CCM Yamshambulia vikali Joseph Warioba

CCM Yamshambulia vikali Joseph Warioba

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Abdallah Bulembo amemshambulia kwa maneno makali Mkiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Warioba.

Akihutubia mkutano wa CCM Tanga Bulembo amesema Warioba hana haki wala mamlaka ya kuwasemea Watanzania kuhusu Katiba mpya.

Bulembo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu CCM amesema Warioba anapaswa kukaa mbali na kuwaamulia Watanzania Katiba aitakayo yeye.

Huku akisisitiza kupinga kinachofanywa na Warioba aliwauliza wananchi kwa msisitizo..'Kwani Warioba ni Nani?' ....

Itakumbukwa Abdalla Bulembo alishindwa vibaya kwenye uchaguzi wa udiwani 2010 na mgombea wa CHADEMA.

Source:ITV
 
Huyu Bulembo ni MAJANGA tu, amejaa uccm wala HANA UTAIFA.
 
Safi sana bulembo tunataka Ccm ijipambanue uzezeta wa viongozi wake ili umma wa watanzania na mkuu wa nchi awatambue na mwisho wa Siku tukae meza moja kujadili katiba na si kupitisha kwa wingi wao.hata Pinda kachemka Huko kigoma eti wana yo haki ya kuamua fate ya katiba kwa wingi wao
 
Bulembo hivi nae ni mtanzania kweli au anajipa utanzania,funga domo bulembo:shut-mouth:
 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Abdallah Bulembo amemshambulia kwa maneno makali Mkiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Warioba.

Akihutubia mkutano wa CCM Tanga Bulembo amesema Warioba hana haki wala mamlaka ya kuwasemea Watanzania kuhusu Katiba mpya.

Source:ITV
Hivi huyu jamaa anayeitwa Bulembo amewahi kupimwa akili yake? Ni jambo lipi ambalo Warioba amelisema lisilo na afya kwa mustakabali mwema wa Taifa letu? Hakika ccm imeishiwa viongozi kama jamii ya kina bulembo,nape,mwigulu,wassira,lukuvi nk ndio viongozi tegemeo wa chama hicho.
 
kweli nimeamini ukiwa CCM huwezi kuwa na akili timamu,yaani hawa magamba pumba wanazoongea utatamani hata kutapika
 
Huyu Bulembo ni MAJANGA tu, amejaa uccm wala HANA UTAIFA.

Kiongozi!

Wala sio U-CCM. Yaani hilo jamaa kichwani hamna kabisa. sawa na lile jamaa jingine la Dodoma. Wote ni ma-KJ.

Hivi akisema Jaji Warioba hana mamlaka ya kuwasemea waTanzania, ina maana hizo kelele zinazo toka kila kona ya Tanzania zote ni za Jaji Warioba? Kweli ni lazima uwe na akili ya maiti kuitetea CCM.

Yeye asubirie 2015 ndio ataona jinsi CCM inavyo wafia mikononi mwao. Tunasubiria Tume Huru ya Uchaguzi kuanzia vijijini hadi Taifa. Hapo ndio wataona moto wa mabadiliko. Hakuna cha sijui POLICCM wala nini.
 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Abdallah Bulembo amemshambulia kwa maneno makali Mkiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Warioba.

Akihutubia mkutano wa CCM Tanga Bulembo amesema Warioba hana haki wala mamlaka ya kuwasemea Watanzania kuhusu Katiba mpya.

