunze ili tufanikishe vita hii kwani ni vita ngumu.
 
Mkuu Mushi,

Heshima mbele sana, mimi ni mwananchi mwenye uchungu na taifa langu ya vyama sio muhimu sana kwangu, ninaamini kama raia wa Tanzania ni haki yangu kulilia mabadiliko, ikiwa ni nia njema kwa taifa langu, yes mimi ni mwanachama hai na mkereketwa wa CCM, siwezi kuwazuia wale wote walioamua kufikiri tofauti,

Ninaamini CCM ina viongozi wachache wabovu, wanaohitaji kuondolewa sio kupewa nafasi zingine tena baada ya kuthibitishwa kwua ni wabovu, niaamini katiba yetu ina mapungufu sana inahitaji kurekebishwa kwa sababu ni ya chama kimoja haikuundwa kwa ajili ya siasa za vyama vingi,

Ninasema Tanzania ni taifa langu kama lilivyo lako, ninao uhuru wa kutoa mawazo yangu kama ilivyo kwa wengine wote, kazi ya kusafisha uovu ndani ya uongozi wa taifa letu sio ya mchezo, lakini pole pole inaonekana tunakaribia kufika wkenye ukweli wa ishu.

Ahsante Ndugu yangu

Nakubalia kwa kiasi kikubwa mkuu FMES kwasababu hata hapo wapinzani walipofikia imechangiwa sana na baadhi ya wana ccm wenyewe kuchoshwa na mwelekeo wa chama na ufisadi uliokigubika chama chenu na jamii kwa ujumla.

Kama ccm isipobadilika basi na wananchi itawachukuwa muda kubadilika.

Tukichukulia mfano wa Ndugu Zitto ambapo kukataa kwake rushwa kulimfanya aonekane mtu wa ajabu...Ndipo utashangazwa kuona kuwa rushwa bado inaweza kuwawezesha wana ccm waendelee kupeta kama wananchi wasipobadilika.

Nadhani pia hata baadhi ya siri za ufisadi zimevujishwa na wana ccm...Na hivyo basi tuendelee kuomba Mungu ili Taifa letu lirudi kwenye hali ya kawaida na mapinduzi yafanyike ili kulikomboa Taifa letu kwa manufaa yetu na vizazi vijavyo.
 
Corruption is so pervasive is our society that you can longer say some, few or many are fisadis. Its like corrupt behavior is in our vains! Mark i use OUR due to PERVASIVE nature of corruption in Tanzania.

We have to address that............. Nawapa mfano.

Juzi nikiwa ofisini kwangu Dodoma, alikuja Mzee mmoja amedhulumiwa magari yake 63 na TRA. Kesi yake ipo wazi kabisa kwamba kaonewa na TRA miaka 10 iliyopita. Kila kiongozi anaefuatwa na Mzee huyu anaomba akatiwe kitakachopatikana. Ni mzee wa kimbulu.

Akaja kwa Dr. Slaa, suala lake likaanza kushughulikiwa na Waziri Mkuu Pinda yeye hakutaka chochote bali alifanya ufuatiliaji mzuri sana na kuagiza mzee apatiwe haki zake.

Katika barua ambayo msaidizi wa Waziri Mkuu alimwandikia Mzee huyu akawa amekosea (sijui kama ni kwa makusudi) na kuagiza TRA wasajili upya magari ya mzee huyu na kupewa magari yake. Magari haya yamekaa yadi miaka 10 bila kutembea kufuatia maamuzi mabaya ya TRA, hivyo yameoza na hakuna magari tena. Uamuzi sahihi ni mzee huyu kupewa magari mapya na kulipwa fidia ya kutofanya kazi miaka 10.

Mzee akanikuta ofisini, akanieleza tatizo lake na nikaanza kulifanyia kazi mara moja maana tayari Dr. Slaa alikuwa amekwisha nieleza tatizo hili. Nikiwa ninachukua kalamu ili kudraft barua kwenda kwa Waziri Mkuu (ilii ichapwe na sekretari wa Dr. Slaa), mzee akainama na kuniambia,

' Mheshimiwa Zitto (ninamquote hapa maana sipendi kuitwa mheshimiwa) kama ukifanikiwa kunisaidia suala hili, nitakujengea nyumba nzuri Kigoma'

Kalamu ilianguka kwa kutetemeka kwa hasira......... Mratibu wa Ofisi yetu alikuwa ananiangalia na akitarajia (he knows me so well) kuachana na Mzee huyu....... Nilimtazama Mzee huyu na kumwambia 'Baba, hii ni haki yako huna haja kuinunua. Mimi pia hii ni kazi yangu, ninalipwa kuifanya. Sitaki nyumba yako. Sitaki chochote kutoka kwako.'

