PreGE2025 CCM yapitisha marekebisho matatu kwenye Katiba ya chama chao ikiwemo vikao vya chama kufanyika kwa njia ya mtandao

PreGE2025 CCM yapitisha marekebisho matatu kwenye Katiba ya chama chao ikiwemo vikao vya chama kufanyika kwa njia ya mtandao

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Blessed Tajiri

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2023
Posts
284
Reaction score
870


Wakuu, CCM wanafanya mkutano wao mkuu maalum leo na kesho (May 29-30) Dodoma, nadhani an wengine watafuatilia mahala walipo kwakuwa sehemu ni ndogo.

Nini kitajili leo, Gwajima hatimaye atavuliwa uanachama? Tutaona yatakayojiri.

============================================

Chama Cha Mapinduzi kimepitisha marekebisho matatu kwenye katiba yao.
Marekebisho hayo yaliyopitishwa ni pamoja na:

1. Mikutano ya CCM kwenye ngazi ya Sektratrieti ya Wilaya, kamati ya siasa Wilaya, Sekretariati ya mkoa, Kmati ya Siasa mkoa, Sekretariati ya kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mkutano Mkuu wa taifa vitakuwa vinafanyika kwa njia ya mtandao.

Kwenye pendekezo hilo, mikutano hiyo ya mitandao itafanyika kwa dharura tu na kwamba Katibu Mkuu wa chama atatakiwa kupewa taarifa pindi mikutano hiyo itakapokuwa inafanyika

2. Baraza la Wadhamini CCM litaongezeka kutoka kuwa na wadhamini 8 kwenda hadi wadhamini 9.

3. Baraza la wadhamini CCM litatoa idhini kwa maandishi kuhusu miradi ya CCM ambayo kamati za siasa na matawi mengine ya chama za CCM itakuwa zinataka kuanzisha au kutekeleza. Zamani mchakato huo ulikuwa unafanyika bila ulazima wa kuwepo kwa maandishi kutoka kwenye baraza la wadhamini.

Hii inamaanisha kwamba, kwa sasa Baraza hilo la wadhamini litakuwa linaombwa idhini kwa maandishi na oganaizesheni nyingine za CCM ili miradi iweze kutekelezwa na baraza hilo pia litatoa majibu kwa maandishi kwa wote watakaoomba idhini

UCHAGUZI MKUU 2025 KWA ILANI MPYA

"Ndugu Wajumbe wa Mkutano Mkuu, mtakumbuka kwamba Mkutano Mkuu Maalumu wa tarehe 18- 19 Januari 2025 ulipokea taarifa ya Halmashauri Kuu ya CCM taifa, kuhusu utekelezaji wa kazi za chama na jumuiya zake kwa kipindi cha miaka miwili, 2022- 2024.

Lakini vilevile tulipokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 kwa kipindi cha miaka minne- mpaka mwaka jana uliofanywa na serikali zetu mbili, tulifanya marekebisho madogo ya katiba ya CCM ya mwaka 1977 na likawa toleo la 2025 na kumchagua Makamu Mwenyekiti wa CCM bara.

Vilevile mkutano ule kwa kuzingatia ibara ya 100 (2) na 101(5b) za Katiba ya CCM ya mwaka 1977 ulimaliza kazi ya kuteua ya kuteua mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na mgombea mwenza. Aidha ulimthibitisha mgombea wa Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi baada ya kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM"

"Mkutano Mkuu huu ni sehemu muhimu ya maandalizi muhimu ya chama chetu kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025, kama inavyoonekana kwenye ratiba ya mkutano huu, ajenda kuu tutakayojadili kuanzia leo: kuangalia yaliyomo kwenye ilani tunayokwenda kuinadi kwa wananchi katika uchaguzi ujao. Itakumbukwa kuwa katika kutimiza jukumu lake la kikatiba lililoanishwa chini ya Ibara ya 103 (4) ya Katiba ya CCM, Halmashauri Kuu ya CCM taifa katika kikao chake kilichofanyika Dodoma tarehe 10 Machi mwaka huu pamoja na mambo mengine ilipokea na kuthibitisha ilani ya uchaguzi ya CCM kwa mwaka huu, hivyo basi kesho tutafanya uzinduzi wa Ilani tutakayokwenda kuinadi kwa wananchi ili watupe imani na ridhaa ya kuturudisha kuendelea serikalini katika kipindi kingine cha miaka mitano"

