CDF mstaafu Mabeyo amelikoroga, Makamu wa Rais ndiye alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kila hatua kujua afya ya Rais

CDF mstaafu Mabeyo amelikoroga, Makamu wa Rais ndiye alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kila hatua kujua afya ya Rais

Wabongo bwana ujuaji mwingi Sana

Hivi unadhania mpaka mtu anakuwa CDF ni Jambo simple simple Sana eh

So wewe unajua utaratibu kuliko mkuu wa majeshi?

Tuache kujifanya wajuaji sana
Ujuaji si kosa kama unachojua ni sahihi na umekipata kwa juhudi zako binafsi..cheo, hadhi au Mali havimfanyi mtu kujua lolote kama yeye mwenyewe hana bidii ya kutaka kujua!
 
Sio kila mtu anaweza kuhandle taarifa za msiba wa mtu

Na Kwa tamaduni za kiafrica wanaume kwanza ndio wanapeana taarifa

Haijalishi huyo mwanamke ana cheo gani, but cha kwanza wanaume lazima wakutane wapange mambo yatakuwaje

So mabeyo Yuko sahihi kabisa
Katiba ndio inasema hivyo?
 
1. Aliyestahili kumpatia taarifa Makamo wa Rais juu ya kifo cha Rais Magufuli ni daktari wa Rais.
2. CDF Mabeyo alikuwa mkuu wa majeshi ndiyo, yeye pamoja na viongozi wengine wa vyombo vya usalama walitakiwa pia kupatiwa taarifa na Makamo wa Rais (Baada ya yeye kuwa mtu wa kwanza kabisa kufahamishwa) ili kuhakikisha tu usalama wa nchi upo vizuri.

3. Makamo wa Rais ndiye alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kila hatua kujua afya ya Rais inaendeleaje.

4. CDF anachukua majukumu ya kuwa msaidizi mkuu wa Rais na mtoa taarifa kwa Makamo kuwa Rais amefariki (Kosa kubwa) mbaya zaidi Makamo wa Rais anakuwa mtu wa nne kuambiwa baada ya Waziri mkuu, CS na Taasisi ya kiswahili (Baada ya kujadili mpaka cheo cha Amiri jeshi mkuu)

Kosa ni la nani? Hayati Magufuli kujiundia kikundi chake cha siri kwa mambo yao huku wakimuondoa Makamo? Wasaidizi wake wakati Rais ni mgonjwa? Makamo wa Rais yupo Tanga anaongea kawaida tu huku Rais yupo kitandani akipigania uhai na wala hajulishwi hadi umauti tena masaa manne mbele baada ya mijadala ambayo kimsingi watu hawaijui katiba. Inafikirisha.

Sishangai kuona daktari binafsi wa hayati Rais Magufuli Prof. Mabula Mchembe kupotea ulingoni baada ya Samia kuwa Rais? Hivi yuko wapi huyu mtu?
Nadhani kwa kiasi kikubwa mtazamo wako upo sahihi. Umesahau tu kujumuisha nafasi ya Bunge na Mahakama.

Ninachoona hapa ni mgongano wa mitazamo inayoegemea nadharia vs mazingira halisi.

Tujiulize, nani aliwakataza hao tunaoamini kuwa walistahili kushika hatamu wasishike hatamu! kwa nini nao walibaki kuwa wananchi!

Mazingira halisi ni kuwa Mkuu wa Serikali na Mkuu wa nchi anapokuwa katika hatari kubwa au nchi inapokuwa katika hatari kuingia au kuingizwa katika failed state kuna watu wanashika usukanai kwa ridhaa ya Mkuu mwenyewe au bila ridhaa yake regardless ya mwongozo wa kikatiba. Na mara nyingine hiyo ndio inakuwa mwisho wa katiba na desturi zilizokuwepo.

Ukimsikiliza kwa makini na ukatafakari kwa utulivu utaona kuwa the three giant ndio walishika usukani katika kipindi mhusika alipopoteza uwezo wa kuongoza hadi siku mbili baada ya kuondoka. wengine walikuwa wasikilizaji na wafuata maagizo. Lakini kubwa zaidi kulikuwa na sintofahamu kadhaa ndio maana mambo hayakwenda pengine vile wengi wangetarajia. Hizo sintofahamu hajaziweka wazi na pengine hazitokuja kuwa wazi kamwe. watabaki watu wachache wanaojua ni kilitokea, chanzo kilikuwa nini na waanzilishi wamechukuliwa hatua gani?

Pengine hao ambao wewe unahisi walipaswa kushika usukanai wangepewa fursa, pengine mambo yasingekuwa hivi yalivyo.

Hao ndugu watatu waliotuvusha wanastahili pongezi za hali ya juu sana, walizishinda nafsi na kuweka maslahi ya Tz mbele. Wangekuwa na tamaa au wangetetereka sijui tz ingekuwa ya namna gani hadi sasa.

Nahisi hao Giants huwa ni muhimu sana wakati wa uchaguzi mkuu hususan inapofika saa moja jioni baada mchakato wa kupiga kura kukamilika hadi saa ya kutangaza matokeo. Katika kipindi hicho hao watatu wasipokuwa na wewe imekula kwako. Ndugu yetu Lungu na Yule aliyepo Nyasa wanajua role ya hao watatu katika nyakati hizo.
 
