Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepokea wanachama wapya zaidi ya 70 kutoka Chama cha Wananchi (CUF), wakiongozwa na aliyekuwa mbunge wa Kilwa Kaskazini, Vedasto Ngombale.
Wanachama hao walipokelewa jana, Aprili 10, 2025, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kilwa Masoko, mkoani Lindi.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Katika hotuba yake, Makalla aliwapongeza kwa uamuzi wao wa kurejea CCM, na kuwataka viongozi wa chama katika ngazi ya wilaya na mkoa kuhakikisha wanawapatia kadi za uanachama, ili washiriki kikamilifu katika shughuli za chama.
"Tumewapokea hapa, aliyekuwa mbunge, ndugu yangu, amerudi CCM na wenzake. Awali walikuwa 70, lakini sasa wameongezeka na kuwa zaidi ya 70. Ninawaelekeza Katibu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa kutengeneza utaratibu wa kuwapatia kadi hawa wanachama wapya," alisema Makalla.
Makalla aliongeza kuwa baadhi ya wanachama hao walikabidhi pia mihuri ya ofisi zao za CUF, ishara kuwa wamefunga rasmi shughuli zao katika chama hicho na kujiunga na CCM.
Vedasto Ngombale alihudumu kama mbunge wa Kilwa Kaskazini kupitia CUF kati ya mwaka 2015 hadi 2020.