Mzee hakuelewa, akashangaa. Akasema, wenzako wameniomba nyingi, wewe ninakumba nyumba unakataa. Mimi siwaelewi wewe na Slaa. Mtakufa masikini.

Sikumjibu kitu, nikamaliza kazi yake na kuipeleka kwa Pinda.

Hii inadhihirisha kuwa upande wa wananchi pia ni tatizo. Wao ni chanzo cha Ufisadi.

Kuna haja ya kufanya 'overhaul' ya jamii nzima kuhusiana na suala hili. Wakati mwingine Tanzania suala la Rushwa huwa ni nani kapata. Mafisadi wanaonena wivu, asiepata anamsema aliepata. Yeye akipata kesho, anasemwa na aliepata jana. Tumefika hapo.

Nafikiri Zitto tukianzia hapa tutafika. Nilishawahi kuzungumzia hili katika post zangu za huko nyuma.

Hii nchi inakopelekwa na CCM siko kabisa, sina imani kabisa na hiki chama hata chembe. Kama katibu wao mkuu anasema huyu ni MWENZETU unategemea nini? Watu wamesha kata tamaa wanasindikiza tu siku. Mtu anafikiria ugali na maharage ya kesho tu ndo anafikiria mbali.

CCM has no plan with this country zaidi ya wao, familia zao, na jamaa zao kuchumia tumboni. Kama kweli wanaplan na hii nchi wasingekuwa wanatuhimiza tuachangine shule za kata na wao watoto wao wanapelekwa ulaya.

Zitto hivi nyie wabunge mnalipa kodi ya allowances mnazopewa? je, kama hamlipi, unaretire against receipt?

please ans then i have more mana naona hapa ndo chanzo cha ufisadi....
 
Zitto hivi nyie wabunge mnalipa kodi ya allowances mnazopewa? je, kama hamlipi, unaretire against receipt?

please ans then i have more mana naona hapa ndo chanzo cha ufisadi....

1. Hatulipi kodi ya allowances. Tunalipa kodi ya mapato kwa mshahara. Tanzania hakuna anaelipa kodi ya allowances hata mmoja. Hii ni moja ya hoja ambayo Kambi ya upinzani Bungeni inasema kila mwaka. TRA walisikia hoja yetu na kuleta Bili kwa Katibu wa Bunge ya kodi kwa miaka 10 iliyopita ambazo wabunge wamekuwa hawalipi maana Income Tax Act inasema posho ni mapto na hivyo lazima zikatwe kodi (sitting allowances na sio per diems, maana per diems are simply transfers). Unajua tulichofanya? Tulikasirika ni kwa nini TRA inaleta Bili Bungeni na kuamua kutunga sheria kwamba income tax act 2004 isitumike kwetu.

Hali ni hiyo hiyo kwa Majaji, nao katika sheria ya majaji hawalipi kodi katika posho wanazopata.

Mimi ninaamini tunapaswa kulipa kodi katika allowances za vikao maana ni kipato kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato. Nimesema hivi wakati wa mjadala wa sheria ya Majaji mwaka jana. Nilisema hivyo (hata kama wenzangu walichukia) ndani ya Bunge mwaka huu wakati wa mjadala wa Sheria ya Bunge (National Assembly Bill, 2008).

Ninaamni kuwa kulipa kodi ni uzalendo - ishara ya uzalendo.

Swali lingine?
 
Corruption is so pervasive is our society that you can longer say some, few or many are fisadis. Its like corrupt behavior is in our vains! Mark i use OUR due to PERVASIVE nature of corruption in Tanzania.

We have to address that............. Nawapa mfano.

Juzi nikiwa ofisini kwangu Dodoma, alikuja Mzee mmoja amedhulumiwa magari yake 63 na TRA. Kesi yake ipo wazi kabisa kwamba kaonewa na TRA miaka 10 iliyopita. Kila kiongozi anaefuatwa na Mzee huyu anaomba akatiwe kitakachopatikana. Ni mzee wa kimbulu.

Akaja kwa Dr. Slaa, suala lake likaanza kushughulikiwa na Waziri Mkuu Pinda yeye hakutaka chochote bali alifanya ufuatiliaji mzuri sana na kuagiza mzee apatiwe haki zake.