Sio kila mtu anaweza kuhandle taarifa za msiba wa mtu

Na Kwa tamaduni za kiafrica wanaume kwanza ndio wanapeana taarifa

Haijalishi huyo mwanamke ana cheo gani, but cha kwanza wanaume lazima wakutane wapange mambo yatakuwaje

So mabeyo Yuko sahihi kabisa
Hizi dharau zenu ndio zilimponza mwendazake
 
1. Aliyestahili kumpatia taarifa Makamo wa Rais juu ya kifo cha Rais Magufuli ni daktari wa Rais.
2. CDF Mabeyo alikuwa mkuu wa majeshi ndiyo, yeye pamoja na viongozi wengine wa vyombo vya usalama walitakiwa pia kupatiwa taarifa na Makamo wa Rais (Baada ya yeye kuwa mtu wa kwanza kabisa kufahamishwa) ili kuhakikisha tu usalama wa nchi upo vizuri.

3. Makamo wa Rais ndiye alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kila hatua kujua afya ya Rais inaendeleaje.

4. CDF anachukua majukumu ya kuwa msaidizi mkuu wa Rais na mtoa taarifa kwa Makamo kuwa Rais amefariki (Kosa kubwa) mbaya zaidi Makamo wa Rais anakuwa mtu wa nne kuambiwa baada ya Waziri mkuu, CS na Taasisi ya kiswahili (Baada ya kujadili mpaka cheo cha Amiri jeshi mkuu)

Kosa ni la nani? Hayati Magufuli kujiundia kikundi chake cha siri kwa mambo yao huku wakimuondoa Makamo? Wasaidizi wake wakati Rais ni mgonjwa? Makamo wa Rais yupo Tanga anaongea kawaida tu huku Rais yupo kitandani akipigania uhai na wala hajulishwi hadi umauti tena masaa manne mbele baada ya mijadala ambayo kimsingi watu hawaijui katiba. Inafikirisha.

Sishangai kuona daktari binafsi wa hayati Rais Magufuli Prof. Mabula Mchembe kupotea ulingoni baada ya Samia kuwa Rais? Hivi yuko wapi huyu mtu?
Huna unalolijua wewe, swala la afya ya Rais ni swala la ulinzi na usalama wa nchi na ndo maana utaona hakuna viongozi walokuwa wakiruhusiwa kumtembelea isipokuwa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.
 
Nimeshangaa pia:
  • Dar es Salaam walikuwepo watatu: CDF, IGP & DGIS
  • Makamu wa Rais alikuwa Tanga, Waziri Mkuu alikuwa mkoani (Dodoma or elsewhere)
  • Lakini Waziri Mkuu aliitwa na alipata taarifa mapema, kabla ya Makamu wa Rais
Something is fishy here.
Inasemwa VP alilazimishwa kufanya ziara Tanga ili kuwekwa mbali
 
Chain of command
PRESIDENT >>V. P>>P. M huyo CDF ni mbali Sana anaripoti kwa waziri wa Ulinzi, Inakuwaje top secret ifahamike na CDF halafu VP na PM wasijue?

Pengine mwendazake alihisi kuna wasaliti hivyo akaamua kuvunja chain of command??
 
Magufuli aliweza kuagiza Mapadri waende, lakini alishindwa kuagiza aitiwe Makamu wake, hata amuachie wosia juu ya Majukumu anayomuachia, naona bado kuna vumbi halijatuama, nasubiri story zaidi.
Hukusikia hotuba ya Mabeyo Chato? hukusikia akimweleza Rais kwamba Hayati alimdokeza kitu atamuona ofisini ampe ujumbe wake? weupe upstairs kabisa.
 
Magufuli aliweza kuagiza Mapadri waende, lakini alishindwa kuagiza aitiwe Makamu wake, hata amuachie wosia juu ya Majukumu anayomuachia, naona bado kuna vumbi halijatuama, nasubiri story zaidi.
Yaani kweli unaona sasa unakufa na una nafasi ya kutubu. Umuite Kiongozi umwachie wosia wa namna ya kuendelea na majukum na uache njia ya kutengeneza njia yako huko uendako? Inashangaza sana.
 
Somebody taught me this one day somewhere..

Akaniambia ni vyema kama ndugu mna mgonjwa wenu amelazwa hospitalini, asubuhi mnapokwenda kumuona msiache mwanamke aende peke yake, lazima aambatane na mwanaume, ili kama mgonjwa akiwa na hali mbaya sana, au bahati mbaya ameshafariki, basi mwanaume awepo ili kumtuliza mwanamke, wanawake hawawezi kujizuia kwenye vilio, wanalia mpaka unajiuliza hivi huyu atanyamaza kweli...
Siyo tu hivyo,hata ktk familia km mtoto wa kiume ni mkubwa au wa kwanza kuzaliwa na tayari walau ana umri wa miaka 20+ na amefunzwa vyema,amekuwa karibu na baba yake,baba akisafiri anakabidhiwa mkuki,upinde na mishale yake halafu mama yake anakuwa kiongozi kivuli ijapo huwa hawajui kuwa wao ni viongozi vivuli.
 
Back
Top Bottom