Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,773
- 1,174
TANGAZO KWA UMMA
Chama Cha Mapinduzi kinawatangazia Wanachama wake kwamba, mchakato wa ndani ya Chama wa uteuzi wa wagombea nafasi za Ubunge, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi na Udiwani, kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, utazanza rasmi tarehe 1 Mei, 2025 kwa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za maombi ya kuteuliwa kugombea nafasi hizo. Zoezi hilo litaanza tarehe 1 Mei, 2025, saa 2:00 asubuhi na kumalizika tarehe 15 Mei, 2025, saa 10:00 jioni. Utaratibu wa kuchukua na kurejesha fomu za maombi utakuwa kama ifuatavyo:
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
a) Wanachama wanaogombea nafasi ya Ubunge au Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi watachukua na kurudisha fomu kwa Katibu wa CCM wa Wilaya inayohusika.
b) Wanachama wanaogombea nafasi za Viti Maalumu vya wanawake katika Bunge au Baraza la Wawakilishi, kupitia kundi la UWT pamoja na makundi maalumu (NGOs, WAFANYAKAZI, WASOMI na WALEMAVU) watachukua fomu na kurudisha kwa Katibu wa UWT wa Mkoa unaohusika.
c) Wanachama wanaogombea nafasi za Viti Maalumu vya wanawake katika Bunge au Baraza la Wawakilishi kupitia jumuiya ya UVCCM watachukua na kurudisha fomu kwa Katibu wa UVCCM Mkoa unaohusika.
d) Wanachama wanaogombea nafasi za Viti Maalumu vya wanawake katika Bunge au Baraza la Wawakilishi kupitia jumuiya ya WAZAZI watachukua na kurudisha fomu kwa Katibu wa WAZAZI Mkoa unaohusika.
e) Wanachama wanaogombea nafasi ya Diwani wa Kata (Bara) au Wadi (Zanzibar) watachukua na kurudisha fomu kwa Katibu wa CCM wa Kata/Wadi inayohusika.
f) Wanachama wanaogombea nafasi ya Udiwani Viti Maalumu vya Wanawake watachukua na kurudisha fomu kwa Katibu wa UWT wa Wilaya inayohusika.