CCM Yamchagua Sitta kuwa mgombea pekee

Kama habari inayosemwa niya kweli, basi CCM imewapa wajumbe wa upande wa pili ndani ya Bunge la Katiba kile walichokuwa wanakipigia kelele sana kwa maana nyingine, imewapa kisu ili wajichinje wenyewe.

Kama kuna mtu anadhani Mh. Sitta atafanya mambo kinyume cha matakwa ya CCM basi huyo lazima akajifunze historia ya wanasiasa ndani ya CCM hasa ikichukuliwa kuwa, hili swala nila chama na siyo makundi ndani ya chama. Linapokuja swala la maslahi ya CCM, sioni Mh. Sitta akienda kinyume na matakwa ya chama chake.

Ninapoangalia mchakato huu, ninaiona CCM ikiwa imejiandaa na huku upande wa pili wakiwa na fikra za namna ya kuzima moto na siyo kuzuia moto usitokee. Upande wa pili unang'ang'ana na hoja ya kusema wafanye kazi kulingana na "matakwa" ya "wananchi" lakini wanashindwa kuelewa kuwa, hata CCM nayo ni wananchi na kwa maana nyingine, CCM inafanya kazi kwa matakwa ya "wananchi"

Kwanza jaribu kuangalia ile timu ya watu 20 ambayo kwa sasa inafanya mapitio na kurekebisha rasimu ya kanuni za uendeshaji wa bunge la katiba na hiyo itakusaidia kupata taswira ya CCM katika zoezi la katiba.

CCM ndiyo iliyotoa idhini ya kuandikwa kwa katiba nani CCM hiyo hiyo inayoongoza njia katika mchakato wa katiba na pia ni CCM hiyo hiyo itakayotoa hitimisho katika mchakato wa katiba.

Kama ukitaka kunielewa zaidi, rejea kauli ya jana ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambayo iliwafanya wajumbe karibia wote kusikiliza na kukubali anachokisema baada ya wajumbe kurumbana sana wakati kisheria, Waziri mkuu kwenye bunge la Katiba kwa sasa ni mjumbe tu kama wajumbe wengine.

Hii kauli hapa chini iliwafanya wajumbe kukaa kimya na kufanya alichowaeleza,
Jina la Mh. Chenge liliwafanya wajumbe wengi wa upande wa pili katika bunge la katiba kudhani kuwa CCM iko katika makundi hata katika kuzisimamia sera zake kitu ambacho kimeonyesha ni tofauti ndani ya vikao vyao kama ilivyotokea katika kupata mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge la Katiba.
 
Kwani Sitta si mmojawapo wa WanaCCM waliozuiwa kugomea cheo chochote kwa miezi 12 au hii haina uhusiano..
 

Hoja hapa ni kuchagua shetani bora miongoni mwa mashetani.Ni yupi mwenye madhara zaidi,kisha unachagua mwenye madhara kidogo.Huyo ndiye shetani bora kuliko wengine ingawa ubora wake haumfanyi kuwa Malaika.Atabakia kuwa shetani tu
 
Kwani Sitta si mmojawapo wa WanaCCM waliozuiwa kugomea cheo chochote kwa miezi 12 au hii haina uhusiano..
CCM hawawezi kusema kwa sauti ya kichama kuwa Mh. Sitta ni mgombea wao kwa sababu taratibu na sheria haziwaruhusu kutanguliza mambo ya kichama kwenye mchakato wa katiba mpya.

Haya ni makubaliano ya faragha ndani ya chama ikiwa ni njia ya CCM kupata kile inachotaka ndani ya mchakato wa katiba.

Mh. Sitta haruhusiwi kugombea cheo ndani ya chama lakini anaruhusiwa kufanya hivyo nje ya chama.
 
Huu mchezo unaenda kuzuri sana.
[(Sita + Lowasa * Udini - Ufisadi)] / [(CCM - Sita-Lowasa-Mwakyembe- Magufuli)]= Raisi wa Upinzani 2015
 
Huna hoja mkuu pengine unalingine la msingi lakini hili jepesi sana halina mashiko kabisa.
 
Huna hoja mkuu pengine unalingine la msingi lakini hili jepesi sana halina mashiko kabisa.
Uwezo wako ni mdogo sana hakunavunachowaza zaidi ya kutetea ujinga....ukweli unabaki pale pale ccm wanatuchezea akili kwenye huu mchakato wa katiba mpya...
 
mbona hivi vigezo vyote vya kuwa mgombea wa uenyekiti wa bunge la katiba ni kama vile ilikuwa kumnadi na kumpittisha sitta??
 
Hoja hapa ni kuchagua shetani bora miongoni mwa mashetani.Ni yupi mwenye madhara zaidi,kisha unachagua mwenye madhara kidogo.Huyo ndiye shetani bora kuliko wengine ingawa ubora wake haumfanyi kuwa Malaika.Atabakia kuwa shetani tu

Kwa maneno haya maana yake wewe naye uko tayari na ndivyo huwa unafanya, yaani unamchagua shetani bora badala ya kumchagua malaika au kuwa radhi kuharibu kura yako ikiwa wamesimama mashetani watupu.
 
