CCM yafuta matokeo ya uchaguzi wa UVCCM mkoa wa Simiyu kwa kilichodaiwa ni kuwepo kwa dalili wazi za rushwa

Je, sisi sote tumenawa kwa sabuni au tunawabana walionaswa na camera peke yao?
 
Wamefuta kwa sababu kulikuwa na DALILI ZA WAZI,hawakushughulika na DALILI ZILIZOJIFICHA!
 
Nini kuhusu vyombo vyetu vya usalama tukianza na TAKUKURU na polisi wamefanya kazi hayo yanayosemwa harufu ya rushwa ?

CCM na rushwa ni chanda na Pete mie sioni ajabu
 
It's not fair kufuta uchaguzi kwasababu tuu clip ya rushwa imeonekana public kupitia mitandao ya kijamii.
Baadhi yetu humu ni wana CCM, CCM yetu ya kisasa tunaijua, na tunajua what it takes ili uchaguliwe, we all know the name of the game, and the games people plays kushinda, hivyo tusifute chaguzi kwasababu tuu watu wamejua!.
P
"Tusifute uchaguzi kwasababu tuu watu wamejua"

Kumbe.
 
Hakuna rushwa CCM, kilichopo na kinachofanyikaga ni utoaji tuu wa fedha kidogo za uwezeshaji wa logistics support kama usafiri, nauli, kwa wana CCM waliopungukiwa nauli, na fedha kidogo za mchango wa kuimarisha chama, na kama una uwezo, hakuna ubaya wowote kuwakirimu wahumbe kwa kidogodogo cha takrima ya maji, soda, chakula na vitafunwa!. Hivi ndivyo siku zote tunavyo wa treat wajumbe wetu!.
Wajumbe ni watu muhimu sana, lazima wawe treated ipasavyo.
P
Ni aibu kubwa kabisa kwa mtu wa kiwango chako kusema uliyosema. Ukiweza kutafsiri tofauti kati ya bribery na corruption, utajua kuwa unatete corruption!! Corruption inakusudiwa kuelekeza ushawishi wakati bribery inaweza kuwa ni zawadi ya kufanya jambo. Katika yote hayo, kuna ushawishi na asiyetoa hiyo corruption anakuwa loser immediately.

You have stooped too low, bro.
 
It's not fair kufuta uchaguzi kwasababu tuu clip ya rushwa imeonekana public kupitia mitandao ya kijamii.
Baadhi yetu humu ni wana CCM, CCM yetu ya kisasa tunaijua, na tunajua what it takes ili uchaguliwe, we all know the name of the game, and the games people plays kushinda, hivyo tusifute chaguzi kwasababu tuu watu wamejua!.
P
😂😂😂😂 It takes alot
 
Ni aibu kubwa kabisa kwa mtu wa kiwango chako kusema uliyosema. Ukiweza kutafsiri tofauti kati ya bribery na corruption, utajua kuwa unatete corruption!! Corruption inakusudiwa kuelekeza ushawishi wakati bribery inaweza kuwa ni zawadi ya kufanya jambo. Katika yote hayo, kuna ushawishi na asiyetoa hiyo corruption anakuwa loser immediately.
Hao ndiyo waasisi wa mdudu takrima miaka ileeee!!
 
Wakati ndio kawaida yetu ila zoezi kama hilo halifanyiki hivi waziwazi hadharani, hufanyika kistarabu kwa staha.
P
Kwa kujificha watu wasione,ila watu wameona wamefuta.

So wafanye upya kwa kujificha wasionekane tena.

So unabariki tuishi humo,muheshimiwa paskali?
 
Sijasema hufanyika kwa kujificha, nimesema hufanyika kistaarabu na kwa staha!.
So wafanye upya kwa kujificha wasionekane tena.
No sio wafanye kwa kujificha, bali wafanye kistaarabu na kwa staha kama kwengine kote!.
So unabariki tuishi humo,muheshimiwa paskali?
No sibariki, bali taratibu ni kama sheria, huo ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa wanachama wenye uwezo kukichangia chama au kuwachangia wanachama individually michango midogo midogo ya nauli na maji ya kunywa!.
P
 
Chama Cha Mapinduzi kimefuta matokeo ya uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoa wa Simiyu kwa kilichodaiwa ni kuwepo kwa dalili wazi za rushwa.

Dodoma. Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimefuta matokeo ya uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoa wa Simiyu kwa kilichodaiwa ni kuwepo kwa dalili za rushwa.

Mbali na Simiyu, lakini CCM kimesimamisha uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kwa mikoa ya Arusha na Mbeya ambao wanatuhumiwa kutembeza rushwa huku wakionya uamuzi wa kufuta unaweza kuendelea katika maeneo yatakayobainika kukiuka sheria.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu Novemba 21,2022 na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa Chongolo, leo ni siku ya tatu timu maalumu ya uchunguzi ipo huko ikichunguza zaidi kuhusu kilichojili ili vikao vifanye uamuzi.

Chongolo ametaja sababu kuu ni vitendo vya rushwa ambavyo vimetajwa katika maeneo hayo na kuwa chama hakitavulimia vitendo hivyo pale inapobainika.

"Mbali na hilo, tunachunguza kuhusu uchaguzi wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi katika tuhuma za kada mmoja kubeba boksi la kura kwenda nalo chumba cha kuhesabia kura ikibainika tutatoa maelekezo ama ya kufuta matokeo au kuruhusu aliyetangazwa aendelee," amesema Chongolo.

Kiongozi huyo ambaye ni mkurugenzi wa uchaguzi ndani ya chama amesema hawako tayari kuona viongozi wanaingia madarakani kwa rushwa na vitendo viovu.

Kuhusu adhabu zitakazotolewa alisema ni kuondolewa kwenye mchakato wa uchaguzi na kupelekwa katika vyombo husika.

Chanzo: Mwananchi

View attachment 2422978
Aibu sana hii.
 
Afute nchi nzima kwani kote wamepata uongozi kwa rushwa,haya maeneo waliyokuwa uchaguzi jua kuwa wamepita watu wasiowataka
 
Wilaya ya Hai huko Kilimanjaro kura za ccm ziliibiwa na zoezi zima limeacha wilaya hiyo kwenye kilio kikubwa. Uchaguzi huo ufutwe tu
 
Back
Top Bottom