Source:ITV[CCM itaiingiza nchi kwenye machafuko. Huyu mwenyekiti naamini ukimuuliza kosa la Warioba hawezi kueleza la maana!/QUOTE]
 
Hivi huyu jamaa anayeitwa Bulembo amewahi kupimwa akili yake? Ni jambo lipi ambalo Warioba amelisema lisilo na afya kwa mustakabali mwema wa Taifa letu? Hakika ccm imeishiwa viongozi kama jamii ya kina bulembo,nape,mwigulu,wassira,lukuvi nk ndio viongozi tegemeo wa chama hicho.

huyo jamaa ni std 7 hayo maneno analishwa na mpambe wake mbeba box alie lost le mutuz na ndo anazunguka naye mikoani,ukisoma post za william malecela kuhusu Warioba na maneno ya Bulembo leo ni copy n paste
 
Unaweza ukahisi kuwa ukiwa waziri mkuu, lazima uwe na akili timamu kwa vitendo, au ukiwa raisi, lazima uwe na akili za kimaamuzi yenye busara kuliko mtu mwingine yeyote katika taifa husika, lakini mmhhh....hapa kwetu, akili na uwezo wa kiuongozi wa viongozi wetu wakuu wa taifa hili ni wakutiliwa mashaka, hasa ukifocus in their decision making especially in very crucial issues kama katiba mpya, Pinda ameshasema hatogombea tena, lakini eti anataka na yeye hakikishe ccm inabaki madarakani ili tuendelee kuwa maskini....kikwete anamaliza muda wake, hana lingine ambalo taifa hili litamkumbuka kwalo, zaidi ya kutuachia katiba mpya ya watz wote, tena atuache nchi hii ikiwa na amani ya kweli, siyo hii ya kila siku vyombo vya ulinzi hasa polisi na usalama wa taifa kutuhumiwa kuhusika kwenye matukio makubwa ya utekaji na utesaji wa watu....Kikwete taifa hili litabaki na historia juu yako, Nimewahi kuandika hapa kuwa KIKWETE ANA NAFASI MBILI KUBWA,
1. KUIKABIDHI NCHI HII KWA CHAMA KINGINE NA KUICHA NCHI IKIWA SALAMA NA YENYE AMANI AU,
2. KUIKABIDHI NCHI HII KWA CCM KWA NGUVU YA DOLA NA TUME FEKI YA UCHAGUZI LAKINI AICHE NCHI KWENYE MACHAFUKO, NA KATIKA HILI, the hegue haitamuacha salama....KATIBA MPYA YA WATANZANIA NDIYO SULUHU YA KILA JAMBO.
 
Tunataka katiba ya watanzania siyo katiba ya mtu....bulembo.
 
Hivi Bulembo alifika hata Sekondari?Nasikia kama alikwamia standard seven hivi,Ujanja ujanja wake tu ndio umemfikisha hapo alipo,Si unajua tena jinsi WanaCCM wengi walivyo!!!??Hawa ndio wanataka kujigeuza wasemaji wa Watanzania wote wakiwemo wale wenye uelewa mkubwa kuliko hata yeye kwenye masuala mazito na nyeti kama haya.Mungu atupishie mbali na majanga haya ya CCM yanayojiita Viongozi.
 
CCM imejaa vichaa, kwani kazi ya kukusanya maoni waliyompa walifikiri anakusanya maoni ya magamba peke yao. Cha muhimu Ulaghai wa CCM kuleta katiba ya usanii tumeushtukia
 
huyo jamaa ni std 7 hayo maneno analishwa na mpambe wake mbeba box alie lost le mutuz na ndo anazunguka naye mikoani,ukisoma post za william malecela kuhusu Warioba na maneno ya Bulembo leo ni copy n paste

Uko kichwani mwangu, hayo ni kweli kabisa, maneno yote kalishwa na yule mzee mwenzake, na yeye kayasema bila kupunguza hata moja.

Hizi dharau zao zitakuja kuwatokea puani, kwani watanzania wa leo sio wale wa 1961
 
Mi namshauri ahachane na siasi..a jikite zaidi kwenye biashara zake za vyoo vya kulipia.
Roja zati..
 
Mbona wanahangaika na mzee warioba?? Warioba hana aliloiandikia na kulitangaza, katamgazamaoni ya watanzania na ndio anayasimamia.. Upumbavu wa ,maccm ni kudhani wao ndio wasemaji wa watanzania.
 
Back
Top Bottom