CCM yashangazwa na urasimu wa mifumo kutumika kama utetezi wa miradi ya maendeleo kutotekelezwa kwa wakati

CCM yashangazwa na urasimu wa mifumo kutumika kama utetezi wa miradi ya maendeleo kutotekelezwa kwa wakati

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ameonesha kukerwa kwake na tabia ya fedha ya miradi ya maendeleo kucheleweshwa kwa kisingizio cha urasimu wa mifumo ya ulipaji kutofunguka kwa muda mrefu jambo ambalo linakwamisha baadhi ya miradi utekelezaji wake kuenda kwa kasi na haraka kama inavyopangwa.

Hiyo ni baada ya kuelezwa kuwa kuna mradi wa maji kijiji cha Mwongozo wilaya ya Kaliua mkoa wa Tabora, umechelewa kutokana na mfumo wa ulipaji kuwa na matatizo ambapo kwa zaidi ya miezi mitatu wameshindwa eti kufanya malipo kwa kisingizio cha mfumo kutofunguliwa.

Shaka amesema haiwezekani mfumo huo kutofanyakazi kwa zaidi mwezi mzima jambo ambalo amesema inatumika kama kichaka cha kuficha uzembe wa baadhi ya watendaji wasimamizi na wakandarasi watekelezaji huku wananchi wakisubiri huduma hizo za kijamii kwa muda mrefu.

“Mimi siamini..tutafuatilia kujua kama kweli mfumo huo umeshindwa kufanyakazi kwa zaidi ya mwezi mzima, Rais Samia anapotoa gedha za miradi alishasema anataka kuoneka fedha zinatumika katika muda husika, tusikwamishe miradi kwa kisingizi za urasimu katika mifumo, hili tutaliguatilia kwa akaribu tujiridhishe haiwezekani” alisema Shaka

 
Mfumo haujafunguka kote. Ndio tatizo la Kiongozi kutokua na uzoefu kwenye utumishi wa Umma
 
Back
Top Bottom