Katika barua ambayo msaidizi wa Waziri Mkuu alimwandikia Mzee huyu akawa amekosea (sijui kama ni kwa makusudi) na kuagiza TRA wasajili upya magari ya mzee huyu na kupewa magari yake. Magari haya yamekaa yadi miaka 10 bila kutembea kufuatia maamuzi mabaya ya TRA, hivyo yameoza na hakuna magari tena. Uamuzi sahihi ni mzee huyu kupewa magari mapya na kulipwa fidia ya kutofanya kazi miaka 10.

Mzee akanikuta ofisini, akanieleza tatizo lake na nikaanza kulifanyia kazi mara moja maana tayari Dr. Slaa alikuwa amekwisha nieleza tatizo hili. Nikiwa ninachukua kalamu ili kudraft barua kwenda kwa Waziri Mkuu (ilii ichapwe na sekretari wa Dr. Slaa), mzee akainama na kuniambia,

' Mheshimiwa Zitto (ninamquote hapa maana sipendi kuitwa mheshimiwa) kama ukifanikiwa kunisaidia suala hili, nitakujengea nyumba nzuri Kigoma'

Kalamu ilianguka kwa kutetemeka kwa hasira......... Mratibu wa Ofisi yetu alikuwa ananiangalia na akitarajia (he knows me so well) kuachana na Mzee huyu....... Nilimtazama Mzee huyu na kumwambia 'Baba, hii ni haki yako huna haja kuinunua. Mimi pia hii ni kazi yangu, ninalipwa kuifanya. Sitaki nyumba yako. Sitaki chochote kutoka kwako.'

Mzee hakuelewa, akashangaa. Akasema, wenzako wameniomba nyingi, wewe ninakumba nyumba unakataa. Mimi siwaelewi wewe na Slaa. Mtakufa masikini.

Sikumjibu kitu, nikamaliza kazi yake na kuipeleka kwa Pinda.

Hii inadhihirisha kuwa upande wa wananchi pia ni tatizo. Wao ni chanzo cha Ufisadi.

Kuna haja ya kufanya 'overhaul' ya jamii nzima kuhusiana na suala hili. Wakati mwingine Tanzania suala la Rushwa huwa ni nani kapata. Mafisadi wanaonena wivu, asiepata anamsema aliepata. Yeye akipata kesho, anasemwa na aliepata jana. Tumefika hapo.

Muda mrefu sijachangia JF, ile hii post imenigusa sana.

Maudhui yake yamehitimisha kile ambacho nimewahi kukisema na kukiandikia mara kadhaa kwamba nchi yetu imeingia katika 'utamaduni wa ufisadi'. Ambapo ile dhana ya kila 'mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake'(ongezea mahali pake)- soma 'kazini kwake', imekuwa ni jambo la kawaida katika maisha ya watanzania.

Hili ndio tatizo na msingi ambalo kama taifa tunapaswa kulishughulikia kurejesha MAADILI na UWAJIBIKAJI.

Wazee wetu wanatuambia enzi za miaka ya awali ya Mwalimu ufisadi hakuwa umeshika kazi na kupenya katika mishipa ya wananchi na viongozi kama ilivyo sasa.

Swali la kujiuliza- ni kwa vipi tumefika hapa? Na tunarudi vipi katika misingi iliyokuwepo awali?

Wengine wanasema ni kwa sababu ya mabadiliko ya kiuchumi kuelekea uchumi wa soko ambao wengine wanajenga hoja kuwa unaambatana na ubinafsi na kutaka kujilimbikizia. Wao wanaamini kwamba ujamaa ungekuwa suluhu ya kuendelea kuwa na maadili.

Wengine waamini kuporomoka kwa uchumi kulikoleta hali ngumu ya maisha na hatimaye mishahara kushuka ukilinganisha na gharama za maisha kumepunguzia wananchi uwezo wa kununua na hatimaye sasa wafanyakazi wengine kugeuka wala rushwa mahali pao na watoa rushwa kwa wengine. Hawa wanajaribu kuelezea rushwa ndogo ndogo(petty corruption). Ukiwauliza ni kwa vipi matajiri wakubwa na viongozi wakuu wa serikali wenye mishahara mizuri na maslahi mazuri nao wanapokea na kutoa rushwa kubwa kubwa(grand corruption), wanakosa majibu mazuri.