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan





 
IMG_1283.jpeg
 
Wakuu, CCM wanafanya mkutano wao mkuu maalum leo na kesho (May 29-30) Dodoma, nadhani an wengine watafuatilia mahala walipo kwakuwa sehemu ni ndogo.

Nini kitajili leo, Gwajima hatimaye atavuliwa uanachama? Tutaona yatakayojiri.
Alshabab wangetusaidia kumaliza kazi leo katika eneo hilo, ingependeza sana
 
Wakuu, CCM wanafanya mkutano wao mkuu maalum leo na kesho (May 29-30) Dodoma, nadhani an wengine watafuatilia mahala walipo kwakuwa sehemu ni ndogo.

Nini kitajili leo, Gwajima hatimaye atavuliwa uanachama? Tutaona yatakayojiri.
Nitampigia kura Rais Dr Samia
 
Mikutano ya ccm haina mvuto tena.. Sio kwa wananchi tu bali hata kwao wenyewe.. Miaka ya nyuma ingekuwa sasa hivi ndio homa ya jiji
ni kweli, mkutano ungekuwa na shamrashamra nyingi, mji wa dodoma ungerindima na kupendezeshwa kwa rangi za kijani mitaani. Media zote zingeupa mkutano huo high coverage na attention kubwa
 
Ngoja kikosi kazi Cha ushindi kikapangwe. Kuna wanaojiaminisha wanaungwa mkono Kila Kona.
 
KILIO MAKATIBU WA CCM WILAYA YA MKURANGA.

Chama Makao Makuu, mtusaidie SISI makatibu wa CHAMA na Jumuiya zake wilaya ya Mkuranga. Tumechoka kutumika.

Mbunge wetu anatulazimisha kufanya mambo kinyume na utaratibu wa Chama Chetu ili kumtafutia kura.

Mara kadhaa amekua anatulazimisha Kuwaita wajumbe kutumia kivuli cha semina elekezi, kumfanyia kampeni (yeye au mkewe) na kuwatisha kua atawashughulikia wanaompinga kutumia mamlaka yake.

Sasa TAR_*EHE 03.06.2025, Ametulazimisha, kuwaita wajumbe wote wa kamati za Utekelezaji kaka zote 25 na matawi yote 247 ya wilaya ya Mkuranga, watakua wajumbe zaidi ya 5000*_, kwa ajili ya semina elekezi, zote zifanyike siku moja na kila jumuiya ktk ukumbi wao. Lengo Kuu ni kuwapa maelekezo wamchague yeye uchaguzi ujao wa 2025, na apate fursa ya kuongea nao na kuwapa pesa ili awashawishi wamchague tena.

Mafunzo gani ya watu zaidi ya 5000?

*Kama hiyo haitoshi amekua anatulazimisha kupeleka viongozi na wanachama wale anoahisi hawamuungi mkono takukuru*_. Hadi sasa tushapeleka zaidi na wanachama/viongozi wa Chama Chetu zaidi 50 takukuru, kinachofanyika huko ni kutishwa na kutakiwa wamuunge mkono mbunge uchaguzi ujao, kwani yeye kiongozi Mkubwa na atawashughulikia wale wote wasiomuunga mkono.

Hali hii inaleta MPASUKO NA CHUKI KWA CHAMA CHETU WILAYA MKURANGA.

Mtusaidie.
 

Attachments

  • IMG-20250529-WA0002.jpg
    IMG-20250529-WA0002.jpg
    33.4 KB · Views: 41
Back
Top Bottom