Zanzibar 2020 CCM Zanzibar yakaribisha wanaccm kuchukua fomu za Urais, yasema uteuzi utafanyika Dodoma siyo Unguja

Zanzibar 2020 CCM Zanzibar yakaribisha wanaccm kuchukua fomu za Urais, yasema uteuzi utafanyika Dodoma siyo Unguja

Histori kutoka maktaba online namna CCM Zanzibar wanavyotia nia na aina ya wagombea kisiasa
Friday, July 9, 2010
Hukumu urais Zanzibar leo

ILE siku ya hukumu kwa wanachama 11 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaowania uteuzi wa kugombea urais wa Zanzibar, imetimia.

Leo Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya Taifa pamoja na Halmashauri Kuu (NEC) vinakutana hapa kufanya uteuzi na kisha kupiga kura ya kuchagua mgombea huyo miongoni mwa 11 waliojitokeza.

Awali, Kamati Kuu ilikuwa ikutane jana, lakini sasa itakutana leo kwanza kabla ya kupeleka majina au jina la mgombea mmoja kupigiwa kura NEC.

Tayari Dodoma imepambwa na rangi za kijani na njano zinazotumiwa na chama hicho tawala, huku kambi mbalimbali zikiwamba ngoma upande wao, katika mbio za nani atasimamishwa na CCM kuwania kumrithi Rais Amani Abeid Karume.

Wanachama 11 wamejitokeza kuwania nafasi hiyo wakiwamo vigogo kadhaa ambao ni Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein, Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, Naibu wake ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Ali Juma Shamuhuna na Waziri Kiongozi mstaafu Dk. Mohamed Gharib Bilal.

Pia wamo mawaziri Haroun Ali Suleiman, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mohammed Aboud, Mohammed Yussuf Mshamba, Balozi Ali Abeid Karume, Hamad Bakari Mshindo, Mohammed Raza na Omar Sheha Mussa.

Miongoni mwao, Dk. Shein, Nahodha na Dk. Bilal wanapewa nafasi kubwa ya kuteuliwa na CCM leo kusimama dhidi ya Maalim Seif Sharrif Hamad wa CUF katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 31 mwaka huu.

Dk. Shein anaelezwa kuwa mwanasiasa mwenye kufuata siasa za ustaarabu, muungwana na anayetenda kazi zake bila kuwa na makundi na anatazamiwa kuwa kiungo kikubwa kati ya Pemba na Unguja, hasa baada ya maridhiano ya kisiasa visiwani.

Hata hivyo, tangu ajitose kuwania uteuzi huo, amekuwa akiandamwa na ‘makombora’ kutoka kwa baadhi ya wapinzani wake, waliofikia hatua ya kumwaga vipeperushi Unguja wakimtuhumu kwa mambo kadhaa.

Hata jana jioni, uvumi ulikuwa unaenezwa mjini hapa kuwa Dk. Shein alikuwa ameandika barua ya kujitoa na kuelekeza nguvu zake kumsaidia Nahodha.

Lakini wanaomtetea wanaamini hali hiyo imefanyika kwa sababu mgombea huyo ni tishio miongoni mwa wenzake na ana nafasi kubwa ya kuibuka mshindi leo.

Baadhi ya wasaidizi wa Dk. Shein walithibitisha kuenezwa kwa uvumi wa kujitoa tangu juzi, lakini akaeleza kuwa habari hizo hazikuwa na ukweli wowote.

Mwingine ni Nahodha ambaye kwa umri wake wa miaka 48, anaonekana kuwa chaguo la vijana, kama ambavyo mwenyewe amesema anataka kuleta mabadiliko Zanzibar na kuifanya kuwa kama Dubai.

Huyu naye anaonekana kuwa miongoni mwa wagombea wenye nguvu katika kumrithi Rais Karume na kwa turufu yake ya ujana, na pengine kuwa kwake karibu kama msaidizi wa Rais, ni karata yake nyingine.

Dk. Bilal ambaye aliwahi kuwa Waziri Kiongozi chini ya Dk. Salmin Amour Juma ‘Komandoo,’ ni mgombea mwingine mwenye nguvu miongoni mwa waliojitokeza.

Alijaribu bila mafanikio kutaka kumrithi Komandoo na akabwagwa na Karume na akajaribu tena mwaka 2005 bila mafanikio, lakini tangu wakati huo, ndoto za kutaka kuwa rais wa Zanzibar hazijafutika kwake.

Alitajwa kuwa mtu wa karibu wa Dk. Salmin, lakini yamekuwapo madai mapya hapa na Zanzibar, kuwa wawili hao sasa hawako pamoja katika mbio za mwaka huu za kuingia Ikulu.

Dk. Salmin alitua hapa juzi akifuatana na Nahodha na haijawekwa bayana kama turufu yake ni kwa mwanasiasa huyo kijana, lakini uwepo wake katika vikao hivi viwili vya leo, ni ishara kuwa amekuja na siri moyoni.

