Cctv video: Huyu mwizi inasemekana kawaliza wafanya biashara wengi kariakoo ila za mwizi 40 kanasa,

Mbona anaiba kiboya na hao jamaa wa dukani mbona nao wanaibiwa kiboya sana? Mbona kama wana act movie?
 
Itakua hufuatilii channel za ci id,hao mbwa wanauwana daily na matukio ya kutosha
 
Tena kuna sharia ya kukatwa mkono kabisa
Sharia ya mwizi kukatwa mkono ipo, pia kukatwa mkono na mguu, pia kuuliwa.

Lakini zote hizo zina namna yake, siyo mtu anakatwa tu.


Uislam ni mwema sana. Usome kijana.
 
Zilitakiwa cctv ziwekwe kote kwenye traffic lights
 
Sharia ya mwizi kukatwa mkono ipo, pia kukatwa mkono na mguu, pia kuuliwa.
Lakini zote hizo zina namna yake, siyo mtu anakatwa tu.
Asante kwa ufafanuzi. Je, kutembea na mke au mume wa mtu, inahesabika pia kuwa ni wizi?
 
Hao wanaionea Kariakoo hatuuwi wezi. Akaibe Kwengine kama hajafungwa tairi huyo.
Sijui unaizungumzia Kariakoo gani ila Kariakoo ninayoijua mimi miaka ya ya nyuma 2008 kurudi nyuma vibaka walikuwa wanapigwa moto kama mishikaki.

Nilishawahi kushuhudia mmoja anachomwa pale mtaa wa Sukuma na Mafia karibu na kwa mpiga zumari mwenzako Maulid Kitenge,Kariakoo pamekuwa pakistaarabu baada ya kuwa na mchanganyiko wa makabila mengi ya watu wasioendeshwa na mihemko ila Kariakoo ya Wazaramo na Wandengereko ilikuwa mwizi hafikishwi polisi mzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…