Katika kukubiliana na rushwa, wapo waomini kwamba tukiweka sheria kali na kujenga taasisi zenye nguvu, rushwa itaondoka. Lakini wanasahau kwamba sheria zinapaswa kusimamiwa na watu, taasisi nazo zinasimamiwa na watu. Kama ukiwa na taifa lenye utamaduni wa ufisadi, sheria hata ziwe nzuri haziwezi kusimamiwa(rejea kauli ya rais kwamba watakaorudisha fedha za EPA watasamehewa- nimeijadili kidogo hapa: JJ: Rais Kikwete: mene mene na tekel; taifa linagawanyika ); mnakumbuka pia mfano(rejea hapa:TAKURU inalinda na kutetea Rushwa? ) wa Taasisi ya TAKUKURU(wakati huo TAKURU) ilivyoisafisha RICHMOND na mchakato wake.

Wengine wanasema basi tuanzie kwa kuweka viongozi waadilifu, halafu wao kwa maneno na matendo yao watasimamia utawala wa sheria na uwajibikaji wa taasisi hizo. Lakini uchaguzi kwenye taifa lenye utamaduni wa ufisadi mara nyingi huzaa viongozi mafisadi. Wananchi mafisadi huchagua viongozi mafisadi.

Kwa hiyo hili suala la ufisadi, ni kama hadithi ya kuku na yai- ni mjadala unaozunguka kusema kwamba kipi kilianza.

Kwa maoni yangu, sababu zote kila moja kwa nafasi yake inachangia katika utamaduni wa ufisadi. Ujamaa wa dola(naita ujamaa wa dola kwa kuwa nina mtazamo tofauti sana kuhusu uzuri na udhaifu wa ujamaa mfululizo wa uchambuzi wangu kuhusu hoja hii upo hapa: Tanzania, CHADEMA, CCM na mjadala wa falsafa na itikadi; Lipi ni jibu? ) ,ulizaa urasimu wa bidhaa na huduma ambao ulichangia katika baadhi ya wananchi kuanza kuweka pemebeni misingi ya maadili na uwajibikaji na kujiingiza katika utamaduni wa ufisadi. Viongozi waliochaguliwa baadaye walikuja tu kuchochea utamaduni wa ufisadi ambao tayari ilishaanza. Utadamuni ambao ulijengwa pia kwa raia kuweka mawazo yao yote kwa dola na serikali. Kushuka kwa hali ya maisha na kupungua kwa uwezo wa kununua kulikoambana na mishahara duni kuliongeza tu huu utamadauni wa ufisadi. Halafu ndipo tukaingia katika mduara ya ufisadi(the cycle of corruption); kwamba chama tawala na vingozi wake wanalinda ufisadi, wananchi nao wanazidi kuwa mafisadi katika mahali pao pa kazi na uchaguzi ukija mafisadi wengi zaidi wanachaguliwa; mzunguko unaoendelea. Sasa changamoto ni kuvunja huu mduara.

Kwa bahati njema, si raia wote ni mafisadi. Si viongozi wote ni mafisadi. Bado kuna tabaka la watu wachache ambao si mafisadi. Hatua za haraka zinahitajika kuchukuliwa na tabaka hilo kuliokoa taifa. Uzoefu unaonyesha kwamba utamaduni wa ufisadi huwa ukikomaa una kawaida ya ama kuangusha dola au kuazaa taifa lenye matabaka kati ya walionacho na wasionacho na lenye vurugu za kijamii. Tunapaswa tusifike huko kama taifa.

Kama ambavyo takaba la watu wachache liliamini kwamba mkoloni anaweza kutoka katikati ya tabaka la waliowengi waliomini kama mkoloni hawezi kushindika na kwamba kutawaliwa ni jambo la kawada na kwamba waafrika wameumbwa kutawaliwa; ndivyo inavyopasa kuwa kwenye suala hili la ufisadi.

Suluhisho ni kurudi kwa umma. Hao waadilifu wachache kwenda kwa wananchi kutoa elimu ya uraia, wananchi wakaunga mkono kwamba ufisadi wao ndio kaburi lao; kwamba ufisadi wa watawala ni jeneza tu la kuwabeba na kuwazika. Kwamba ufisadi unawaathiri zaidi wao wenyewe. Wananchi wakaelewa uhusiano kati ya maisha yao kuwa mabaya, huduma za kijamii kuwa mbovu na ufisadi. Wananchi wakajua kwamba ufisadi ni dhambi si ya kuliathiri taifa tu bali kujiathiri mtu mwenyewe. Hapo ndio wananchi watachukua hatua kwa nguvu ya umma. Tararibu tutajenga taifa lenye utamaduni wa maadili ambao mimi huwa napenda kuuita utamaduni wa uwajibikaji. (Niliwahi kugusia kidogo hii dhana hapa: 45th Anniversary: My greetings to you and reflections with Mwalimu Nyerere). Katika taifa la namna hiyo, viongozi wanamachaguo matatu; ama kukubaliana na sauti ya umma na wao kuanza kusimamia uwajibikaji(Rais Kikwete kuunda kamati ya bomani na Bunge kuunda Kamati ya Richmond ni matokeo ya umma kuanza kuchukua hatua baada ya Hoja ya Zitto kuhusu Buzwagi na hoja ya Dr Slaa kuhusu BOT. Kupelekwa kwa kesi za EPA ni matokeo ya yaliyojiri baada ya Kutajwa kwa Orodha ya Mafisadi); ama watawala kunyamaza(na wakati mwingine kugeuka madikteta) na kuruhusu kuzuka kwa utamaduni wa hukumu ya ujmma(mob justice) ambao unaweza kuwa na faida katika usalama wa taifa ama unaweza kutishia utangamano wa umma(unaweza kuwa na mifano ya hivi karibuni) ama wananchi kuvuta subira na kusubiri kuchukua hatua wakati wa chaguzi(kuondoa madarakani utawala na watawala waolinda ufisadi).