Wagombea wengine wanane waliosalia katika kinyang’anyiro hicho, hawapewi nafasi kubwa ya kuteuliwa, kwa sababu mbalimbali, ingawa katika siasa, lolote linaweza kutokea.

Chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, vikao hivyo vinatarajiwa hadi kufikia majira ya jioni leo, vitakuwa vimetoa jina la mgombea na la mgombea mwenza wa Jamhuri ya Muungano.

Rais Kikwete ndiye mgombea pekee wa CCM katika urais wa Muungano na kwa mujibu wa Katiba ya Chama hicho, atapigiwa kura katika Mkutano Mkuu utakaofanyika kwa siku mbili kuanzia kesho.

Katika suala la mgombea mwenza, bado ni siri kubwa kwa Rais Kikwete mwenyewe, ingawa yamekuwapo majina kadhaa yanayotajwa kwa nafasi hiyo.

Majina ya wanasiasa kama Zakia Meghji, Dk. Salim Ahmed Salim, Muhammed Seif Khatib na hata Dk. Shein na Nahodha, yamehusishwa na nafasi hiyo, ingawa ukweli wa mambo utakuwa hadharani majira yoyote leo.

Katika maandalizi ya vikao hivyo, Rais Kikwete jana alitembelea Kizota ambako Mkutano Mkuu utafanyika kesho na keshokutwa, na maandalizi yalikuwa yanaelekea hatua za mwisho kukamilika.

Rais Kikwete alitembelea eneo hilo muda mfupi baada ya kutua mjini hapa na alikuwa Kizota na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba na watendaji wengine wa CCM na Serikali
 
CCM Zanzibar imesema ni ruksa kwa wanaccm wanaotamani urais wa Zanzibar kwenda kuchukua fomu.

Naibu Katibu mkuu wa CCM Zanzibar amesema uteuzi wa jina la mgombea utafanyika jijini Dodoma na siyo Zanzibar na kisha litapelekwa Tume ya uchaguzi.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Kweli zenji ni kamkoa ka tanganyika
Bisha kwa hoja!
 
Juni 10, 2020
Othman Masoud: Historia ya Zanzibar yathibitisha ghiliba za uchaguzi huleta machafuko - Part 2


Aliyekuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amekumbusha kuwa historia ya Zanzibar imejaa ushahidi unaothibitisha kwamba wanaotumia ghiliba na hila kwenye chaguzi husababisha maafa makubwa na wanaotumia ushawishi hufanikiwa kwenye kisanduku cha kura.

Zanzibar ilikuwa Empire kubwa na empire ina maana hakuna ambaye hakuwepo ni mchanganyiko wa wengi hivyo hakuna mgeni na ndiyo sifa ya Empire kuwa na kusanyiko la watu toka sehemu mbalimbali.

Source : Weyani TV
 
Juni 8, 2020
Othman Masoud: Zanzibar haikuanza 1964 - Part 1

Othman Masoud Othman anarejelea umuhimu wa historia na kutupeleka kwa muasisi wa mapinduzi ktk nchi za Latin Amerika, Simon Bolivar Simon Bolivar and the Spanish-American revolutions .

Nini maana ya uchaguzi ? Shujaa wa latin Amerika aliyeshiriki kuleta mapinduzi katika nchi 6 za Latin Amerika ikiwemo Bolivia na Venezuela alitoa hotuba murua mwaka 1819 mwezi February tarehe 15... ktk Bunge la Venezuela....

Othman Masoud Othman aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya SMZ , amesema kwamba ni makosa kudhani kwamba Zanzibar ilianza mwaka 1964 baada ya Mapinduzi au 1995 baada ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi na kwamba jambo ambalo haliwezi kuepukika muda wote ni mabadiliko. Msikilize kwenye sehemu hii ya kwanza ukijitarisha kwa ajili ya sehemu ya pili ya mazungumzo aliyofanya na Radio Noor ya Mjini Unguja.

source : weyani TV
 
11 Feb 2020
Zanzibar, Tanzania

Wasiotimiza Miaka 2 Kwenye Vyama Vyao
Mwakilishi, Mwanasheria wapambana Zanzibar kwa hoja


Hamza Hassan Juma, mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar anayetaka sheria ibadilishwe kuwazuwia wanachama wasiotimiza miaka miwili kwenye vyama vyao kuwania chaguzi za serikali, anajadiliana na Omar Said Shaaban, mwanasheria anayepinga pendekezo hilo, kwenye kituo cha redio cha Zenj FM. Sikiliza mjadala mkali baina yao.

Source : Weyani TV
 
Nchi ina vituko urais wa Zanzibar form zinapatikana Tanganyika.


