King Kong III
Platinum Member
- Oct 15, 2010
- 64,227
- 98,761
Chama Cha Mapinduzi(CCM)Kimekanusha taarifa zinazoesambaaa kwenye Mitandao ya Kijamii kuwa Kuna baadhi ya watia nia wa Udiwani na Ubunge majina Yao yamekatwa huku wengine wakifanikiwa Kupita katika mchakato wa uteuzi
Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Julai 13,2025 Jijini Dodoma Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, CPA Amos Makalla amesema kuwa hakuna mtu aliyekatwa,kuenguliwa wala kufuvyekwa kama baadhi ya taarifa zinavyosambazwa na baadhi ya watu kwenye Mitandao ya Kijamii
CPA Makalla amesema kuwa mchakato wa uteuzi wa majina hayo bado unaendelea na utahitimishwa na kikao Cha kamati kuu ya CCM
CPA Makalla ameongeza Kwa kusema kuwa kamati kuu itakapokamilisha uteuzi wa majina ya wagombea hao watatangaziwa ili majina hayo yaende kupigiwa kura ya maoni ndani ya Chama hicho
Aidha Makalla amesema kuwa nafasi ni Chache ikilinganishwa na watu waliomba hivyo wawe na uvumilivu na wawaunge mkono Kwa wale ambao watapata bahati ya kuteuliwa
View attachment 3404618
Tushajua watu wamekatwa maana hao wajumbe waliopo kwenye hizo kamati tunaishi nao mitaani.
1.Mwita Waitara Mikwabe - Fyekelea Mbali
2.Luhaga Mpina - Fyekelea Mbali
3.Furaha Dominic - Fyekelea Mbali
4.Mrisho Gambo - Fyekelea Mbali
5.Ole Sendeka - Fyekelea Mbali
6.January Makamba -Fyekelea Mbali.