Hoja hapa ni kuchagua shetani bora miongoni mwa mashetani. Ni yupi mwenye madhara zaidi,kisha unachagua mwenye madhara kidogo.Huyo ndiye shetani bora kuliko wengine ingawa ubora wake haumfanyi kuwa Malaika.Atabakia kuwa shetani tu

Kwa mtu ambaye ni makini na hasa ambaye amepewa nafasi pana katika maamuzi, basi nilitegemea kutomchagua shetani kabisa bila kujali kama ni shetani bora au siyo bora.

Kwa maana nyingine, unajenga hoja kuwa, bunge la katiba halina watu wenye uwezo wa kuwa mwenyekiti zaidi za Mh. Sitta and Mh. Chenge.

Angalizo hili linaturudisha kule kule kuwa upande wa pili wa wajumbe nje ya CCM umeingia bungeni bila kujiandaa vizuri kukabiliana na changamoto kama hii ya kupata Mwenyekiti wa bunge.

Ulichofanya ni kuisimika hoja yangu in different context.
 
Huu mchezo unaenda kuzuri sana.
[(Sita + Lowasa * Udini - Ufisadi)] / [(CCM - Sita-Lowasa-Mwakyembe- Magufuli)]= Raisi wa Upinzani 2015
Mkuu Samahani unaweza kunisaidia kwa kufafanua zaidi.
 
yaani wewe taahira sijui unatumia kiungo kipi kufikiri

We ----- umejiunga juzi humu leo unajifanya unajua ............... Naona imekuuma kweli mpaka unafatilia posting zangu ili tu uandike hilo taahira!! Umo humu kuongeza namba tu!! MEMBERS wa MUSIMU mtapita tu kama upepo!!
 

.
Hii picha mheshimiwa S alikuwa na dalili zote za uoga....
Ndo kusalimiana gani huko mtu unainama kiasi hiki, tena ukimsalimia mwanamke!
.
 
genekai
Siku zote tunasema Chadema ni wapiga deal hamna jipya; wao waliwaza posho zaidi; katiba tulipaswa kuipigia kura moja kwa moja; watanzania tunafahamu tunahitaji kitu gani; upinzani mlishindwa kushinikiza hilo kwa njaa zenu sasa unalaumu nini?
Sijui kama umeshirikisha ubongo kabla ya kupost hii kitu!!!!!!
 
genekai
Siku zote tunasema Chadema ni wapiga deal hamna jipya; wao waliwaza posho zaidi; katiba tulipaswa kuipigia kura moja kwa moja; watanzania tunafahamu tunahitaji kitu gani; upinzani mlishindwa kushinikiza hilo kwa njaa zenu sasa unalaumu nini?



Huyu jamaa nadhani huyu jamaa anaejiita Chama, anakurupuka kuongea vitu ambavyo hana uhakika navyo. Ningependa kumkumbusha tu kwamba, wale wajumbe waliotaka kuongezewa posho wao wenyewe walitishia kuwa bila posho kupanda, hawata-support mapendekezo ya serikali mbili! Je, Serikali mbili ni chama gani kina-support?
 
Mkuu japo sikumaanisha wengi waelewe iko hivi? Naona kiza kimakundi:-

*Kundi Fisadi (hawa jamaa wana hela sana tena ya ''kurithi''. kutoka kwa nani usiniulize tafadhali
*Kundi lisilo Fisadi (Hawa wanauma na kupuliza na wanataka tuamini wanapopuliza, wakiuma sio wao)
*Kundi Udini (Kwa gharama na karata yeyote (utaifa-ubara na usiwani/ukanda/jinsia/etc) – Bahati nzuri kwa wenye macho wanajua tayari ni Buddha kama sikosei ila usiniulize nimejuaje)
*Kundi Pendwa (Wanajiaminisha wanapendwa sana na wananchi) vigezo wanavyotumia havijulikani hata kwao wenyewe.

Ingekua yule Mwl Mkali yupo angeibuka tu na mtu wake makundi yote yakamsikiliza, kwa kuwa yuko ng'ambo ya ardhi hii na hata kama angekuwepo wasingemsikiliza kama wakati ule wa yule mwandishi kuelekea hii ngwe. Sioni usalama wa makundi na hiki chama wakati huo huo wote wako hai kisiasa au kimwili.

Sijui kama nimeeleweka kidogo au nimechanganya zaidi Mkuu? Vinginevyo tutamuomba Mkuu PakaJimmy alieipatia hio MAGAZIJUTO asaidie kung'amulia zaidi

Asante.
Tz
NB: Kwa nini Sitta na kwa nini sasa na sio 2010? hio connection unamalizia mwenyewe.

Mkuu Samahani unaweza kunisaidia kwa kufafanua zaidi.
 
Ningelikua mbunge nisingeshiriki mchakato wa katiba mpya.
 
mzee wa speed na viwango,anaweza kutufanya tupate kile tukitakacho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…