LGE2024 CCTV Camera kwenye chumba cha kupiga kura

LGE2024 CCTV Camera kwenye chumba cha kupiga kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Allency

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2011
Posts
14,830
Reaction score
14,472
Moja moja kwa mada:

Ili kuondoa haya malalamiko ya wagombea wa CCM kuanzisha vurugu na kuwasingizia wapinzani ili watolewe nje na Police then wao wanabadilisha matokeo then mawakala wanarudishwa ndani kuhesabu, pamoja na hujumu zingine kama kwenda kula chakula ndani watu wanafanya yao.

Kwanini kila kituo cha kupigia kura pasiwekwe CCTV camera na iwe ina record kila kitu kwenye local server pamoja na kuonyesha kwenye simu ya kila mgombea ili kama ikitokea shida kwenye local server basi kila mgombea anabaki na CCTV footage copy yake.

Kwanza ni nafuu maana huitaji internet zaidi ya network tu. Hili litapunguza hujumua kwa kiasi kikubwa.

Je, kwa sheria za uchaguzi zetu zilivyo na makandokando wanaweza ruhusu hili?

Pia niwaulize wadau hili linaweza kusaidia kupunguza hujumu zinazofanyika?

Asanteni

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - NEC: CCTV zifungwe kuepusha wizi wa kura
 
Tofauti ni nn hapo mm najua cctv huwa zinaitaĵiii bundles
Swali la lilikua utafauti wa network na internet.
Kitendo Cha wewe kuunganisha server zako na simu yako au computer na vifaa vingine hiyo ni Network.
 
Tofauti ni nn hapo mm najua cctv huwa zinaitaĵiii bundles
Hapana mkuu, huitaji bundle ni network (LAN) tu na siyo internet sasa wewe kama mgombea kupitia simu yako utaweza kurekodi na kuitunza hiyo footage in case watu wakifanya yao na server ya Nec
 
Alipopigwa risasi Lissu hizo camera zilikuwepo ila zikang'olewa
Hapa nitoe elimu kidogo. Kwa ishu ya Lissu ni kuwa only server ya pale ndiyo ilikuwa na record lakini kwa hii kila mgombea anakuwa na record ya kila kinachofanyika ndani ten live na siyo kuja kuona baadae.
 
Alipopigwa risasi Lissu hizo camera zilikuwepo ila zikang'olewa
Kwa lugha rahisi ni kama video conference kati ya kinachoendelea ndani na wewe mgombea sema mgombea anakuwa observer huku ana record matukio. Na ni kupitia network na siyo Internet so hakuna gharama zozote zaid ya CCTV camera na server tu, simu itakuwa gharama ya mgombea, connection ni wireless.
 
Yani Unataka CCM washindwe? Watavaa mambomu nchi nzima hakutakaliaka. Unajua hata majambazi huenda misikitini na makanisani, na nyuso, lakini hakuna jambazi linalokiri kutenda ujambazi popote, mpaka likamatwe.
 
Sijui tunakwama wapi kuhusu hili, binafsi hili wazo nimelipata leo jioni while it's too late, lakini kwa chaguzi zijazo tunaweza kwenda na hili wazo na mimi niko tayari kufanya demo juu ya hili. Hata kama ikibidi records zote ziende central serve pia inawezekana lakini kwa mgombea hapa lazima abaki na copy yake. Kwenda central server ndiyo internet itahitajika kutuma central server lakini wagombea wao watakuwa safe na central database baadae wanaweza kuja kwenye local server wakaichukua copy yao kama walipata changamoto ya internet. Samahanini kama lugha imekuwa ngumu. Unaweza uliza kama kuna kitu hujaelewa
 
Kwa lugha rahisi ni kama video conference kati ya kinachoendelea ndani na wewe mgombea sema mgombea anakuwa observer huku ana record matukio. Na ni kupitia network na siyo Internet so hakuna gharama zozote zaid ya CCTV camera na server tu, simu itakuwa gharama ya mgombea, connection ni wireless.
Hebu endelea kutoa elimu hapo mkuu! Sasa kwa mbunge itakuwaje maana ndani ya jimbo ana vituo vingi vya kupigia kura ataweza vipi kufuatilia matukio kwenye vituo vingine?
 
Back
Top Bottom