Lakini hatua hii inapaswa kwenda sambamba na umma kutaka hatua zichukuliwe ili kuboresha pia maeneo mengine mathalani suala la mishahara na usimamizi wa taasisi za uwajibikaji.

Hii ni njia ya amani kuelekea maadili na uwajibikaji. Njia nyingine ni kikundi cha watu wachache kujitwalia madaraka ama kwa sanduku la kura lakini mara nyingi kwa mapinduzi na kujivika dhima ya kulitoa taifa kutoka katika utamaduni wa ufisadi na kuelekea katika maadili na uwajibikaji. Hawa huitwa madikteta wakarimu!(mifano imewahi kutokea katiika mataifa mengine). Hawa huweka adhabu kali dhidi ya aina zote za ufisadi na huzisimamia adhabu hizo na hatimaye kujenga hofu katika taifa kwa mafisadi na hiyo watu kuacha ufisadi si kwa kuelewa au kwa kupenda; bali kwa hofu! Tatizo la msingi la njia hiyo ni kuwa linaanzia kwenye njia yenyewe na hivyo baada ya muda fulani watawala hao hao wenyewe hugeuka kuwa mafisadi kwa kujilimbikizia kutokana na mamlaka makubwa wanayokuwa nayo ama huishia kukataa kutoka madarakani na hatimaye kuzua tena utadamuni wa ufisadi.

Hivyo, nawapongeza Dr Slaa na Zitto kwa njia mliyoamua kuipitia. Mabadiliko huanzia kwa mtu mwenyewe, naamini kwa kukataa kwako umemuambukiza huyo mzee utamaduni wa uadilifu na uwajibikaji. Majaribu ni mengi lakini hakuna sababu ya kukata tamaa. Uovu hushamiri wema unapokata tamaa.

Lakini tukumbuke pia rushwa kubwa kubwa katika mataifa ya Afrika inachangiwa pia na mataifa ya nje hususani kupitia makampuni makubwa(MNC). Nilikuwa napitia sheria za nchi mbalimbali, mataifa mengi yanakataza ndani ya nchi zao mashirika yao kutoa chochote kupata zabuni lakini mataifa hayo hayo yametunga sheria ambazo zinaruhusu mataifa yao kuwahonga viongozi wa kifrika katika kupata zabuni. Hivyo uhusiano wa kimataifa umejengwa katika misingi ya utadamuni wa ufisadi uliojificha katika vivuli vya commission nk.

Jambo moja lazima tuamue, kama tunataka maendeleo ya taifa letu-hatuna jinsi zaidi ya kuendeleza utamaduni wa uwajibikaji. Ambapo kila mtu atawajibika kwa nafasi yake na atakayeshindwa kuwajibika atawajibishwa. Umaskini wetu umechangia katika ufisadi, lakini umaskini wetu sio chanzo kikuu cha ufisadi huu. Hivyo, lazima tufikiri zaidi na kuendelea kuchukua hatua.

BTW 1: Thread inahusu Kamati Kuu ya CCM, mod aidha badilisheni heading au hii michango kuhusu ufisadi ianzishwe thread yake.

BTW 2: Zitto, mpe hongera Chachage Jr.

BTW 3: Unaweza kuwa ulishawahi kuwa fisadi, ama ulishawahi kuwa fisadi lakini kama kuna chochote kinaweza kukugusa katika mjadala huu, unaweza kuwa wakala wa mabadiliko unayotaka kuyaona. Kwenye kitabu kitakatifu kimojawapo kuna hadhithi ya Saul ambaye alikuwa anachinja watu wa dini, baadaye akaongoka na kuwa Paulo mweneza dini.