Sio kweli Fomu zitachukuliwa Afisi Kuu ya CCM hukuUnguja , Zanzibar


IMG_9eio0b.jpg
 
wazanzibar ipo siku mtakuja kujikomboa.
ni swala la kujipanga na kuwa kitu kimoja.
NI WAZI MNACHAGULIWA RAIS KUTOKA DODOMA.
 
rais wa zanzibar kabla haja pewa urais anakuja kwanza huku bara.
WANA MJAZA SUMUUUU.
alafu ndo wanampeleka huko
Nimeelewa kuwa mwana CCM anayehusudu hoja za upinzani au aliyetayari kufanya kazi na upinzani hawezi kupitishwa kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM kuongoza serikali ya nchi ya Zanzibar.
 
June 15, 2020
Unguja Zanzibar
Tanzania
Balozi Ali Karume achukuwa fomu
Ali Abeid Amani Karume



Balozi Ali Karume amekuwa wa pili kujitokeza kuchukuwa fomu ya kuwania kugombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM). Bakari Juma amekuwa mwanachama wa kwanza wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuchukua fomu ya kugombea urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka huu. Rais Dkt. Ali Mohammed Shein ataondoka madarakani baada ya kuongoza kwa vipindi viwili (miaka 10) kwa mujibu wa katiba.
Source : Global TV Online
 
June 15, 2020
Toka Afisi Kuu Kisiwandui
Unguja, Zanzibar


Mbio za kugombea kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi kugombea Urais Zanzibar zimeanza rasmi leo asubuhi. Katibu wa kamati maalum ya NEC Zanzibar Idara ya Organization Galos Nyibo amemkabidhi fomu Mbwana Bakari Juma, mgombea wa kwanza aliyefungua ungwe ya wagombea Urais Zanzibar. "Urais unahitaji moyo wa kujitolea, Urais ni maisha ya watu, nitaanzia pale ambapo atakapoishia Mhe. Rais Ali Mohamed Shein" Mbwana Bakari Juma - Mgombea Urais Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

MBIO ZA URAIS WA ZANZIBAR: MBWANA ATAJA VIPAUMBELE VYAKE
Posted by Chumba-cha-Habari | Jun 15, 2020
Mbio za Urais wa Zanzibar: Mbwana ataja vipaumbele vyake

Baada ya Chama cha Mapinduzi Zanzibar kufungua milango kwa wanachama wake wanaotaka kuwania nafasi ya Urais kupitia Chama hicho, Mbwana Bakari Juma amekuwa wa kwanza kujitokeza na kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar.
Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo Afisi Kuu Kisiwandui amesema amejitathimini na kuona kuwa anafaa kukalia kiti cha Urais wa Zanzibar.
Akitaja mambo ambayo atayafanyia kazi iwapo atafanikiwa kupata kiti hicho ni kuhakikisha Zanzibar inakuwa kitovu cha biashara, kupiga vita umaskini, maradhi pamoja na ujinga.
Aidha mgombea huyo amesema atadumisha muungano na kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kama inavofanywa na na viongozi waliotangulia.
Mbwana ametokea mkoa wa Kaskazini Unguja na amezaliwa katika kijiji cha Kikwajuni.

Source: Mbio za Urais wa Zanzibar: Mbwana ataja vipaumbele vyake
 
Wanaodhaniwa kuweza kutia nia Urais Zanzibar tiketi ya CCM

April 17, 2020

Shamsi Vuai Nahodha : isingekua muungano, Zanzibar tungevurugana tu

Mbunge wa Jimbo la Kijitoupele na Waziri Kiongozi wa Zamani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha amesema kama sio Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hivi sasa wangekua wanavurugana kwa migogoro ya ardhi kwani arfhi iliyopo haiwiani na idadi ya watu hivyo amewasihi Wazanzibari kutumia vyema fursa hiyo.

updates 18 Juni 2020
SHAMSI VUAI NAHODHA ACHUKUA FOMU YA URAIS, ATOA AHADI MAMBO 3 MAZITO

 
Why Dodoma? Kuna mjumbe mmoja wa Balaza mapinduzi alishawahi kusema wajumbe wakishavuka maji tu kufika Dodoma sijui hupatwa na kitu gani....

Wanabadilika kabisa hata kama walikuwa na msimamo wa pamoja kabla ya kuondoka Zanzibar
 
Toka maktaba

Shamsi Vuai Nahodha katika majadiliano ya kisomi na Prof. Anna Tibaijuka kuhusu Tanzania na Zanzibar
 
June 15 2020

ZANZIBAR KUMEKUCHA SASA MBIO ZA UCHAGUZI MKUU "TAHADHARI ZATOLEWA"

Watia nia wasibebwe, kufanya, kufanyiwa kampeni kabla ya teuzi ndani ya CCM muda bado maana ni katazo kubwa ndani ya CCM Mpya chini ya Mwenyekiti John Pombe Joseph Magufuli na Makamu Mwenyekiti Ali Mohamed Shein kipenzi cha wanaCCM waZanzibari
Source : KTV TZ online
 
Back
Top Bottom