CCM yakanusha kukata majina ya waliochukua fomu

CCM yakanusha kukata majina ya waliochukua fomu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Chama Cha Mapinduzi(CCM)Kimekanusha taarifa zinazoesambaaa kwenye Mitandao ya Kijamii kuwa Kuna baadhi ya watia nia wa Udiwani na Ubunge majina Yao yamekatwa huku wengine wakifanikiwa Kupita katika mchakato wa uteuzi

Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Julai 13,2025 Jijini Dodoma Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, CPA Amos Makalla amesema kuwa hakuna mtu aliyekatwa,kuenguliwa wala kufuvyekwa kama baadhi ya taarifa zinavyosambazwa na baadhi ya watu kwenye Mitandao ya Kijamii

CPA Makalla amesema kuwa mchakato wa uteuzi wa majina hayo bado unaendelea na utahitimishwa na kikao Cha kamati kuu ya CCM

CPA Makalla ameongeza Kwa kusema kuwa kamati kuu itakapokamilisha uteuzi wa majina ya wagombea hao watatangaziwa ili majina hayo yaende kupigiwa kura ya maoni ndani ya Chama hicho

Aidha Makalla amesema kuwa nafasi ni Chache ikilinganishwa na watu waliomba hivyo wawe na uvumilivu na wawaunge mkono Kwa wale ambao watapata bahati ya kuteuliwa
 
Kukanusha bila kuweka wazi majina ya waliopo katika hatua ya sasa ya mchakato ni kushindwa kujibu hoja halisi.
 
Rais ni mzima anachapa kazi baada muda bendera ikapepea nusu mlingoti...

Hao, jamaa wa kijani sio wa kuamini sana
 
Ccm wameogopa baada ya kuona nyuma ya pazia kuna watu wanataka kuiteketeza kabisaa chama Kwa kifupi nia ilikuwa kuwaondoa akina mpina ila Kwa haya yanayoendelea wamekuwa wapole ghafla.
Wabunge wenye ushawishi na wananchi wataendelea kwenye majimbo Yao baada ya CCM kunusa kifo
 
Sasa vile vikao vyao vinavyofanyika kupendekeza majina matatu ni vya kazi gani?

Makalla katishwa na wimbi la wanaosema viongozi wa juu wana majina ya mfukoni
Inafurahisha sana unapofuatilia kwa umakini mkubwa mchakato wa uteuzi wa wagombea wa Udiwani na Ubunge nddani ya CCM! Hongera na endelea kufuatili kwa maana CCM ni dude kuuuuuubwa sana!!
 
Hata hivyo hizi taarifa zinavujishwa na watu wa CCM wenyewe!
Bado kuna mtifuwano chamani.
 
Chama Cha Mapinduzi(CCM)Kimekanusha taarifa zinazoesambaaa kwenye Mitandao ya Kijamii kuwa Kuna baadhi ya watia nia wa Udiwani na Ubunge majina Yao yamekatwa huku wengine wakifanikiwa Kupita katika mchakato wa uteuzi

Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Julai 13,2025 Jijini Dodoma Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, CPA Amos Makalla amesema kuwa hakuna mtu aliyekatwa,kuenguliwa wala kufuvyekwa kama baadhi ya taarifa zinavyosambazwa na baadhi ya watu kwenye Mitandao ya Kijamii

CPA Makalla amesema kuwa mchakato wa uteuzi wa majina hayo bado unaendelea na utahitimishwa na kikao Cha kamati kuu ya CCM

CPA Makalla ameongeza Kwa kusema kuwa kamati kuu itakapokamilisha uteuzi wa majina ya wagombea hao watatangaziwa ili majina hayo yaende kupigiwa kura ya maoni ndani ya Chama hicho

Aidha Makalla amesema kuwa nafasi ni Chache ikilinganishwa na watu waliomba hivyo wawe na uvumilivu na wawaunge mkono Kwa wale ambao watapata bahati ya kuteuliwa
View attachment 3404618
CPA Makala ndiyo mdudu gani?
 
JF ina mchakato wao wa kuteua watia na CCM ina mchakato wao wa kuteua watia na maelezo ya kina A to Z.

Saa zingine JF unakuta unabishana na watu wanaotoa mambo vichwani kwao tu.
 
Kipindi cha uchaguzi walikuwa wanakwangua ata bara bara, ila kipindi hiki wako wenyewe hamna upinzani hawajali ukipita kura za maoni tayari wewe mbunge.
 
Back
Top Bottom