BTW 4: Kwa fisadi yoyote anayesoma hapa-aelewe kwamba ufisadi ni uuaji wa taifa na wananchi walio wengi. Ni ubatili, sawa na kufukuza upepo! Ni raha ya muda fulani na karaha ya muda mrefu.

Nawakatika mjadala mwema mpaka panapo majaliwa

JJ
 
1. Hatulipi kodi ya allowances. Tunalipa kodi ya mapato kwa mshahara. Tanzania hakuna anaelipa kodi ya allowances hata mmoja. Hii ni moja ya hoja ambayo Kambi ya upinzani Bungeni inasema kila mwaka. TRA walisikia hoja yetu na kuleta Bili kwa Katibu wa Bunge ya kodi kwa miaka 10 iliyopita ambazo wabunge wamekuwa hawalipi maana Income Tax Act inasema posho ni mapto na hivyo lazima zikatwe kodi (sitting allowances na sio per diems, maana per diems are simply transfers). Unajua tulichofanya? Tulikasirika ni kwa nini TRA inaleta Bili Bungeni na kuamua kutunga sheria kwamba income tax act 2004 isitumike kwetu.

Hali ni hiyo hiyo kwa Majaji, nao katika sheria ya majaji hawalipi kodi katika posho wanazopata.

Mimi ninaamini tunapaswa kulipa kodi katika allowances za vikao maana ni kipato kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato. Nimesema hivi wakati wa mjadala wa sheria ya Majaji mwaka jana. Nilisema hivyo (hata kama wenzangu walichukia) ndani ya Bunge mwaka huu wakati wa mjadala wa Sheria ya Bunge (National Assembly Bill, 2008).

Ninaamni kuwa kulipa kodi ni uzalendo - ishara ya uzalendo.

Swali lingine?

Mheshimiwa Zitto,

Asante sana kwa uchambuzi makini na kujitoa sana katika kushughulikia watanzania Mungu akubaliki sana.

Suala la Ufisadi hasa wa shukranmi lip[o sana Serikalini na limechangaiwa sana na masiha magumu waliyo nayo wafanya kazi hao.Mathalani utakuwa Mtu ni Senior Office na analipwa Mshahara wa laki tano uila anaweza kufanya maamuzi ya zaidi ya millioni 100.Hapo unaona kuna tatizo.

Ili kupunguza Rushwa serikalini,Cha kwanza ni kuboresha maisha ya wafanyakazi wa serikali ,Serikali iwape uwezo wa wao kukopeshwa nyumba na watoto wao waweze kusomeshwa na serikali kwa gharama nafuu.

Back to the Point:

Mkutano wa NEC umekwisha ila nimeshtushwa sana na Ufadhili wa Goodfather wa Jeetu Patel,Somaiya wa millioni 400..Nahisi kuna jambo baya sana litakuja kutokea..Watuhumiwa wa EPA watakuja kulipwa Fidia baada ya kushinda kesi,Hakuna ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani watu hawa coz kuna sababu moja ya msingi sana....i know you know...Balali

Mtu mmoja anachangia 400m,na asitegemee kulipwa.?Hapa ndipo tunakosea..Nchi hii ilianza kuyumba pale tulipoana Vyama vyetu haviwezi kuenda bila kupata ufadhili wa wafanyabiashara..Unakumbuka kipindi Manji alivyombusu Manji...?
 
Wakuu someni analysis ya baadhi ya maandiko ya chachage na wenzake walipojaribu kuichambua nchi.

Hizi rushwa kuu hazikuanzia enzi ya mwinyi kama tunavyodhania, hii ni kuwekeza nguvu nyingi ktk kuangalia wapi tumeangukia na kuacha kujua kiini cha mweleka wetu. Ukiwasoma wanakupa data na taarifa za kichambuzi za kutosha zinazoonyesha kuwa nchi ilichimbiwa kaburi mapema sana ktk lindi la rushwa na mmomonyoko wa maadili pale watawala walipoacha kutuongoza kwa mujibu wa sheria na kuwajibika kwa kila jambo liwapasalo.

Epa ni mmoja wa mfano wa kutowajibika kimaono, kisera na kiuchumi kwa watawala wetu.

