CCM Yamshambulia vikali Joseph Warioba

Chaajabu dada zetu ma mama zetu wanashangilia utafikili kinachoongelewa ni cha maana yani hizo kanga ma vitambaa vinasababisha hata tukose utu mh hii nchi sijui ina Lana?
 
Bulembo kweli akili zake ni pumba. kwani aliyoyaandika warioba katika rasimu yametoka kichwani mwake? Aliyoandika warioba katika rasimu ni yale maoni ya wengi aliyokusana toka kwa wananchi sasa bulembo anataka kumuonea bure mzee wa watu. bulembo amuombe radhi warioba na wananchi wote waliotoa maoni ambayo tume waliyanukuu rasimuni.
 
Wasitumie nguvu nyingi bila sababu,wanaweza kutamka tu Katiba hakuna na tunaohitaji katiba bora ya watanzania tutashukuru zaidi,maana NIA ya Katiba hawakuwa nayo.
Hapo tatizo ni kudandia Gari njiani usilojua linakoelekea, likifika njia panda lazima uchanganikiwe kama litaelekea usikokwenda.

CCM wananikumbusha kisa cha Bwana Matata katika kitabu cha JIFUNZE KUSOMA WAKATI NI HUU!.

Washuke sasa wakalie GOGO.
 

Hii ndio shida ya kupita darasani kama kupeleka mifugo joshoni lisilo na dawa, maskini Bulembo anafikiri yeye ni bora kuliko Sinde warioba na CCM ndio watanzania!! Bulembo New Metro Merchandise yako inadaiwa na manispaa Arusha, kalipe deni kwanza upate moral authority ya kukemea wazee!
 
Najiuliza hawa CCM ni nani msemaji wao mkuu maana kila mtu anajifanya katibu mkuu au Nape. Matamshi ya mwenyekiti wa wazazi jana yalinistua, lakini si hivyo tu mara nyingi matamshi yake yamekuwa hayalingani na cheo chake. Niliwahi kumsikia akisema viongozi wa serikali (walioteuliwa na rais) wasipotimiza wajibu wao chama (sijui cha wazazi) kitawaondoa madarakani. Jana nimeshangaa tena alipomrukia mzee Warioba na tume yake. Jamani mchungeni huyo mtu wenu, jana pia nimemsikia akisema mkurugenzi wa halmashauri sijui Pangani asiingilie kabisa shule za wazazi, hivi shule isipodhibitiwa na mkurugenzi wa halmashauri tatizo kubwa likitokea aulizwe nani kama siyo mkurugenzi, huyo ndiyo mwenyekiti wa wazazi, wakati mwingine najiuliza hawa wazazi anaowawakilisha ni akina nani hao. Nashukuru kwamba kati ya hao anaowakilisha mimi si mmoja wao. Katibu Mkuu wa CCM ana busara sana hajaona haya ya huyu mwenyekiti kwa madhumuni ya kumfunga gavana kwa usalama wa CCM?
 
Katika maswala muhimu Kama haya tuchunge ndimi zetu si kurushiana Maneno. Hivi jamaa na Mzee wetu Warioba nani anauzoefu na inchi hii!!
 

mkuu maccm ni sawa na samaki aitwaye kambale, baba,mama,mtoto,mjomba,bibi wote wana ndevu hujui nani ninani. hata bulembo std seven amekuwa msemaji wa maccm!

kweli kifo cha nyani miti yote huteleza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…