GE2025 CCM yakanusha matumizi ya namba feki za magari zenye alama SSH 2530

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekana kuhusika na matumizi ya namba feki za magari zenye alama SSH 2530. Akizungumza na waandishi wa habari leo, Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Saipulan Ramsey, alisema chama hicho hakina mamlaka ya kutengeneza vibao vya namba za magari kwani kuna taasisi husika zinazoshughulika na jukumu hilo.

Aidha, Ramsey alibainisha kuwa CCM haijatoa kibali kwa mwanachama wake au kwa mwananchi yeyote kutengeneza au kutumia namba hizo, na akasisitiza kuwa yeyote atakayebainika kufanya hivyo atakua anakiuka sheria za nchi

Nimeshakutana na magari zaid ya kumi nikajiuliza hivi ikitokea shida tunaanzia wap
Imagine gari lenye namba hizo likisababisha ajali na kukimbia litatambuliwa vipi.
Au wahalifu wakiamua kumbandika namba hizo na kwenda kufanya uhalifu litatanbulika vipi.
Polisi wamekaa kinya kuuona huu uhalifu wakati wana kauli yao ya til sheria bila shuruti
 
In a kakistocratic society lawlessness is the order of the day
 
CCM ipo taabani shida ni kuwapa wezi madaraka. Uingia pale chini Mlimani City hayo magari yapo na vibaka Trafiki wapo kama hawayaoni. CCM ni laaaana
 
CCM inawaongoza Watanzania kama Wanyama, wanaamini wananchi hawana akili kabisa, ngoja tuone kama wananchi wenyewe watakubali kupuuzwa kwa kiwango hiki
ibilisi wa ccm walikwisha wadharau watanzania sana wanajua hawana cha kuwafanya sasa IGP na Traffic wake yaani Polisiccm wanaimba nyimbo moja ya ibilisi wa ccm magari yanatembea hayana namba mengine Tinted hadi vioo vya mbele utazani Nchi haina Serikali , South Africa ulaya America ni marufuku kwa Gari kuweka tinted kioo cha mbele lakini Tanzania ni ruksa kuweka hata kwenye side mirror Nchi imeingiliwa mkoloni toka Zanzibar anahangaika kuididimiza chadema huku mambo ya hovyo yakiongezeka mitaani
 
Magari mengi yanatembea yakiwa hayajalipiwa kodi hususani yenye namba za South Africa ambayo huingia Tanzania kama yanakuja kutembea na kurejea South Africa na mengine sasa wanaweka namba SSH ili kukwepa kukamatwa na TRA, Nchi inapata hasara kwa ukwepaji kodi mkubwa unaoendelea kwenye show room zinazoota kama uyoga kwa njia haramu za utakatishaji fedha
 
Wengine hupachika namba hata za gari mbovu au hata SU wanatembea barabarani hawaogopi Polisiccm kwani juzi wamechangia chama
 
Magari mengi yanatembea yakiwa hayajalipiwa kodi hususani yenye namba za South Africa ambayo huingia Tanzania kama yanakuja kutembea na kurejea South Africa na mengine sasa wanaweka namba SSH ili kukwepa kukamatwa na TRA, Nchi inapata hasara kwa ukwepaji kodi mkubwa unaoendelea kwenye show room zinazoota kama uyoga kwa njia haramu za utakatishaji fedha
Yah ni kweli,magari mengi yenye namba hizo SSH 000 ni za kunjunga tu
Watu wamejiongeza wametumia mwanya wanajuwa wale wanapenda sifa wataziachia tu
Ila nawashanga TRA na POLICE muda wote huo wameziachia tu
Hawazigusi

Ova
 
Magari mengi yanatembea yakiwa hayajalipiwa kodi hususani yenye namba za South Africa ambayo huingia Tanzania kama yanakuja kutembea na kurejea South Africa na mengine sasa wanaweka namba SSH ili kukwepa kukamatwa na TRA, Nchi inapata hasara kwa ukwepaji kodi mkubwa unaoendelea kwenye show room zinazoota kama uyoga kwa njia haramu za utakatishaji fedha
Sababu yako ni MUFILISI.
Kwani usajili wa namba ni mamlaka ipi inayofanya?hivi mtu anaweza kukurupuka tu akaweka plate hizo bila serikali kujua?
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekana kuhusika na matumizi ya namba feki za magari zenye alama SSH 2530. Akizungumza na waandishi wa habari leo, Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Saipulan Ramsey, alisema chama hicho hakina mamlaka ya kutengeneza vibao vya namba za magari kwani kuna taasisi husika zinazoshughulika na jukumu hilo.

Aidha, Ramsey alibainisha kuwa CCM haijatoa kibali kwa mwanachama wake au kwa mwananchi yeyote kutengeneza au kutumia namba hizo, na akasisitiza kuwa yeyote atakayebainika kufanya hivyo atakua anakiuka sheria za nchi

Imagine gari lenye namba hizo likisababisha ajali na kukimbia litatambuliwa vipi.
Au wahalifu wakiamua kumbandika namba hizo na kwenda kufanya uhalifu litatanbulika vipi.
Polisi wamekaa kinya kuuona huu uhalifu wakati wana kauli yao ya til sheria bila shuruti
Tatizo lipo police, kwa nini traffic police hawayakamati, kubandua na kutoza fain.
 
Wakati wa JK, tulikumbana na matatizo makunwa ya nani ni mtawala halisi, wakati wa JPM tukapata mtawala, sasa tumerudi nyuma ya JK, hata wenye akili hawajui tuliko na tunakoelekea.
 
Back
Top Bottom