Epa ni fedha za wazalendo wa nchi hii waliokuwa na biashara za ku import ktk zama zile za kambarage, ilikuwa ni baada ya kutaifisha na udhibiti wa biashara ya nje pamoja na fedha za kigeni(mnyamwezi), serikali ilimtaka kila mwenya kuagiza bidhaa nje ailipe serikali madafu yenye thamani sawa na gharama zote za kuingiza bidhaa hiyo nchini, baada ya hapo order hiyo hiyo inapelekwa abroad na serikali yetu inamlipia huyu mtz , ikaenda ktk style hiyo mpaka pale nchi ilipoyumba kiuchumi, jkn na serikali yake ikajikuta inapokea madafu ya wananchi wake na kutoa order na garantii ya malipo kwa wadau huko abroad na bidhaa kuingia nchini huku wakishindwa kuwasilisha malipo stahili kwa wakati, hali ikaanza kuwa sugu na wakajikuta wanaanzisha akaunti hii ili hapo baadae wawalipe hao wadai na pia kujihami na upotevu wa taarifa za muhimu.

Baada ya muda mwingi makampuni mengi yaliyokuwa yakiidai tz kwa dhamana za wafanyabiashara wa kijamaa zama hizo walijikuta wanalipwa na bima na mengi yalishajifia automatically.

Serikali iliendelea kulundika mapesa ya wale jamaa ambao wanaidai ktk nbc, baada kubinafsishwa wakaamua mafungu haya yahamie bot.

Hapo tunajifunza wazi namna mfumo wa utawala wetu unavyoweza kuzalisha uovu halafu wewe na mimi tuakaanza kulumbana.

Nasisitiza rushwa ni janga la jamii na mzizi wake mkubwa ni mwanzo wa utawala wetu , wananchi hawakuandaliwa bali waliogopeshwa zaidi kwa adhabu kama viboko.

Tuombe mungu waungwana
 
Mkuu Kitila,

I begg to differ, I mean a proven fisadi hata kama ana msimamo namna gani, hawezi kua kiongozi anayetufaa wananchi na atakayemchagua atakwua ni kama yeye yaani fisadi, ni huzuni kwa mtu makini kama wewe kushauri tushushe standards kwa sababu ya hela za ufisadi za kiongozi fisadi kama Mkono.

Kitila tunataka kusafisha taifa letu sio kurudidsha wale wale mafisadi waliokwisha tambuliwa na DR. Slaa, eti kisiasa wana msimamo na hela nyingi za ufisadi, wananchi kama mimi na wewe tunatakiwa kulilia hawa mafisadi wafikishwe kwenye sheria sio kupewa tena uongozi!

asante kwa jibu lako maridhawa. haya ndio maneno, si kusema mtu ni genius labda huyo mtu aseme yeye ni genius. nafikiri tumeelewana kiungwana?
 
asante kwa jibu lako maridhawa. haya ndio maneno, si kusema mtu ni genius labda huyo mtu aseme yeye ni genius. nafikiri tumeelewana kiungwana?

Kitila ni mtu makini sana na wengi tunamtegemea siku moja kushika uongozi wa Chadema, kwenye maneno yangu ameiona hoja nzito ndio maana hakurudi, naona umegundua kuwa ya kunichonganisha naye yameshindwa maana hajajibu toka jana, sasa leo umebadilika lugha, ninawaonea huruma sana humu ndani wasiokujua vizuri maana ni wengi sana, tena wengine hata wanaoaminika.

Hoja yangu ni kwamba Mkono anatakiwa afikishwe kwenye sheria, sio kupewa uongozi tena, maana DR. Slaa alipomtoa kwenye ile list alisema atamfikisha kwenye sheria, sasa mbona mpaka leo hajaenda kama sio fisadi? Badala yake anataka uongozi zaidi tena na kuna watu kama wewe wanaomshangilia apewe uongozi badala ya kumpeleka kwenye sheria.
 
tunapopishana na wewe ni maneno yasio faa yanapo tumika eg kwenye ile issue ya epa ingawa sija comment sentensi ulio tumia ambayo haileti picha inaofaa au maana haliisi ni pale ulipo sema moja wa watuhumiwa hakuwa MASKINI, nafikiri hakuna mtu aliyesema walikuwa maskini, bali wanaweza kuwa watu wa hali ya juu, kati au yakawaida, na wale wa ngazi ya chini.
Sasa hawa wenzetu siwezi kuwaweka katika kundi la watu wa chini au wengi wetu hatuwaweki huko (maskini) sasa hayo mengineyo ni additional information, kama waliuza dagaa etc etc ni yao. Yakwetu ni pale mtu anapo tuinbia iwe mimi au wewe.
 
