CCM yatoa wiki moja Walimu wote wapate vishikwambi

Na Mwandishi Wetu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa wiki moja kwa Wizara ya Elimu na TAMISEMI kuanzia leo Januari 20, 2023, kuhakikisha vishikwambi vilivyotolewa na serikali kwa ajili ya walimu vinawafikia walengwa.

CCM Imesema imepokea malalamiko ya kutotekelezwa kikamilifu kwa maelekezo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu ugawaji wa vishikwambi hivyo.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Edward Mjema, alisema wakati akizundua ugawaji wa vishikwambi hivyo Novemba mwaka jana, Waziri Mkuu Majaliwa aliagiza kuhakikisha vifaa hivyo vinakwenda kwa walengwa.

"Ulitengwa muda maalumu wa kutolewa kwa vishikwambi hivyo ambao ulikuwa unaishia Januari 15, mwaka huu, lakini Chama kimepokea malalamiko kwamba hadi leo kuna baadhi ya makundi hayajapata hivyo vishikwambi. Lakini pia kuna baadhi ya wilaya hawajagawa kabisa vishikwambi hivyo.

"Kuna maeneo mengine unakuta walimu wako 10 na wote wanahitaji na wanastahili kupata, lakini unakuta vishikwambi vinatoka vinane wawili wanaachwa.

"Chama kinatoa maelekezo, kinaielekeza wizara husika (Wizara ya Elimu na TAMISEMI) kuhakikisha zoezi hili linakamilika na walengwa wote wanaostahili kuhakikisha wamevipata vishikwambi hivyo, lakini sio hivyo tu bali pia wahakikishe malalamiko haya hayapo na wasimamie zoezi kuona makundi yaliyopaswa kupewa yanafikiwa na wale ambao hawajapata wapate. Baada ya wiki moja tupate taarifa zoezi hili limekwendaje," amesema.

====View attachment 2488865View attachment 2488866

Wakapige kwanza rangi majengo waliyopara kutoka mfumo wa chama kimoja cha siasa.
 
Ila nchi hii Kuna maigizo,waziri mkuu alisema vinatosha huku halmashauri wametuletea vishikwabi sita na tuko walimu 12.Hapa unajiuliza nani mkweli na nani muongo.Tuseme halmashauri wameuza vishimbi vyetu?au waziri mkuu ametupiga fix kama enzi zile"magufuli Yuko ofisini anatusalimia" kumbe anapumulia mashine.
Hata hivyo hatuna shida kivileee mana hata bila vishikwabi tupo na Jf yetu na tunakula matunda kimasihara.
Wilaya ya bahi dom walimu wote na wataalamu wa maabara wote wamepata vishkwambi......!! Halmashaur nyngne wamevipiga hivyo
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa wiki moja kwa Wizara ya Elimu kuanzia leo Januari 20, 2023 kuhakikisha vishikwambi vilivyotolewa na serikali kwa ajili ya walimu vinawafikia walengwa.

CCM imesema imepokea malalamiko ya kutotekelezwa kikamilifu kwa maelekezo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu ugawaji wa vishikwambi hivyo.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema, alisema wakati akizundua ugawaji wa vishikwambi hivyo Novemba mwaka jana, Waziri Mkuu Majaliwa aliagiza kuhakikisha vifaa hivyo vinakwenda kwa walengwa.

"Ulitengwa muda maalumu wa kutolewa kwa vishikwambi hivi ambao ulikuwa unaishia Januari 15, mwaka huu, lakini Chama kimepokea malalamiko kwamba hadi leo kuna baadhi ya makundi hayajapata hivyo vishikwambi. Lakini pia kuna baadhi ya wilaya hawajagawa kabisa vishikwambi hivyo.

"Kuna maeneo mengine unakuta walimu wako 10 na wote wanahitaji na wanastahili kupata, lakini unakuta vishikwambi vinatoka vinane wawili wanaachwa.

"Chama kinatoa maelekezo, kinaielekeza wizara husika (Wizara ya Elimu) kuhakikisha zoezi hili linakamilika na walengwa wote wanaostahili kuhakikisha wameipata vishikwambi hivyo, lakini so hivyo tu bali pia wahakikishe malalamiko haya hayapo na wasimamie zoezi kuona makundi yaliyopaswa kupewa yanafikiwa na wale ambao hawajapata wapate. Baada ya wiki moja tupate taarifa zoezi hili limekwendaje," amesema.

Mjema alisema kutolewa kwa vishikwambi hivyo ni mwendelezo wa jitihada za serikali kuwawezesha na kuwajengea uwezo walimu kuwa na vitendea kazi na kuimarisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Katika kuendelea kuwawezesha walimu kuwa na vitendea kazi na kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji Septemba 15, mwaka jana kwamba vishkwambi vilivyotumika wakati wa sensa ya watu na makazi Agosti 23, mwaka 2022 vitatagawiwa kwa walimu wote baada ya shughuli hiyo kumalizika.

Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Juma Kipanga alisema jumla ya vishikwambi vilivyotumika wakati wa sensa ya watu na makazi 6,600 kwa upande wa Zanzibar na 293,400 Tanzania Bara.

Aidha, alisema wizara hiyo imeongeza vishikwambi zaidi ya laki moja hivyo kufanya idadi hiyo kutosheleza.

Walengwa na ugawaji huo ni walimu wote, baraza la mitihani, wadhibiti ubora, wakufunzi wa vyuo vya ualimu, vyuo vya maendeleo ya jamii na vyuo vya ufundi pamoja na waratibu elimu kata na maafisa elimu wilaya na mkoa.
View attachment 2488850
Tayari naye kaanza maigizo !
 
Ndo maana wapinzani huwa wakilalamika wanasema serikali ya CCM, ko ndo chama chenye mamlaka juu ya serikali
 
Huyu mama kumbe bado mrembo namna hii.

Then sikujua kama chama kinaweza kuielekeza serikali iteteleze maagizo.

Kama inawezekana waielekeze serikali iache kununua magari ya kifahari ili pesa zitumike kwenye miradi ya maendeleo kwa faida ya watanzania wote.

Alafu hapo anamuelekeza mwenye kiti au nani.
Sababu mwenyekiti ndio anaesimamia serikali.
 
Back
Top Bottom