Hapana uko mbali sana na ukweli, Mkuu Kasheshe, alionyesha kushangaa kwamba bwana Lukaza ametoa wapi hela za dhamana, ndio nikajibu wazi kwamba familia ya Lukaza ni watu wenye uwezo siku nyingi sana, sio masikini kwenye hili sina cha ku-apologize maana sioni tatizo lako lilipo, ukiwa nazo ni tajiri ukiwa huna ni masikini, I have nothing to with it! Mimi sina uwezo ni masikini period hakuna butts about it!

Halafu kuwa muangalifu na maneno ya kiswahili, anayepishana na mimi ni wewe tu mtu mmoja sio tunapopishana na wewe hiyo ni lugha ya kinafiki ua kujaribu kuwaingiza na wengine wasiohusika ambayo ni kawaida yako, yaani kuchonganisha, ili u-divide na kutawala, kwenye hii mitego yako hutakuja kunipata hata siku moja, labda hao wengine uliokwisha wapata!

Kichwa cha mada hakuhusiani na haya ya personal unayajribu kuya-inject au?
 
By the way hii CCM ya kuanzia Mwinyi mpaka Kikwete ina tofauti kubwa na CCM iliyopita wakati wa Nyerere. [B]Kikwete aliahidi ahadi nyingi sana wakati wa kamoeni zake ambazo zilimfanya aingie madarakani kwa ushindi wa kishindo lakini hadi hii leo hakuna hata moja aliyoitekeleza. Kwa kifupi tunaweza kusema aliudanganya umma wa Watanzania umchague akichagua fika hana mpango wa kutimiza hata moja ya ahadi zake.[/B] Utakaaje madarakani miaka mitatu ushindwe kutimiza hata moja ya ahadi zako wakati wa kampeni? Kwa mantiki hayo basi kuchaguliwa kwa CCM hasa miaka ya karibuni kuanzia Mkapa ni ukosefu wa mawasiliano kupitia magazeti, radio na TV huko vijijini ambako Watanzania wengi ndiko wanaoishi. Wengi wanajua chama cha kukichagua ni CCM tu na wakishasikia neno 'wapinzani' basi wanawahusisha na machafuko. Hivyo kamwe hatuwezi kusema kuchaguliwa kwa CCM kunaonyesha sera nzuri zozote.

Kama kweli CCM viongozi wabovu na mafisadi wangekuwa wachache basi masuala haya yangepewa kipaumbele na walio wengi ndani ya chama hicho ili yajadiliwe bila woga wala kificho ili yapatiwe ufumbuzi na kama kuna sheria zilipindwa basi wahusika wote wachukuliwe sheria zinazostahili, lakini mpaka leo viongozi mafisadi na wabovu ambao ni wengi ndani ya CCM wanataka kuyazima haya yote kimya kimya.

BAK... UMEIBUA SUALA Moja la msingi.... uongo wa viongozi dhidi ya uwezo wa wananchi kupambanua ukweli na uongo. Kuna mwanamziki mmoja wa kizazi kipya aliwahi kuimba kuwa kampeni za kisiasa ni sawa na kutongoza mwanamke. Ukiangalia utaona kuna ukweli fulani maana ni kweli kuna ahadi lukuki hutolewa pale mtu anapotaka kukonga moyo wa anayemtamani na hasa kama matamanio hayo yamelenga kitu fulani ( KURA AU MAPENZI).Inakuwaje watanzania kwa miaka yote hiyo wameshindwa kupambanua ahadi hewa zisizoweza kutekelezeka na ahadi za kweli zenye uwezekano mkubwa wa kutekelezwa.Tuchukulie mfano ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania! Hivi kweli inahitaji kuvaa miwani kuona kuwa ahadi hii ni sawa na ndoto tu?
CCM itaendelea kushika madaraka hadi pale watanzania watakapokuwa na uwezo wa kutambua uongo from ukweli...au watakapoacha "kupenda kudanganywa"..

Tutaendelea kulalamika, kukosoa kwenye mijadala, makongamano, midahalo,mitandao..huku wao wakiendelea kufanya vitu vyao.Viongozi wazuri wanapokaa na viongozi wabovu kama tunavyoshuhudia kila siku ni uambukizo usiokuwa na kikomo.Hii itaendelea hadi pale kila mmoja wetu atakaposema BASI...NA SIJUI KAMA HII ITATOKEA MAANA WATU WANAONA MAOVU YANAYOTENDEKA NA HAKUNA HATUA KALI ZINACHUKULIWA.MATOKEO YAKE INAKUWA KAWAIDA NA HATIMAYE DESTURI KUFANYA MAOVU.
( do we have any other option?)
 
Back
Top Bottom